NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Sunday, March 6, 2016

RAIS MAGUFULI AMTEUA BALOZI JOHN WILLIAM KIJAZI KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Kabla ya Uteuzi huo, Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.
Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
06 Machi, 2016.

CHID BENZ: SIPENDI KUUSIKIA WIMBO ‘DAR ES SALAAM STAND UP’

Msanii Chid Benz amesema huwa hapendi kuisikiliza nyimbo yake ya Dar es salaam Stand Up na kwamba hata anapo ‘perform’ jukwaani hujisikia vibaya.
Chid Benz ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema ukubwa wa wimbo huo unamuumiza hisia zake, hivyo hujisikia vibaya kila anapousikiliza.

“Hii nyimbo sipendi kuisikiliza kwa sababu inaniumiza ni ngoma kubwa flan kubwa sana, hata nikiwa na perform ile watu wanashangilia , kelele nini ndiyo inanipa ushindi ila inanipa hisia tofauti”, alisema Chid Benz.

Chid Benzi amesema ngoma hiyo aliiachia kwa baraka za mama yake, baada ya kumuambia aitoe kwani ndiyo ilikuwa ngoma bora kati ya nyimbo 80 alizokuwa amerekodi kabla haijatoka.

“Dar es slaam stand up ilikuwa ndani ya nyimbo hizo 80 nilizorekodi, siku moja mama yangu akaniambia ule wimbo unaoanza unalia tttt uko wapi? nikamwambia, ngoja nikutafutie, akaniambia hii itoe, nzuri hii nikaichukua nikaipeleka kwa Duly nikamkuta Pancho, nikamuita Ditto akaja kuweka sauti na tukaifanyia kazi”, alisimulia Chid Benz.

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI MJINI ATEMBELEA MASOKO

Mbunge wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akisalimiana na wafanyabiashara wa soko la Pasua alipofanya ziara ya kutembelea masoko yaliyopo katika mji wa Moshi kusikiliza kero za wafanyabiashara hao.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya wakitembelea soko la Mbuyuni kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kuona namna bra ya kuboresha masoko hayo.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akimsikiliza kiongozi wa soko la Mbuyuni aliyefahamika kwa jina la Lameck ,wakati Mbunge huyo alipofanya ziara ya kutembelea masoko ya mjini Moshi akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,Raymond Mboya.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya wakitembelea soko la Mbuyuni kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kuona namna bra ya kuboresha masoko hayo.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya wakitembelea soko la Majengo  kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kuona namna bra ya kuboresha masoko hayo.

CHADEMA WATOA TAMKO KUHUSU KUAHIRISHWA UCHAGUZI WA MEYA DAR...'HATUTASUSIA UCHAGUZI MPAKA KIELEWEKE'

Uchaguzi wa Meya Dar es salaam unazidi kuchukua headline kila siku. Ikiwa jana tu Baadhi ya Wabunge na Madiwani wa Ukawa walitinga ofisi ya Halmashauri  ya jiji kutaka kujua tarehe ipi uchaguzi utafanyika lakini hawakupata majibu hayo. Leo March 5 2016Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA‘ Taifa, Freeman Mbowembele ya Waandishi wa habari ameyazungumza haya….

’Hatutaomba tena kumpata Meya wa jiji la Dar es salaam, tutadai kumpata Meya, Serikali wasifikiri watapanga wao tarehe ya kumchagua Meya, wamekuwa na utaratibu wa kutaka tarehe ya kumchagua Meya kwa kutushtukizia masaa 24 kabla, kanuni inadai siku saba, tutataka tarehe ya kuchagua na siku hiyo atachaguliwa Meya asipochaguliwa Meya siku hiyo tusilaumiane’:-Freeman Mbowe

Aidha Mbowe ametoa msimamo wa  chama alipoulizwa kama watasusia uchaguzi, haya ni majibu yake…


’hatuwezi kususia uchaguzi wa Meya kwa sababu ni haki yetu kuongoza jiji kwa sababu ni maamuzi ya wananchi kwa hiyo hatuwezi kususa maamuzi ya wananchi’:-Freeman Mbowe

NDOA YA RAYUU CHALI BAADA YA WIKI MOJA TU..KISA SKENDO CHAFU ZA MAGAZETI

Baada ya kutamba kuwa tayari amepata mume wa maisha, mambo yameharibika msanii wa filamu Rayuu, kwani sasa hatoki nje wale hapokei simu za shoga zake.

Wiki moja iliyopita msanii huyo aliiteka mitandao ya kijamii hasa instagram, kwa picha zake za harusi huku akiwa na bwana ake ambaye sasa si bwana tena.

Chanzo kikubwa cha kuvunjika kwa ndoa hiyo inadaiwa kuwa mwanaume ambaye alimuoa ni mume wa mtu, ambaye tayari mke wake ana ujauzito wa miezi mitatu, lakini pia inadaiwa kuwa ni kutokana na matukio kadhaa ya msanii huyo.

Rayuu alitafutwa ili kujibu tuhuma za kuachika, alijibu yote ni matokeo na kuachika kwake isiwe sababu ya yeye kusemwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Sina muda wa kuzungumzia mambo hayo kwani nilipofunga ndoa sikusema, sitaki nasema sitaki, maana watu wanaona ni jambo la kuzungumzwa mbona wapo wanaoolewa kifahari na wanaachika,” alisema kwa ukali kisha akakata simu.

BAADA YA NDOA MKE WA DR SLAA AFUNGUKA....'HAIKUWA RAHISI KUFUNGA NDOA NA DK SLAA TUMEPITIA MENGI'

Baada ya kuenea taarifa za Dk Willibrod Slaa kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Josephine Mushumbusi, mwanamke huyo ameibuka na kuthibitisha huku akisema haikuwa kazi rahisi kufanikisha jambo hilo.

Dk Slaa na Mushumbusi walifunga pingu za maisha Februari 26 katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Merciful Redeemer, Canada na mwanamke huyo amelieleza gazeti hili kuwa, mchakato wa kufungwa kwa ndoa hiyo uliwachukua muda mrefu na kupitia vikwazo vingi.

Wanandoa hao waliondoka nchini kwenda Marekani Septemba mwaka jana, siku chache baada ya katibu mkuu huyo wa zamani wa Chadema kujiuzulu uongozi na kujivua uanachama wa chama hicho na kuachana na siasa za vyama. Baadaye walihamia Canada wanakoishi hadi sasa.

Akizungumzia ndoa yao, Mushumbusi alisema ilikuwa ngumu kufungwa, lakini walipambana na kutimiza taratibu zote na kuifanikisha.

“Tunampa Mungu sifa na utukufu, haikuwa rahisi. Tumefuata taratibu zote na kufunga ndoa takatifu kanisani kama tulivyotamani,” alisema.

Ndoa hiyo ilifanikiwa baada ya kukwama hapa nchini Julai 21, 2012 kutokana na pingamizi la mke wa zamani wa Dk Slaa, Rose Kamili na mgogoro ulitokana na aliyekuwa mume wa Mushumbuzi, Aminiel Mahimbo.

Mushumbusi alisema iliwachukua muda mrefu kukubaliwa kufunga ndoa kutokana na taratibu za Canada ambazo ziliwataka wapate mafunzo kwanza, wathibitishwe kuwa hawakufunga ndoa kabla na kuwasilisha tangazo maalumu la kustaafu upadri wa Dk Slaa.

Alisema Canada siyo rahisi kufunga ndoa bila kibali cha Serikali na kukipata ni mchakato mrefu.

“Tumevumilia na kukamilisha yote hayo, siyo kama nyumbani ambako ni rahisi kufanyika, watu wanawaza sherehe huko Tanzania lakini huku unaumiza kichwa kupata vibali vya kanisa na Serikali,” alisema.

Ndoa ya Mushumbusi na Dk Slaa ilisimamiwa na wanandoa raia wa Canada aliowataja kwa jina mojamoja la Rosemary na Emmanuel na mashuhuda kadhaa kutoka Tanzania ambao hakutaka kuwataja.

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa wawili hao hawakufunga ndoa katika Kanisa Katoliki kutokana na kushindwa kutimiza kanuni na taratibu, lakini Mushumbusi alisema ndoa hiyo imefungwa kanisani na kupata baraka zote. Akizungumzia maisha ya huko Mushumbusi alisema kwa sasa Dk Slaa anasoma na baada ya kumaliza masomo hayo watarejea nyumbani.

Azungumzia uchaguzi
Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, Mushumbusi alisema alifurahia Rais John Magufuli kushinda kwa kuwa anayajua madhara ya Ukawa kushinda chini ya Edward Lowassa.

“Si unaona Ukawa wanalalamika majipu kutumbuliwa, niliyajua madhara kama hayo ndiyo maana nimeshukuru Magufuli kushinda,” alisema.   

MREMBO TUNDA AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA TETESI KUWA WAMEACHANA NA YOUND D

Mrembo ambaye amewahi kung’arisha vichupa kadhaa vya mastaa Bongo maarufu kama Tunda amekuwa akitajwa kutoka kimapenzi na rapa kijana maarufu kama Young D au Paka Rapper.

Hivi karibuni kuna uvumi ulizuka kuwa wawili hao wameacha baada ya mrembo huyo kufuta baadhi ya picha alizowahi kupiga na Young Dee huku kati ya zaidi ya picha 480 zilizopo kwenye ukurasa wake wa Instagram amebakiza picha moja tu ya rapa huyo.

Vilevile katika ukurasa wa Young Dee kati ya picha 125 alizowahi kupiga na mrembo huyo wa vichupa ameiacha picha moja tu, jambo ambalo limeibua maswali mengi kwa wapenzi wa burudani wanao wafuatilia mastaa hao.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio mrembo huyo wa vichupa amefungukia suala hilo na kueleza  kuwa yeye na Young Dee wapo sawa ingawa kuna baadhi ya maneno yake yaliashiria kuwepo jambo analolificha.

Alipoulizwa kama yeye na Young Dee ni wapenzi alijibu.”ndiyo Mimi na Young Dee tulikuwa wapenzi”, huku kitendo hicho cha mastaa hao kufuta picha limekuwa ni jambo ambalo linawatokea mastaa wengi pindi kunapotokea tofauti kati yao.

BABA LEVO: WANAOSEMA SHILOLE KACHUJA NI KINA NANI?

Baba Levo ambaye hivi sasa ni mheshimiwa Diwani Kata ya Mwanga Kigoma kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kusema kuwa wanaosema Shilole amechuja ni kina nani hao? Baba Levo alijiuliza hilo na kuzua utata kwani baadhi ya watu walianza kuhisi kwamba watu hao ni wapenzi kutokana na ukaribu wao pindi Baba Levo anapokuwa Dar es Salaam.

Kufuatia kuzua utata kipindi cha eNEWS cha EATV kilimtafuta Baba Levo ili kutatua utata juu ya suala hilo na kutaka kufahamu kama kweli Baba Levo anatoka na Shilole, lakini Baba Levo alikana kutoka kimapenzi na Shilole na kudai kwamba Shilole anatakiwa kutoka na wahanagwa wenzake lakini sio yeye, na kudai wao ni marafiki tu wa karibu.

“Shilole hawezi kuwa na mtu kama mimi, unajua mimi ni kiongozi saizi hivyo huyo Shishi anatakiwa kutoka na wahanagwa wenzake sio mimi nikija Dar es Salaam nakaa kwangu, na kuhusu mimi kuchukua gari la Shilole na kuweka bond hizo ni stori tu kwani natambua kuna watu ambao wanataka kunichafua, lakini hawajui mimi ni mchafu kwani nilishachafuliwa sana kwenye siasa lakini wale walionichafua walishindwa wao na mimi nikashinda na kuwa Mh. Diwani.” Alisema Baba Levo

LULU MICHAEL NA SINGLE MTAMBALIKE WA BONGO MOVIE WATISHA NIGERIA!

Usiku wa March 5 2016 nyota ya Tanzania iliweza kushine vilivyo kunako tasnia ya uigizaji baada ya waigizaji wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Single Mtambalike ‘Rich Richie’ kunyakua Tuzo za (MVCA) zilizofanyika jijini Lagos nchini Nigeria. Tuzo hizo pia ziliweza kuhudhuriwa na mastaa wengi tu wa kibongo.
Usiku wa March 5 2016 nyota ya Tanzania iliweza kushine vilivyo kunako tasnia ya uigizaji baada ya waigizaji wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Single Mtambalike ‘Rich Richie’ kunyakua Tuzo za (MVCA) zilizofanyika jijini Lagos nchini Nigeria. Tuzo hizo pia ziliweza kuhudhuriwa na mastaa wengi tu wa kibongo.

Saturday, March 5, 2016

CHANZO RASMI CHA KIFO CHA MTOTO WA WHITNEY HOUSTON BOBBI KRISTINA CHAFAHAMIKA…!


Chanzo rasmi cha kifo cha Bobbi Kristina Brown kinakaribiana na kile cha mama yake, Whitney Houston – kuzama kwenye maji baada ya kutumia madawa ya kulevya Bobbi Kristina alikufa kutokana na kuzama kichwa chake kwenye maji baada ya kuwa ametumia mchanganyiko wa madawa.

Umebaini vitu alivyokuwa ametumia ni bangi, pombe, madawa yenye uhusiano na cocaine, benzoylecgonine, benzodiazepines na morphine. Ripoti imedai kuwa alifariki kutokana na kupata The pneumonia na encephalopathy – kwamba mapafu yake yalijaa maji na ubongo wake ulijeruhiwa.

Kifo cha Whitney kilitokana na kuzama kwenye bafu katika hoteli ya Beverly Hilton, kulikochangiwa na cocaine na ugonjwa moyo. Bobbi Kristina alifariki July 26 baada ya kukaa miezi kadhaa mahututi. Alikuwa na miaka 22.

LADY JAYDEE KUFUNGA NDOA TENA BAADA YA KUPEWA TALAKA NA GADNER


Siku chache baada ya kupewa talaka na aliyekuwa mumewe, mtangazaji Gardner G. Habash ‘Captain’, mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva anayekuja na ujio mpya alioubatiza jina la Naamka Tena, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide amedaiwa kupata mwanaume mwingine ambaye yupo kwenye mikakati kabambe ya kumuoa, Risasi Jumamosi lina ubuyu kamili.

Jide ambaye amekuwa kimya kimuziki kwa zaidi ya miaka miwili, Februari mwaka huu alipewa talaka katika Mahakama ya Manzese-Sinza jijini Dar baada ya mvutano uliodumu kwa muda mrefu tangu wawili hao washindwe kuishi pamoja.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Jide alimpata mwenza muda mrefu tangu walipomwagana na Gardner lakini mipango ya ndoa ikashindwa kwenda haraka kwa sababu hakuwa amepewa talaka hiyo aliyoidai mahakamani.

“Mbona Jide kitambo tu alishapata mtu sema alikuwa hawezi kufanya mambo ya ndoa kwani hakuwa amepewa talaka na Gardner ila sasa hivi yupo huru na mwaka huuhuu huenda kikaeleweka,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Sema Jide kama unavyomjua, mtu wa usiri sana. Anatumia nguvu nyingi kweli kumficha mchumba wake wa sasa. Hataki watu wamjue.”

Mwanahabari wetu alijaribu kumvutia waya Jide kupitia simu yake ya mkononi ambapo alipopatikana aliomba  asizungumzie mambo ya uhusiano na badala yake akadai aulizwe kuhusu ujio wake mpya.

“Niulize kuhusu program yangu ya Naamka Tena, nipo bize kuandaa ngoma hiyo na kama unavyoona siku chache zijazo natarajia kuiachia, inanifanya niwe bize sana please niache kwanza,” alisema Jide.

Hata hivyo, mmoja wa mameneja wa msanii huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa kile alichoeleza kuwa hapaswi kumsemea Jide katika masuala ya uhusiano, alikiri Jide kuwa na mchumba ambaye wapo katika hatua nzuri ya kuyaanza maisha ya ndoa.
Chanzo:Risasi

JIBU LA VANESSA MDEE KWA SHABIKI ALIYEMDISS JUMA JUX.....ILIKUAJE?


Kupitia akaunti yake ya instagram Vanessa amepost picha ya promo ya Jux na cyril ya kwa ajili ya show ya Morogoro na Dodoma na kuandika maneno haya..

 “Moro na Dodoma sio kwa kunichukulia mtu wangu weekend nzimaaaa dahhhhh!!! Freshi lakini nendeni mkashow love basi. @cyrill_kamikaze @juma_jux @bdozen”

Katika hali isiyo ya kawaida shabiki mmoja alijitokeza na kuandika comment inayoonekana kumdiss mpenzi wa msanii huyo,Jux iliyosomeka ifuatavyo..

”Afu Vanessa mwambie msela wako aache tabia ya kuingia chumvini!!!”

Vanessa alionekana kutopendezwa na comment hiyo na kumjibu kama ifuatavyo..

“@d.magezi kwaresma yote hii usije ukanishindisha nja mwananangu naona kuna mengi yanakustress kama vipi Pita LEFT arif isiwe tabu.” kama inavyoonekana kwenye picha chini..

 
 

KILA MTU ANA WAJIBU WA KUBRAND MALI ASILI ZETU ZISIPOTEE

HARAKATI katika mitandao ya kijamii zimekuwa zikionekana sana tangu wiki iliyopita baada ya msanii Witnesz a.k.a Kibonge Mwepesi kuanzisha kampeni ya utunzaji wa Mali asili zetu nchini zisipotee.

Akiongea na XXL ya Clouds Fm, Witness amesema, ''Kubrand maliasili zetu ni jukumu la kila mtanzania na siyo kwa serikali peke yake, nchi nyingine wananchi wake wanajitahidi kutangaza mali asili zao mpaka wanapitiliza mipaka kwa kuiongopea dunia kwa kusema baadhi ya vitu vyetu vipo nchini kwao.''

Sakata hili la kutangaza mali asili za Tanzania limekuja juu baada ya kuonekana kipande cha video ikimuonesha mwanadada aliyejulikana kama Rosemary Odinga ambaye ni mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya akisema kuwa Olduvai George ipo nchini Kenya.

Lakini pia mtandao mmoja wa habari ambao ulisha wahi kuandika kuhusu nyimbo ya ushirikiano ya msanii Diamond na AKA na kusema kuwa Diamond Platnumz ni msanii toka Kenya.

HARMONIZE: NILIMUULIZA DIAMOND NI MWANAMKE GANI AMEACHANA NAE LAKINI ANASHINDWA KUMSAHAU

Msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya WCB, Harmonize amesema wazo la wimbo wake mpya ‘Bado’ aliyomshirikisha Diamond, lilikuja baada ya kumuuliza Diamond ni mwanamke gani

ambaye ameachana nae lakini bado anashindwa kumsahau.

Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Harmonize amesema baada ya kupata wazo kutoka kwa Diamond ndipo akaanza kuandika wimbo.

“Idea ilikuja kuna siku tulikuwa kwenye gari nikamuuliza (Diamond) kuna mwanamke gari ulimpenda sana hadi leo unashindwa kumsahau, akaniambia hakuna masihara kwenye mahusiano, mimi ndio nikapata idea,” alisema Harmonize.

Aliongeza, “Nikaona kama ni Diamond sio Diamond peke yake ambaye amekutwa na mambo hayo kwenye mahusiano, hata mimi mwenyewe yameshanikuta. Kwa hiyo nikaanza kuandika,

nilivyoandika mistari yangu, nikampa producer akanipa beat nikachagua. Baada ya hapo kwa sababu Diamond alikuwa Nigeria alivyorudi siku nipo nae kwenye gari nikaiplay akaikubali akasema na mimi nitaingiza verse ya pili,”

MR NICE AFUNGUKA KUHUSU PICHA YAKE AKIWA AMEKONDA ILIYOSHTUA WATU...ADAI ALILISHWA SUMU

SIKU chache baada ya kusambaa kwa picha yake inayomuonesha akiwa amepungua mwili na kuzua mjadala mitandaoni huku wengi wakimuonea huruma, mkongwe wa Muziki wa Takeu, Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ ameibuka na kufungukia afya yake.

Picha inayomuonesha Nice akiwa amepungua mwili ilizagaa mapema wiki hii kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi waliochangia mjadala wa picha hiyo, walisema staa huyo aliyetikisa kwa utajiri enzi hizo, kwa sasa atakuwa anaumwa sana huku mjadala mkubwa ukawa ni ya lini?

Baada ya Ijumaa kuinasa picha hiyo, lilifanya jitihada za kumpata msanii huyo kwa kumvutia waya alipopatikana, alifunguka kwa kirefu kuhusu afya yake:

“Kwanza hiyo picha ni ya kitambo sana. Si unakumbua lile sakata langu la mimi kulishwa sumu kwenye chakula? Basi ndiyo kipindi kile.

“Namshukuru Mungu niliiwahi ile sumu na kupewa dawa ambazo natumia mpaka sasa. Kweli nilipungua lakini ni wakati huo, kwa sasa sipo hivyo kama kwenye hiyo picha inayosambazwa mitandaoni,” alisema Mr. Nice.

Akaongeza kuwa ni kweli afya yake haiko poa sana kwa kuwa bado anaendelea kutumia dawa za kuimaliza sumu ile lakini siyo kama vile anavyoonekana kwenye picha hiyo.

FAHAMU AINA 7 YA VYAKULA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME


Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.
Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.

 Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.
1. Blueberry

Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.
2. Mtini (Figs)

Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.
3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)

Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.
4. Karanga

Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.
5. Vitunguu saumu

Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.
6. Ndizi

Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).
7. Chocolate

Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.

SABABU HII HUMPA KIGUGUMIZI ROMA KUMPOST MKE WAKE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII..!

Msanii wa Hip Hop Tanzania,Roma amefunguka kuwa huwa hapendi kumpost mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii kwa kuhofia kuwa inaweza kumharibia biashara yake muziki.

Roma anaamini kuwa kuna mashabiki wengi na kila mtu anapenda kitu fulani kutoka kwa msanii sio nyimbo tu,wengine hata kukupenda kimapenzi kwa hiyo kumpost mpenzi wako kila mara inaweza kuwafukuza mashabiki wa namna hiyo.

“Sometimes kumpost sana unaharibu biashara yako hasa hii ya sanaa yetu,mashabiki wanakuja kwenye show yako sio tu kwa sababu ya ngoma zako,kila mtu anachokipenda kwako...” alisema Roma ambaye amewahi kumpost mpenzi wake mara moja toka ajiunge instagram.

KOCHA MKUU WA MBEYA CITY KINNAH PHIRI ATAJA WACHEZAJI 18 WATAKAO CHUANA NA SIMBA FC

Kocha Mkuu wa Mbeya City Fc, Kinnah Phiri ametangaza majina ya nyota 18 watakaoivaa Simba Sports Club kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliopangwa kuchezwa jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Phiri ameuambia mtandao huu kuwa anatua jijini Dar na kikosi cha nyota hao ambao aliwaandaa maalumu kwa mchezo huo wa mwishoni mwa juma akiwa na imani kubwa kuwa wataiwezesha City kuibuka na ushindi kutokana na ‘kuiva’ vizuri kimazoezi na mafunzo waliyoyapata katika wiki nzima ya maandalizi kupitia mifumo mbalimbali aliyokuwa akiifundisha .

“Nina imani nao,wamefanya vizuri sana kwenye mazoezi ya wiki hii, sina shaka na wao kutupatia matokeo kwa sababu wako sawa tayari kwa mchezo,tutacheza kwenye mfumo mpya ambao haujawahi kuonekana tukicheza, hii ni kwa sababu tumedhamiria kupata ushindi kama ambavyo timu imekuwa ikifanya kila inapokutana na Simba”, alisema.

Miongoni mwa nyota walio kwenye orodha ya kuivaa Simba siku hiyo ya jumapili ni pamoja na beki wa kushotoHassan Mwasapili, mlinda lango Haningtony Kalyesubula pia wamo Temi Felix, Haruna Shamte,Yohana Moriss,Kenny Ally,Geoffrey Mlawa,Issa Nelson na wakali wengine 10 ambao wamepewa majukumu kadhaa kuhakikisha City inaandikisha pointi tatu muhimu mbele ya timu hiyo ya Msimbazi.

Huu utakuwa ni mchezo wa sita kwa timu hizi kukutana katika michuano hii ya ligi kuu ya vodacom huku City ikifanikiwa kushinda mara mara mbili sare mbili na Simba ikishinda mara moja katika michezo mitano iliyozikatanisha timu hizi hapo awali.

HANGING WITH THE BRO! DIAMOND PLATNUMZ & KANYE WEST TAKE A SELFIE IN L.A

Hanging With The Bro! Diamond Platnumz & Kanye West Take A Selfie In L.A. Tanzanian music sensation Chibu Dangote also known has Diamond Platnumz just landed in Los Angeles and guess who he bumped into…Kanye West! Though Platnumz is actually headed to Las Vegas, he had to take a connecting flight at L.A which is where he met Kanye and they posed for a snap. He captioned the photo: “LA am in Town Baby!!!….. With my bro #WEST”

Diamond Platnumz amekutana na rapper ambaye watu wengi wangependa kukutana naye na kuongea mawili matatu kutokana na heshima yake, Kanye West.

Najua kuwa Diamond na Kanye wana kitu kimoja wanachofanana – wote wanapenda fashion kwahiyo kwa hitmaker huyo wa ‘Make Me Sing’ kukutana na Yeezy hata kwa dakika chache tu ni kitu alichokipokea kwa heshima kubwa.

Bila shaka Diamond alikutana na rapper huyo aliyeachia album mpya The Life of Pablo hivi karibuni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles, LAX.

“LA am in Town Baby!!!….. With my bro #WEST,” aliandika Diamond kwenye picha aliyopost Instagram.

Hata hivyo mwisho wa safari yake ni Las Vegas.

“Duh tangu jana saa 10 jioni nipo kwa mandege tu [disappointed_relieved] ….What a Long a** flight!…. Still gat 28 mints to land in LA, then wait for 4 hrs transit….then connect from LA to Las Vegas,” aliandika kwenye picha hiyo chini.

Friday, March 4, 2016

ISIKILIZE NA UIPAKUE HIT SONG MPYA YA OCHU SHEGGY - SHEMEJI YAKO *AUDIO*



Ochu Sheggy ni msanii anayefanya vizuri katika Tasnia ya burudani kwa Hit songs kibao kama vile Ntendezeze, Kingereza, Umechakachuwa, Dumange na sasa Shemeji yako ambayo imekuwa ni msumali unaofanya vizuri masikioni mwa wengi.
Hebu enjoy kwa kuipakua audio hapo chini..!

BEYONCE KAVUA PETE YA NDOA ALIYOVALISHWA NA JAY Z...IS IT OVER?

Beyonce na Jay-Z wanazidi kuandamwa na taarifa za kuachana na kupeana talaka. Taaarifa hizi zimepewa nguvu na kitendo cha Beyonce kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya rafiki yake Kelly Rowland aliyefikisha miaka 35.
Mtu aliyekuwepo kwenye pati hio anasema “Beyonce alivua pete yake na kuiweka juu na kusema hii ni mara ya mwisho ataonekana amevaa pete hio,marafiki walibidi wamtulize”

Jay Z ’46’ na Beyonce wamekuwa wakizungukwa na taarifa hizi kwa muda mrefu sasa

DAYNA NYANGE ANAJICHUBUA???


Picha hapo Juu ni Kabla na Baada ya Dayna Msanii wa Bongo Flava Kujichubua na Kuwa Mweupe Kama Mzungu, hii inamfanya aingie katika list kubwa ya Mastaa wa Bongo waliojikoboa Ngozi na Kubadilika kabisa muonekano,

Swali Langu : Sikuhizi ukiwa Staa ni Lazima Ujichubue ? Kuna Siri Ngani Huko ? na Je Hawaelewi Madhara ya Kujichubua?

MWANAMKE ALIYEFANYA MAPENZI NA SAMAKI AINA YA DOLPHIN AONGEA KWA MARA YA KWANZA…!!

 
Unaweza kushangaa na kuona ni kitu cha ajabu lakini hii imetokea ambapo mwanamke ambaye alifanya mapenzi na samaki aina ya Dolphin ikiwa ni sehemu ya utafiti wa kisayansi amezungumza kwa mara ya kwanza juu ya hatua hiyo.

Mwanamke huyo Margaret Howe Lovatt ambaye ni mtafiti wa wanyama amesema alikuwa sehemu ya utafiti huo uliofanyika katika kisiwa cha Virgin nchini Marekani kwa ajili ya kuwafundisha viumbe wa baharini wenye akili jinsi ya kuongea kiingereza.
Margaret Lovatt Howe
Margaret Howe Lovatt anasema alikuwa akijaribu kumfundisha Peter (the dolphin) jinsi ya kuongea kiingereza lakini uhusiano wao ulikwenda mbali zaidi.

Ilikuwa mnano wa mwaka 1963 ambapo walimsaidia kutengeneza bwawa la Dolphin nyumbani kwake ambako wanasayansi wangeweza kuwasoma wanyama hao wakiwa nyumbani, ndipo hapo Margaret alipokuna na Peter ambaye ni samaki aina ya Dolphin kwa wakati huo akiwa bado mdogo ambapo wawili hao wakapatana na mahusiano yao kukua zaidi kimwili.

Margaret amenukuliwa akisema kuwa “Peter (Dolphin) alipenda kuwa na mimi, mara nyingi alikuwa akijisogeza mwenyewe karibu yangu kwenye mguu wangu au mkono na kuruhusu kitendo hicho.”
Dolphin
Anaendelea kusema kuwa “Haikuwa shida kwangu kwani Peter alikuwa akihisi uwepo wangu na kuona ni kitendo cha kimapenzi kwa upande wake lakini kwangu niliona ni kitu cha kawaida kama sehemu ya masomo yangu.”

ZILIZOSOMWA ZAIDI