Baada ya kupita kwa miaka mingi tangu Ashanti na Ja Rule waliposhirikiana kufanya wimbo wa pamoja – sasa wawili hao wamekutana tena kwenye wimbo mpya ‘Helpless’ wa Ashanti aliomshirikisha Ja Rule. Usikilize hapa chini.
NYUMBANI KITAIFA
Ulimwengu wa habari.
KATIKA BIASHARA
Ulimwengu wa habari.
MATAIFA MENGINE
Ulimwengu wa habari.
KATIKA BURUDANI
Ulimwengu wa habari.
MAAJABU DUNIANI
Ulimwengu wa habari.
Saturday, November 26, 2016
RAIS ZA ZAMANI WA CUBA, FIDEL CASTRO AFARIKI DUNIA
2:17 AM
No comments
RAIS wa zamani wa Cuba na kiongozi wa mapinduzi ya kikomunisti, Fidel Castro amefariki akiwa na umri wa miaka 90, mdogo wake Raul ametangaza.
Amefariki usiku wa saa nne na dakika 22, kwa mujibu wa Rais Raul Castro.
Fidel Castro aliiongoza Cuba kama nchi ya chama kimoja kwa takriban miaka 50 kabla ya Raul kushika madaraka mwaka 2008.
Mazishi yake yanafanyika Jumamosi hii kwa mwili wake kuchomwa moto. Kutakuwepo na siku kadhaa za maombolezo ya nchi nzima.
Friday, November 25, 2016
RAIS MAGUFULI - 'WATU KIBAO WAMEKIMBIA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI'
9:13 AM
No comments
Na Emmy Mwaipopo
RAIS Dkt John Pombe Magufuli amesema zoezi la uhakiki wa vyeti litaendelea nchini na kudai kuwa wakati limeanza wengi walikimbia.
Dkt Magufuli aliyasema hayo jana wakati wa Mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) yaliyofanyika Kampasi Kuu iliyopo Bungo, wilayani Kibaha, Pwani.
“Wakubwa wenu wa section kule ambapo mnapangiwa kazi wahakikishe wanawapa promosheni mara moja kwasababu kama ni elimu mmeshapata wasiwatafutie visingizio. Nyinyi mmetoka, wapo watu kule hawana hata vyeti na ndiyo maana tulipoanza zoezi la ukaguzi wengine walichukua malikizo ya moja kwa moja,” alisema.
“Nilitegemea watachukua likizo ya kuja kusoma wamepotea, na zoezi hili la kukagua vyeti lazima liendelee ili wasomi kama nyie mliosotea elimu yenu mkafaidi matunda ya elimu yenu,” aliwapa moyo.
“Haiwezekani wewe uliyesoma hapa unakwenda mtu anayekuongoza kumbe ni kilaza hana chochote, kwahiyo ndiyo maana nawapongeza sana wahitimu. Mmefanya kitu kizuri, mmeamua vizuri na serikali itahakikisha inawasimamia kuhakikisha mnakwenda vizuri na hiki ndicho tunachokitaka.”
“Tunataka mtu kama una elimu yako ya form four sema mimi ni form four kama ni form six sema ni form six, kama ni graduate sema ni graduate sio kwamba udanganye kwa mavyeti ya kuprin, nenda na wewe ukasome ukaone shida yake.”
MWANA FA AONYA KUHUSU BIFU ZINAZOENDELEA BONGO ‘TUNAKOELEKEA TUTATOANA MACHO’
9:04 AM
No comments
MWANA FA ameonya kuhusu bifu zinazoendelea kwenye muziki wa Bongo Flava kwamba zinakoelekea, watu wanaweza kufanyiana vitu vya hatari zaidi.
Akiongea kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV leo, FA amesema busara zinahitajika kumaliza tofauti baina ya wasanii wanaohusika kwenye bifu hizo.
“Tufike mahali kwamba tujiwekee mipaka kama binadamu kwamba hivi vitu ambavyo tunaambiana kama ungekuwa unaambiwa wewe na familia yako ingekuwa sawa? Maana yake tunavyoelekea tutatoana macho hivi karibuni,” alisema rapper huyo.
“Watu pekee wanaoweza kufanya ni wao wenyewe wanaohusika. Nafikiri watu wawe humble, warudi chini kidogo, wanaelea sana juu, turudi chini kidogo, tujikumbuke sisi nani na kama malengo yetu ni kutoana roho ama kuendelea kufanya muziki tuweze kujitengenezea vipato,” amesisitiza.
Ushauri wa Mwana FA umekuja katika wakati ambao uhasama kati ya kambi ya Diamond na Alikiba unazidi kushika kasi.
Rapper huyo ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Dume Suruali’ aliyomshirikisha Vanessa Mdee.
HATIMAYE MOHAMMED HUSSEIN AMALIZANA NA KLABU YA SIMBA SC
9:02 AM
No comments
MCHEZAJI wa klabu ya Simba SC ambaye anacheza nafasi ya beki wa pembeni Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ hatiamye amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na nusu katika klabu ya Simba ambao utamalizika mwaka 2019.
Mchezaji Mohammed Hussein akisaini mkataba mpya akiwa na Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva
CALISAH - 'NIPO TAYARI KUFUNGWA ENDAPO ITAJULIKANA NILISAMBAZA VIDEO YA KIMAHABA NA WEMA SEPETU'
8:56 AM
No comments
CALISAH ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali katika kipindi cha Weekend Gossip kinachorushwa na kituo cha runinga cha TV1 siku ya jumamosi (19 Nov, 2016).
Katika kipindi hicho kinachoruka hewani kila jumamosi saa 3:30 usiku, mtangazaji Mimi Mars alimuuliza kuhusu mkanda wa video uliosambaa unaomuonesha akiwa katika wimbi zito la mahaba na mwanadada huyo maarufu nchini wakinyonyana ndimi.
''We do have pictures me and her, and those pictures nilikuanazo mimi na yeye, only two of us, kwahiyo isingekuwa rahisi wema kama wema kuleak zile picha'' alisema.
Calisah akaendelea kwa kusema kuwa yeye mwenyewe pia hakuvujisha kwa makusudi zile picha kama inavyosemekana na watu wengi.
''Mimi pia sijaleak zile picha na hamna mtu yeyote niliyemuachia simu yangu''
Calisah akaenda mbali zaidi kwa kusema yupo tayari kufungwa endapo itabainika kuwa yeye ndiye aliyesambaza picha na mkanda huo wa video.
Msikilize Calisah akihojiwa hapo chini kisha tupe maoni yako kuhusu sakata hili.
SERIKALI YATOA TAHADHARI JUU YA UGONJWA WA HOMA YA MANJANO NA DALILI ZAKE
8:47 AM
No comments
WANANCHI wametakiwa kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa homa ya manjano huku akisema licha ya ugonjwa kutoingia nchini, wananchi wanapaswa kupata chanjo ili kuepuka homa hiyo.
Akizungumza jijini Dar es salaam, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambapo amesema kuwa wananchi wanatakiwa kupata chanjo ili kuepuka kupata ugonjwa huo.
“Ugonjwa huu wa homa ya manjano bado haujaingia nchini kwahiyo kwao ni motisha hata mtu anasafiri au anajihusisha na masuala ya utalii na uwindaji ni motisha kwao kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa manjano. Na pia nitoe rai kuepuka au kupokea vyeti bila kupata chanjo kwani kufanya hivyo kuna hatarisha maisha yako na ya watu wengine na chanjo hizo zinapatikana katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ,uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) na uwanja wa ndege wa Mwanza lakini pia bandarini, bandari ya Dar es salaam, bandari ya Tanga, bandari ya Mwanza, bandari ya Kigoma na mipaka ya nchi kavu, Morogoro, Namanga, Holili, Tarakea na Sirari,Kasumulu, Tunduma na Dar es Salaam. Pia tumeweka katika kituo cha afya cha Mnazi mmoja,” alisema Mwalimu.
“Wizara inatoa onyo kwa vituo vinavyotoa chanjo hii bila kibali kuacha mara moja lakini kwa upande wetu sisi wizara tuna wajibu wa kuhakikisha chanzo hizi zinakuwa katika vituo hivyo hivyo ambavyo tumevipa mamlaka ya kutoa chanjo hizo,” alionya.
Aidha Waziri Ummy alitoa dalili za ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na, “kuwa na homa, kuumwa na kichwa, maumivu ya misuli pamoja na maumivu ya mgongo,mwili kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kusikia kichefuchefu, kutapika na mwili kuwa na manjano. Dalili nyingine ni kutokwa na damu sehemu za wazi mdomoni, puani, machoni, masikioni pia wakati mwingine damu huonekana kwenye matapishi, kinyesi na figo kuacha kufanya kazi kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa huu wa manjano ni kati ya siku 3 hadi siku 6 baada ya kuambukizwa. Ugonjwa wa homa ya manjano hauna tiba kamili lakini kinachotibiwa ni zile dalili ambazo zinatokana na homa ya manjano hivyo mtu akiupata ugonjwa huu anaweza akapoteza maisha kama hajapata huduma za afya mapema,” alisema.
“Habari njema ni kwamba ugonjwa huu una chanjo ambayo mtu akipata kinga asipate maambukizi na chanjo hii imekuwepo kwa muda mrefu na imethibitishwa na shirika la afya duniani kuwa na uwezo wa kumkinga mtu dhidi ya maambukizi ya virusi.”
MSIKILIZE RAIS MAGUFULI AKIONGEA MUBASHARA NA MAKONDA KWENYE MKUTANO MBELE YA WANANCHI *AUDIO*
8:44 AM
No comments
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amempigia simu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuongea naye ‘live’ akiwa katika mkutano wa ziara yake ya wilaya ya Ubungo ya kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kuzitatua.
Makonda alimpigia simu mkuu huyo wa nchi ili kuomba ufafanuzi juu ya changamoto za wananchi wa Ubungo hasahasa kwa wale ambao wanabomolewa nyumba kutoka na utanuzi wa barabara.
Tuesday, November 22, 2016
SIKILIZA BRAND NEW MUSIC TOKA KWA MWANA FA FT VANESSA MDEE – DUME SURUALI
9:11 AM
No comments
BAADA ya kufanya vizuri na ngoma ya ‘Asanteni kwa Kuja”, Mwana FA ameachia ngoma yake mpya, ‘Dume Suruali’ aliyomshirikisha Vee Money. Producer ni Daxo Chali.
CHIKUNE WA NAMIBIA AMTAJA MSANII WA BONGO FLEVA ALIYEFANYA NAYE KOLABO
9:07 AM
No comments
MSANII Chikune kutoka Namibia amethibitisha kufanya kolabo na msanii wa Bongo Fleva.
Muimbaji huyo ambaye amefanikiwa kushinda tuzo ya Afrimma mwaka huu ameiambia Bongo5 kuwa tayari ameshafanya kolabo na msanii mmoja wa kike kutoka Tanzania ambaye anatarajia kupata connection za huku.
“Kwa kuanzia nimeshafanya kolabo na Kleyah. Ni msanii wa pekee sana na anaangalia zaidi biashara na naamini ana nafasi kubwa ya kwenda sambamba kwenye tasnia ya muziki iliyotawaliwa na wanaume. Lakini pia tumeweza kuunganisha elimu kwa pamoja,” amesema Chikune.
Chikune ameongeza kuwa ana mipango ya miaka mitatu mbele ya kuitangaza brand yake Afrika na kuufanya muziki wa Namibia kujulikana zaidi.
CLEMENT SANGA ATHIBITISHA MZAMBIA GEORGE LWANDAMINA NDIYE KOCHA MPYA
9:02 AM
No comments
MAKAMU mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga amethibitisha kuwa Mzambia George Lwandamina ndiye kocha mpya wa timu hiyo akichukua mikoba ya Mholanzi,Hans Van Pluijm.
Lwandamina,53,ambaye alikuwa ni kocha wa Zesco United ya Zambia, ataanza kukinoa rasmi kikosi hicho cha jangwani katika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara.
Pia Sanga amesema kuwa Hans Van Pluijm ataendelea kuwa klabuni hapo kama Mkurugenzi wa benchi la Ufundi na kocha msaidizi Juma Mwambusi ataendelea kuwa katika nafasi hiyo mpaka itakapotangazwa vingine.
MADHARA YA CHAI NA KAHAWA KIAFYA
8:58 AM
No comments
Kafeina ni nini?:
1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’.
Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina.
Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini.
Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya.
2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics).
Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio cha chai, kahawa au soda.
Madhara yake ni nini?, Moja; kama unakunywa kinywaji na muda si mrefu unalazimika kwenda kukitoa inamaanisha kinywaji hicho hakikutumika vema na mwili. Pili; kumbuka ulikunywa kikombe kimoja na umeenda kutoa viwili, hivyo umekopwa maji mwilini mwako na ukumbuke kuwa MAJI NI UHAI.
3. Kafeina husababisha KANSA.
Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini. Kafeina yenyewe ni asidi, hivyo ikiwa mtu anafanya chai au kahawa ndivyo vinywaji vyake vya kila siku basi mtu huyo lazima atakuja kupatwa na kansa katika siku za usoni kwakuwa seli za kansa huishi katika hali ya uasidi pekee na kafeina ndimo mazingira mazuri ya kuishi asidi.
Jarida moja la afya la Uingereza, ‘The British Medical Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishwaji wa mkojo.
4. Kaffeina huchangia upotevu wa madini na vitamin mhimu mwilini.
Kafeina ambayo ni kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.
5. Kaffeina husababisha kisukari.
Mwili una vyanzo 3 vya nguvu ambavyo ni Sukari, Mafuta, na Maji/Chumvi. Tumesema kaffeina ni kikojoshi, hivyo kaffeina hupelekea upotevu usio wa lazima wa maji mwilini, mwili unapokosa maji kama chanzo chake cha nguvu, moja kwa moja huhamia kuitegemea sukari kama chanzo chake cha nguvu na mwishowe kisukari lazima kitokee.
6. Uchovu sugu.
Wapenzi wengi wa chai ya rangi na kahawa mara nyingi wanapojisikia uchovu hukimbilia kikombe cha kahawa au chai. Kaffeina iliyomo katika chai au kahawa huenda kuiamsha na kuitumia nguvu iliyokuwa imehifadhiwa na mwili kwa ajili ya matendo ya dharura na kukuacha wewe ukiwa huna nguvu ya ziada kwa ajili ya kazi za dharura, matokeo yake ni mwili unakuwa upo katika hali ya msukosuko muda wote.
Utolewaji wa sukari iliyokuwa imehifadhiwa, kunapelekea mfadhaiko mkubwa kwenye mfumo wa dharura wa mwili. Unaposhitushwa kidogo tu, unakuwa na nguvu za haraka (Unahamaki) kushughurika na tatizo. Hali hii hatimaye inaweza kupelekea kukauka kwa tezi ya adreno kutakakosababisha damu chache yenye sukari (hypoglycemia), udhaifu, na kuumwa sana iwapo sukari haitachukuliwa mapema kupandisha juu damu sukari.
Kwa sababu ya biashara kuunda vyakula vyetu vyote maalumu na vinywaji vyenye radha mpya, radha nzuri na nguvu ya kutosha kwa kutumia kafeina toka katika mimea na mitishamba kama vile ginseng kuisisimua tezi ya adreno, kunasababisha Ini kutoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa mwilini kwa ajili ya matumizi yake ya dharura.
Hakuna nguvu iliyomo kwenye kafeina au ginseng. Kuna majina mengine mengi ya visisimuwaji hivi kama vile, kokwa za guru, kokwa za cola na mfalme wa yote ni guarana. Mbegu za guarana zina kiasi cha kafeina mara tatu zaidi ya zile za kahawa, na hawatakiwi kuliorodhesha neno kafeina kwenye vifungashio (packages) au kontena.
Ungaunga wa guarana hutumika kutengenezea vidonge vya kupunguza uzito kwa sababu kafeina itazisambaratisha hisia za njaa, lakini hakuna mahala neno kafeina linaonekana kwenye vifungashio vya dawa hizi.
Kuna mimea, kokwa na kemikali nyingi ambazo zitaisisimua tezi ya adreno na kusababisha ini kuitoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa au hata kuitengeneza toka tishu za mwili wenyewe ‘(gluconeogenesis)’.
Imethibitika pia kuwa kafeina imekuwa ikiingilia na kuathiri unakilishaji wa kinasaba (DNA), namna ambavyo seli mpya hutengenezwa. Kafeina inaweza kusababisha upotevu toka mwilini wa vitamini nyingi za kundi B, kundi C, zinki, potasiamu na madini mengine. Kahawa huongeza hali ya uasidi kwenye utumbo mdogo.
Kafeina inaweza kusababisha msukosuko ndani ya mwili.
Kafeina siyo kwamba tu huimaliza nguvu iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ubongo, bali pia huzuia mfumo vimeng’enya katika kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo.
Kituo cha Sayansi kwa maslahi ya umma (Center for Science in Public Interest) kimewashauri kinamama wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.
‘Madawa na wewe’, kwa mjibu wa Dr. Earl Mindell, mwandishi wa kitabu; ‘Earl Mindell’s New Vitamin Bible’ (zaidi ya nakala milioni 10 zimeuzwa), anasema katika ukurasa wa 414 wa kitabu hicho kuwa ‘kafeina ni dawa yenye nguvu kubwa, uwezekano ni kuwa, hauifurahii tu kahawa au cola yako ya kila siku, bali umekuwa mtegemezi au teja (addicted) wa hiyo kafeina’.
Madhara ya chai ya rangi na kahawa mwilini ni mengi sana na tatizo moja litapelekea lingine na orodha inakuwa haiishi.
Namna ya kuepuka kaffeina kwenye kahawa na chai:
Badala ya kutumia majani hayo ya chai meusi, wewe chemsha maji yako ya chai kama kawaida na unaweza kutumia vifuatavyo kukamilisha chai yako; unaweza kutumia tangawizi na kumbuka pia tangawizi ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini.
Kwahiyo unapoinywa chai ya tangawizi siyo tu unaepuka madhara ya kaffeina peke yake, bali pia unakuwa umekunywa dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!. Unaweza pia kuweka mdalasini, mchaichai, kukamulia ndimu, pia unaweza kutumia mchanganyiko wa viungo vingi vya chai (spiced tea) ambavyo vinapatikana kwa wingi katika soko la Kariakoo Dar – Es – Salaam na Zanzibar.
THE GAME AKUMBANA NA RUNGU LA MAHAKAMA
8:44 AM
No comments
MAHAKAMA imemshika pabaya The Game – imemuamuru kumlipa msichana aliyemnyanyasa kijinsia dola milioni 7.
The Game alidaiwa kumnyanyasa msichana huyo ambaye ni mwanamitindo anayefahamika kwa jina la Priscilla Rainey kupitia kipindi chake cha runinga mwaka jana.
Priscilla Rainey anayedaiwa kudhalilishwa kijinsia na The Game
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mahakama imemuamuru rapper huyo kulipa kiasi cha dola 7.13 milioni. Miezi tisa iliyopita The Game aliandika ujumbe kupitia mtandao wa Instagram unaopinga kumlipa mwanamitindo huyo.
Let’s get one thing very CLEAR: that thirsty Gatorade mascot of a transvestite WILL NEVER see $10,000,000 or anything close 2 a penny of my money. People think because they read a headline in BOLD PRINT it’s true. She won a judgment of 10 million $’s & that means that a judge because I’m overseas has given this chicken a chance 2 MAYBE be able to afford a lifetime supply of lace front hair glue if my lawyers don’t respond to this suit by the 26th of this month which they will do tomorrow am. Soon as I’m home, me & my lawyers will EAT THIS CASE like a box of Minion Twinkies on sale at Walmart ! @VH1 has a seperate suit filed against them by this Thot Bot that they will also win because #1 this BIYATCH (Snoop’s voice) is a liar. She has a history of theft, fraud, prostitution arrests & a lot of other “Tranny Panty” activity in her past that makes this false claim irrelevant. Don’t be fooled by these accusations or the dollar amount in the headlines cause I put that on my favorite aunties poodle this broad ain’t gettin shit ! Every girl on that show will tell u I never touched this chick or ever desired to be anywhere near her. She got kicked off the show & as a result she filed this lame lawsuit which was probably her intentions before the show was ever even started. She was begging for my attention the entire time we shot the show & was given the ultimate Major League Baseball CURVE ball so that upset her & made her lil wee wee hard so she did what all chicks like her do when life gives them no other options…. They sue you ! This is really a crying shame so at this point I will use the crying shame emoji . See you in court Mister Rainey. N I say Mr. because ur mustache is probably a bit longer than it was during taping being that it’s about to be spring & that’s usually when mine is at its healthiest, hit @Beboprbarber for the best mustache edge up u can find. Tell em I sent u & it’s on the house u dusty bitch you !#TellEmBoutThatScratchNSniffWigYouBeWearing #HairyAssUnderArms #BitchWasUsingMyOldSpice(insert old spice whistle) #PS #iHateAll17OfYoWigs#AndYesIFlushedUrClosurePieceDownTheWaffleHouseToilet take these #JuwannaMann
HANS VAN PLUIJM AKUTANA NA RUNGU LA TFF
8:37 AM
No comments
KOCHA wa Yanga, Hans van Pluijm ambaye saivi amepata cheo na kuwa mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo, amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu baada ya Kamati ya Saa 72 ya TFF kukaa na kubaini ana makosa anadaiwa kuwazonga waamuzi na kuwatolea maneno ya kashfa.
Pia baada ya mechi kumalizika alikwenda kwenye chumba cha waamuzi na kuwatolea maneno ya kashfa. Adhabu hiyo ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 40(1).
Klabu ya Yanga pia imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya washabiki wake kuwazonga waamuzi na kuwatolea maneno ya kashfa walipokuwa wakiingia vyumbani wakati wa mapumziko. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1).
MTV BASE YATOA ORODHA YA RAPPERS 10 WAKALI BONGO 2016
8:36 AM
No comments
KITUO cha runinga cha MTV Base kimeyataja majina ya wasanii kumi wa muziki wa Hip Hop kutoka Tanzania wanaofanya vizuri kwa sasa nchini.
Namba moja ya orodha hiyo imeshikiliwa na rapper Fareed Kubanda aka Fid Q huku kundi la Weusi likifanikiwa kuingiza wasanii watatu kwenye ordha hiyo. Tazama orodha kamili hapa chini.
1)Fid Q
2)Joh Makini
3)AY
4)Mwana FA
5)ROMA
6)Mr. Blue
7)Nick wa Pili
8)G Nako
9)Prof Jay
10)Chindo Man
2)Joh Makini
3)AY
4)Mwana FA
5)ROMA
6)Mr. Blue
7)Nick wa Pili
8)G Nako
9)Prof Jay
10)Chindo Man
AUGUST ALSINA AUMIZWA NA TUKIO LA KUZIMIWA MIC KWENYE TUZO ZA AMA
8:11 AM
No comments
MUIMBAJI wa Marekani, August Alsina ameumizwa vikali na tukio la kuzimiwa mic wakati akitumbuiza kwenye tuzo za AMAs mwishoni mwa wiki.
Katika post ndefu aliyoiweka kwenye Instagram, Alsina amesema kitendo hicho kimempa hofu zaidi kuhusiana na career yake.
Akiweka picha hiyo juu, msanii huyo aliandika:
Woke up to this message.. This Has bothered my spirit for the longest time , I’m more confused than yesterday.Is it because I’m new and that was my first introduction to the AMA world? Is it because I’m black and you don’t know what to expect ? Is it because of my past that you may be trying to bind me to ? Or
Is this pure hate and just to rob me of a moment? To make people think I’m lip syncing as if I’m not even a person who tries! Someone whose not serious about his craft. I’m from the bottom where if we don’t do anything else, we TRY! And last night I not only tried but DID & conquered & it’s as if it never happened. Someone help me understand.. Im sorry for rambling but I’m just confused.
I went into this with the most reverence for your establishment and platform only to be failed in return. You may have muted my mic to TV but you can’t mute reality and the infection of that crowd rock.
The response from people in that building afterward.
A really sweet older & very graceful white woman had an interaction after the performance on my way to the restroom & she said “wow, you were just magical up there, how do I not know you.” She then went on to apologize to me & said I’m sorry (which I was confused about) so I asked why for clarity. She said “with what I just saw and felt you should be lots of awards at this place”. I kindly smiled and said Thankyou with the most gratitude & honor & formally introduced myself to her and went to shake her hand. She ended with “ohhhh trust me, I know who you are now.. You’re unforgettable”! So I am just completely and utterly confused.
Once again though, I will say Thankyou for the opportunity AMA’s.
Through it all, Allah keeps on blessing me. #DoUMind is the number one record in the country. God is my Solid Rock!
NISHER AKONGA MIOYO YA WATZ KATIKA FILAMU *VIDEO*
7:45 AM
No comments
NISHER alikaa kimya kwa muda na kupotea kiasi kwenye fani ya uongozaji wa video za muziki. Na sasa amerudi, lakini akiwa amekuja na kitu cha ziada kuongezea katika catalog ya kazi zake.
Siku chache zilizopita, muongozaji huyo mwenye makazi yake jijini Arusha alitoa filamu yake fupi aliyoipa jina ‘Alex.’ Inaelezea kisa cha kibarua mwenye jina hilo ambaye ana familia yenye mke na mtoto mmoja.
Lakini kutokana na kutegemea kibarua cha ujenzi chenye kipato duni, anajikuta akishindwa kuihudumua vizuri familia yake na kumfanya mke wake amchukulie tu kama mwanaume suruali. Hilo linampa stress sana lakini hana namna ya kuliepuka zaidi ya kukubaliana na ukweli.
Katika mazingira anayofanya kazi Alex anakutana na warembo wa kila aina kutoka kwenye familia za kitajiri ambao anaishia kuwatamani tu na shida zake zikibaki pale pale.
Alex imeonesha kuwavutia wengine wanaoamini kuwa kama ikiendelezwa inaweza kuwa series ya kuvutia. Haya ni baadhi ya maoni ya watu walioitazama.
Nchakalih
NISHER, this is very very encouraging work. Love the grading, the cinematography, the scoring…you can only go higher from here. very encouraging that tuna KIPAJI kama chako in TZ….keep PUSHING, wengi tunaweza kukosoa na sio wanaokosoa wote ni mahaters but for me…..UMETHUBUTU, UMEFANYA, UMEWEZA. Mengine, ntakutafuta chamber ila for now….YOU ARE ONTO SOMETHING FAM!
Beatrice Shelukindo
If U get serious enough Nisher, ALEX will get bigger than u can ever imagine. We’re looking forward to see more of ALEX episodes. Thanks X
Samwel Wilfred
Nia yangu sio kuonekana nakusifia au nakupaka mafuta kwa mgoingo wa chupa hapana film yako inautoauti mkubwa sana style ya shot na movie za kibongo ni short story ila inakufanya uwe na hamu ya kendelea kuiangalia iko tofauti sana japo kuna mapungufu machache ila almost epic mtengeneze alex afike mbali
Monicah Mugo
Coming from music background to films ain’t a something light. Simple story well executed. Apart from the continuity factors which have been contributed by the fact that most are first time actors and actresses, the cinematography portrays the emotions perfectly. The scoring and color is good. It stands out against the Bongo films commonly used style. You are a game changer and so is the way to go long. Is there a continuation? I wanna see how dramatic you wanna develop it. Cheers bro.
Makai Kasala
Story, video quality, actors.. Awesome.. I wish u do something big for the revolution of tz movies… Hope wadau wamekuona… Keep it live…
Daphne Munialo
Damn,I didn’t want Alex to end, is there anymore of Alex please?
Reply 1
Hezzron S. Josephs
Good work. Great story telling techniques
I love that part Alex is leaving his home Alafu hana hata ela ya kuacha nyumbani Ila hataki kuonyesha hio kwa mwanae. Still anamwambia ntamletea zawadi. That’s giving hope .
Ramadhani Hamisi
Great work, great and fascinating story with a strong message in it. I like that part at the cite where Alex was working, you’ve managed to capture some amazing shots and also show the hardships that low earners face like working without steel toe shoes, gloves and also helmets. I am fan of your work since day one, keep the hardworking moving and blessings will be on their way. Nice one Nisher, looking forward for the next move
AMANI CHANG’A
Haters won’t like it, here what should we appreciate most is the video quality, then about story and video content will be depending upon actors and story owners, Nisher z the video director with filming skills and not only music videos, so if he will get great actors with great stories I swear all over the world gonna know about Tanzania, let’s cooperate each other as Tanzanians and not making someone down so to make someone else a deal like fid q said in sumu
Jocelyn William
The video quality is very nice, characters are very realistic, the set is perfect I think it would make a very nice movie, I especially liked the fact that it didn’t feel like I was watching people act but rather I was viewing someone’s life which made it very interesting and the technology of showing what was going on on Monica’s phone is very creative nothing I’ve seen in any Tanzanian movie, keep up the good work, tengenezaga movie tu kaka angu, watazamaji tupo
MAUA SAMA - 'KUONDOKA KWA RUBY HAKUJAIUA PROJECT YA BUTTERFLY'
7:26 AM
No comments
MAUA SAMA amedai kuwa licha ya kuondoka kwa Ruby THT, kundi lao la Butterfly halijafa.
Maua ametoa taarifa hizo kupitia kipindi cha Vibe la Kitaa cha ABM Radio ya Dodoma kinachoendeshwa na Dj Rodger. Amedai kuwa kwa sasa kila member anafanya kazi zake za solo na amesema hivi karibuni kulikuwa na mambo mengi ikiwemo Fiesta.
“Project bado ipo hai na inaendelea na wakati wa msimu wa Fiesta tulikuwa tunaendelea kuipa promo kama kawaida na kulikuwa kuna project ya Kipepeo ambayo tulikuwa tunatembea kila shule katika mikoa tuliyopita kwenye Fiesta kwaajili ya kuwahiza wanafunzi ,” amesema Maua.
“Kwahiyo haimaanishi kuwa sababu Ruby ameondoka THT basi na project ya Butterfly imekufa, hiyo sio kweli,” amesisitiza.
Kundi hilo sasa limebakiwa na Maua, Nandy na Alice.
SABABU ZA MAKAMPUNI MAKUBWA YA TEKNOLOJIA KUNUNUA MAKAMPUNI MADOGO/YANAYOCHIPUKIA
7:23 AM
No comments
‘WhatsApp yanunuliwa kwa dola za kimarekani bilioni 19’, ’Facebook yainunua Instagram kwa shillingi za kitanzania trillioni…’ ni miongoni mwa vichwa vya habari ambavyo si vigeni sana kwenye macho yetu, kampuni fulani kununua kampuni nyingine.
Ni jambo la kawaida kwenye ulimwengu wa teknolojia lakini unajua sababu kuu zinachofanya kampuni hizi kumwaga mabilioni ya pesa zote hizo? (Tena kwenye Apps zinazopatikana BUREE kwenye app stores?!Natania kidogo) kaa hapa nikujuze:-
Kuinua thamani ya hisa na uwekezaji
Kampuni kama Microsoft,Google,Apple zimejiandikisha kwenye masoko makubwa ya hisa duniani kama NASDAQ na moja ya sifa kuu ya kuwa na uwekezaji wenye thamani na unaoongezeka ni kuwa na huduma au bidhaa zenye mvuto kwa watumiaji muda wote,hivyo basi kampuni hizi kubwa hupenda kuwahi bidhaa au huduma mpya zinazoelekea kukua kwa kasi ili kuvutia wawekezaji wao na wawekezaji wapya jambo ambalo huinua kwa kiasi kikubwa thamani ya hisa za kampuni husika,ndio maana kampuni hizi muda wote huwa macho kodo kuangalia kampuni mpya/zinazochipukia zinazoweza kukidhi matakwa yao na kuwapatia faida katika masoko hisa.
Taarifa za watumiaji
Kila kampuni ina mfumo wake na sheria katika kukusanya na kutumia taarifa mbalimbali za watumiaji wake(Mfano,namba za simu,barua pepe anwani makazi n.k)na kutokana na hilo haiwezekani kampuni moja kuazima au kuchukua taarifa za watumiaji wa kampuni nyingine bila watumiaji wenyewe kuhamisha,lakini vipi kama kampuni hizi zikiwa chini ya mmiliki mmoja? Hilo linawezekana na kufanyika kwa urahisi zaidi na ndio maana baada ya Facebook kununua WhatsApp walirekebisha sheria zao za taarifa za wateja na kuwapa mamlaka Facebook kutumia anwani za wateja wa WhatsApp na marafiki zao moja kwa moja.
Taarifa hizi ni muhimu sana sababu ndizo hutumika katika mambo mbalimbali kama uonyeshaji wa matangazo, habari na taarifa mbalimbali kwa mtumiaji. Pia taarifa hizi hurahisisha kujiunga kwa huduma fulani kupitia taarifa zilizokwisha tolewa kwa huduma nyingine(Kama kujiunga YouTube au kutumia Firebase kwa kutumia taarifa za akaunti ya Google moja kwa moja bila kuidhinisha)Au jinsi Google wanavyotumia taarifa zako ulizoweka kwenye kifaa chako cha android moja kwa moja katika ushawishi wa matangazo na uwasilishaji wa taarifa mbalimbali.
Kubadilishana mifumo teknologia (API)
Kipindi cha nyuma kabla Instagram haijanunuliwa na Facebook, picha zilizowekwa instagram zilionekana kama link zikiwa shared Facebook, hii ni kwasababu kushea mifumo teknolojia (API) kuna mipaka yake, lakini daraja hili linaweza kuvukwa kama kampuni hizi zikifanya kazi pamoja na kuwa na uwezo zaidi ya unaoruhusiwa na API, ndio maana baada ya Facebook na Instagram kuwa kampuni moja picha za Instagram zinaonekana moja kwa moja Facebook endapo tu mtumiaji akitaka (Share)
Pia, ubadilishanaji mifumo huo ndio unaofanya iwezekane kulipia, kuandaa na kuangalia maendeleo ya matangazo ya Instagram kwa kupitia akaunti ya Facebook ya muhusika au kualika marafiki wa Facebook katika group la WhatsApp kupitia link moja kwa moja.
Kuendana na mabadiliko
Teknolojia kwa kiasi fulani ni kama fasheni, sababu vyote hubadilika badilika na hubadilika bila utabiri wa kitu gani kitakuwa na uhitaji zaidi.Hivyo inapotokea App fulani kutokea kupendwa na watumiaji huonekana kama bakuli la dhahabu, Instagram ilianzisha huduma ya video za sekunde kadhaa mwaka 2013 na ikaonekana ni kitu kipya sana na kuvutia, lakini huduma kama hiyo imekuwa ikitolewa na App ya Vine toka mwaka 2012 na kuonekana kawaida tu!
Periscope iliyoanzishwa 2015 ni App maarufu sana ya video za moja kwa moja lakini huduma kama hiyo imekuwa ikitolewa na Ustream, iliyokuwepo toka mwaka 2007!
Ubadilikaji huu na kutotabirika ndio unaofanya kampuni inayoonekana kupendwa kutafutwa sana na kampuni kubwa maana uanzishwaji wa huduma mpya kwa kampuni kubwa haumaanishi kufanikiwa kwake,hivyo ni bora kununua kitu ambacho tayari watu wameonyesha kuvutiwa nacho tofauti na kuiga na kukosa watumiaji wa kutosha.
Kukuza bidhaa/huduma
Android ni mfumo wa simu unaoongoza kwa umaarufu duniani ukifuatiwa na iOS, lakini pengine usingekuwa katika nafasi hiyo au ingechukua muda mrefu pasipo Google kununua mfumo huu mwaka 2005, sababu ya jina na uwezo wa Google, wingi wa wataalam iliyonayo imewezesha mfumo huu kuwa thabiti na wenye ushindani zaidi kwa iOS kuzidi hata mifumo iliyokuwa na nguvu kabla yake kama BlackBerryOS ya BlackBerry na Symbian ya Nokia zilizokuja kufa sababu ya ushindani mkubwa.
Uwekezaji huu wa Google ndio uliofanya Android kuwa na uwezo wa kutoa matoleo mapya kila mwaka na mabadiliko madogo madogo mara kwa mara kutokana na ushindani wa iOS wanaofanya hivyo pia, na ndio uliosaidia ushawishi kwa makampuni makubwa ya vifaa vya umeme kama Samsung na mengineyo kuwaamini na kufanya mfumo huo kuwa wa lazima kwa vifaa vyao na kuufanya pia uwe utanuke kutoka kwenye matumizi ya simu pekee mpaka kwenye vifaa vingine kama saa za mkononi na vifaa vya nyumbani kama jokofu, runinga na mashine za kufulia.
Utaalamu
Aliyekutangulia amekutangulia tu, kampuni kubwa zina uzoefu, wataalamu, miundombinu ya kutosha. Sababu ya ukubwa waliyonayo unazofanya wawe na wataalamu wa hali ya juu wanaolipwa pesa ya kutosha.
Hivyo kununua kampuni ndogo waliyovutiwa nao huwa ni ahueni fulani kwa kampuni hiyo kulingana na malengo yake ya kukua au kuongeza watumiaji, utaalamu huu husaidia katika kuboresha huduma za kampuni, kuongeza watumiaji na masoko pamoja na huduma nyingine, kampuni ya Firebase inayojihusisha na uhifadhi database iliyoanzishwa mwaka 2011 mpaka kufikia mwaka 2014 ilikuwa na watumiaji 110,000 lakini mwaka mmoja na nusu baada ya kununuliwa na Google ilipanda na kuwa na watumiaji zaidi ya 450,000!
Hivyo kwa kampuni yenye malengo ya ukuaji wa haraka kununuliwa na kampuni kubwa huwa ni jambo la neema.Pia utaalamu huu husaidia kupanua teknolojia husika katika kuwezesha kutumika katika mifumo tofauti na mazingira mbalimbali kutokana na ushawishi na nguvu ya kampuni mama.
Fedha/vipande
Pengine hili ndio jambo ambalo huzingatiwa sana wakati wa manunuzi haya, sababu kwanza…inaposemekana kampuni imenunuliwa sio kwamba imechukuliwa moja kwa moja toka kwa waanzilishi! Manunuzi ya kampuni yanahusisha uhamishaji wa teknolojia, taarifa na mfumo mzima wa wafanyakazi na utendaji toka kampuni inayonunuliwa kwenda kampuni nunuzi,ikimaanisha kwamba maamuzi makuu kuhusu bidhaa/huduma hiyo yatatoka katika kampuni mama lakini waanzilishi wa kampuni inayonunuliwa hupewa kiasi fulani cha pesa kutokanan na maelewano na thamani ya huduma/bidhaa husika pamoja na uwekezaji wa vipande hisa katika kampuni mama, hii ni katika kuhakikisha kuwa hata kama huduma/bidhaa iliyofanya kampuni kununuliwa ikiisha thamani au ikikosa watumiaji waanzilishi bado watakuwa wana hisa katika kampuni mama pamoja na uwezo wa kutoa maamuzi katika bodi kuhusu huduma/bidhaa nyingine na pia kuendelea kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Kuwa na bidhaa ya tofauti
App inapokua kwa kasi na kupata wateja wengi hujipanga kwa ajili ya kupata faida kutokana na mtaji mkubwa wa watumiaji wake, lakini ili kuwa na uhakika zaidi na kujihakikishia wateja wa aina tofauti tofauti huitaji kuwa na huduma yenye utofauti kidogo na bidhaa/huduma yake iliyozoeleka kuliko kujiweka kwenye box la huduma/bidhaa moja.
Ndio maana kampuni kama Snapchat iliamua kununua kampuni inayochipukia ya Spectacles inayojihusisha na utengenezaji wa miwani zenye uwezo wa kupiga picha sababu Snapchat kama kampuni inajiandaa kuingia kwenye soko la hisa(IPO) hivyo lazima ijitanue tofauti na huduma ya application za simu pekee ambayo pengine inafanya itumike sana na tabaka la aina moja sana kuliko matabaka mengine(Vijana) na ununuzi huo kupanua wigo na tabaka la watumiaji na huduma, sababu watumiaji wa spectacles kabla haijanunuliwa watahama na ununuzi huo hivyo Snapchat kuongeza mtaji wa watumiaji na utanuzi wa huduma zake.
Uzoefu
Mwisho wa yote hii ndio sababu kuu inayofanya kampuni kubwa kuwa na kiburi na uwezo wa kununua kampuni changa/zinazochipukia, hapa nazungumzia uzoefu katika nyanja zote za kiteknolojia, biashara, mawasiliano, ujuzi na kila kitu kuhusu huduma na hali ya soko.
Kampuni iliyokuwa na muda mrefu kwenye soko ina uzoefu wa kutosha kuhusu bidhaa/huduma pamoja na mambo mengine kadha wa kadha ambayo kampuni ndogo hukosa na hivyo kutoa mwanya wa kununuliwa ili kulinda ukuaji wake,mfano kampuni ya kutengeneza michezo ya simu ya King yenye michezo maarufu kama Candy Crash Saga,Pet Rescue Saga na mengineyo,baada ya kupata faida ya kutosha kutokana na mauzo ya michezo hiyo iliamua kuingia kwenye soko la hisa kwa kuweka vipande vyake hadharani(IPO)
Lakini kinyume na utabiri wa thamani, ununuzi halisi ulikuwa sio wa kuridhisha na sababu kubwa ni wanunuzi na wawekezaji wengi kutokuwa na imani kwamba kampuni hiyo ingeendelea kupata faida kwa muda mrefu na kwa kutegemea huduma moja tu ya michezo pekee tena inayofanana ,jambo ambalo pengine lingeepukika kama King wangekubali kununuliwa mapema waingie kwenye soko chini ya mwamvuli wa wazoefu,uwekezaji ungekuwa maradufu na faida ingeongezeka somo lililokuja kuwaingia baadae sana na kuwafanya wakukubali kununuliwa Februari 2016 na Activision ambao ni maarufu na wazoefu wa miaka mingi kwenye kutengeneza michezo mbalimbali ya kompyuta.
Baraka W. Mgalula
Twitter: Barker5lime
Twitter.com/Barker5lime
OLE SENDEKA - 'TUNAHESHIMU MAAMUZI YA MOSES MACHALI KUHAMIA CCM'
7:18 AM
No comments
BAADA ya kutolewa taarifa ya aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Kasulu Mjini, Moses Machali kuhusu kuunga mkono serikali ya awamu ya tano hivyo na kujiunga na Chama cha Mapinduzi, Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ole Sendeka amezungumzia uamuzi huo.
Haya ndio machache aliyoyatoa Msemaji wa Chama cha Mapinduzi baada Machali kuhamia CCM akitokea chama cha ACT.
“Sisi kama chama cha mapinduzi tunaheshimu uamuzi wake na hatua ya pili kumpokea kwenye chama katiba za kikanuni zitafuatwa na hasa ukizingatia mimi namfahamu ni mtu mwenye msimamo, kwahiyo naheshimu maamuzi yake na hatua zingine zitafuata kwa mujibu wa katiba na kanuni zetu za chama kuwapokea wananchama wanaoingia katika chama chetu kutoka upande wa vyama vingine,”amesema Sendeka.
Taarifa ya aliyekuwa mbunge wa Kasulu Mjini imetolewa na kiongozi huyo yeye mwenyewe.
JERMAIN DEFOE AFIKISHA IDADI YA MABAO 150
7:12 AM
No comments
MCHEZAJI wa klabu ya Sunderland, Jermain Defoe ameungana na watabe wengine wa soka ambao wamefikisha idadi ya mabao 150 kwenye historia ya mashindano ya ligi kuu England.
Siku ya November 19 Defoe amekuwa ni mchezaji wa 8 kuungana na wengine kwenye historia hii mara baada ya kuifungia klabu yake ya Sunderland FC bao moja kwenye ushindi wa mabao 3 dhidi ya klabu ya Hull City.
Hii ndo idadi ya wafungaji wengine
RAY J AMDISS KIM KARDASHIAN KWENYE WIMBO WAKE MPYA ‘FAMOUS’
7:10 AM
No comments
MUIMBAJI wa RnB Marekani, Ray J amemdiss Kim Kardashian kwenye wimbo wake mpya ‘Famous (Kim Kardashian Diss)’ aliomshirikisha Chris Brown.
Kwenye wimbo huo Ray J amerap, “She fucked me for fame, look in her eyes. She was the first one to sign on the line / She was the real one to plan it all out / Look at the family, they walk around proud / All because she had my dick in her mouth.”
Naye Chris amepigilia msumari kwenye baadhi ya mashairi ya wimbo huo kwa kuimba, “I bet me and Ray J would be friends if we ain’t love the same bitch. Yeah, he might’ve hit it first / Only problem is I’m rich.”
Jina la wimbo limetoka kwenye wimbo wa Kanye West aliouachia mwezi Juni mwaka huu ambao video yake ilizua utata huku Ray J akionekana ndani ya video hiyo.
Ray J na Kim waliwahi kuwa wapenzi kabla ya Kanye kung’oa jiko.
Subscribe to:
Posts (Atom)
ZILIZOSOMWA ZAIDI
-
Bondia Pacquiao amerejia nyumbani Ufilipino baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega huko Marekani ambapo pamoja na kushindwa Floyd ...
-
ZILE picha za mahaba za msanii wa Hip Hop Bongo, Nay Wa Mitego akiwa na msichana kitandani zimezua balaa kwa mama mtoto wake Siwema Eds...
-
Walter Mguluchuma, Sumbawanga. MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Richard Tha...
-
Staa wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiingia ukumbini na kigauni kilichoacha sehemu kubwa ya kifua wazi. MASTAA wawili Bongo wali...