NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Tuesday, March 31, 2015

MFAHAMU YULE MRIMBWENDE WA KIJAPAN ALIYEDAIWA KUWA SI MJAPANI *PICHAZ*

Mrimbwende wa japan ameleta kizaazaa baada ya watu kuanza kuhoji Ujapan wake eti kwa kuwa kazaliwa na mama Mjapan na baba mwafrika.
Baba mwenyewe ni mwafrika kutoka Marekani.
Mrimbwende huyu ambaye pia amesomea nchini Marekani anazungumza Kijapan kama lugha yake ya kwanza na mama yake ni Mjapan  kikwelikweli.
Pamoja na ukweli kwamba alizaliwa na kulelewa Japan mrimbwende huyu Ariana Miyamoto  anaonekana katika macho ya wajapan kwamba si Mjapan wa kihivyo, lakini kisheria na hata kwa tafsiri ya nani ni mjapan hakuna shaka anaswihi.
Nchini japan watu wlaiochanganya damu wanaitwa "hafu", na ushindi wa Miyamoto kuwakilisha japan katika Miss Universe kumeleta mtafaruku mkubwa hasa katika vyombo vya habari kwamba inakuwaje hafu awasilishe japn kama Mjapan kamili.
Mdada huyo ambaye amejaliwa miguu ameleta taabu kiasi cha watu kuuliza katika vyombo vya habari kama ni sawa kwa hafu kuiwakilisha Japan.
Mrembo huyu anakuwa hafu wa kwanza kuwakilisha taifa hilo katika michuano ya urembo duniani Miss Universe.
Pamoja na mafanikio makubwa, ushindi wake haukuja kirahisi katika nchi ambayo haina mchanganyiko wa kutosha wa damu.
Akiwa na urefu wa futi sita akiwa katika viatu vya mchuchumio, binti huyu wa miaka 20 analazimika kujihami baada ya kudaiwa kwamba yeye si Mjapan hasa kwa kuwa baba yake ni mtu mweusi kutoka Arkansas, Marekani.



Miyamoto, amekulia Nagasaki, Japan, na pia alifika Marekani kwa ajili ya kujipatia elimu.
Kutokna na mchanganyiko na hasa kusomea Marekani baadhi ya wajapn wanaona kwamba yeye si Mjapan halisi na hafai kuwaikilisha nchi hiyo katika michuano ya urembo kama Mjapan.
Binti huyo alitumia  muda wake wa kwanza kutokea katika televisheni kuwaeleza waandishi wa habari kwamba japo anaoinekana kwa nje yeye sio mjapan lakini ndani yake yeye ana vitu vingi vinavyomuashiria kuwa yeye ni mjapan.
Katika mahojianoi na CNN alisema kwamba  amekuwa akipata taabu sana nchini japan kwani hata katika makuzi yake watu walikuwa wakimtenga, wakimvurumusha na hata kumtupoia uchafu kwa madai kwamba yeye si mjapan.

 
Kwa mujibu wa tafsri iliyofanywa na Washington Post, katika moja ya twita ilisema kuwa japo anawakilisha Japan katika shindano hilo sura yake inaonesha kwamba yeye si Mjapan hata kama unataka kujikomba.
Mwingine alisema, "Miss Universe Japan  ni... Nini?Huyu ni mtu wa aina gani?Sio Mjapan, sawa?"
Ingawa webu ya Kotaku ilipongeza ushindi wa Miyamoto na kusema ni dalili kwamba japan inabadilika japo kw ataratibu sana imesema kwamba wengi wa waliotoa maoni yaow alitaka mwakilishi ambaye ni Mjapan kwa kila kitu.
Hata hivyo si kila mtu anafikiria kinyume, wapo wengi waliounga mkono kufanikiwa kwake na mitandao ya jamii ilisema kinachojalishwa ni mapenzi kwa nchi wala si wajihi.
Na wengine wamesema kilio kwamba si Mjapan hasa ni shauri la kijinga na fikira za kizamani sana.

BASATA YAMKABIDHI BENDERA MSHINDI WA AIRTEL TRACE MUSIC

 
Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Nsao Shalua (kushoto), akikabidhi bendera ya taifa kwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha nchi katika fainali za Afrika za Airtel Trace Music Stars zitakazofanyika Jumamosi Machi 28, nchini Kenya .Anayeshuhudia (katikati), ni Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga.
Barasa la Sanaa Tanzania jana limemkabithi bendera mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Bwana Nalimi Mayunga anayeondoka leo nchi
kwenda kuhudhuria mashindano ya Airtel Trace Afrika yatakayoshirikisha washiriki toka nchi 13 barani Afrika yanayofanyika nchini Kenya siku
ya Jumamosi tarehe 28 March 2015.

Mayunga aliibuka mshindi katika kinyanganyiro cha kusaka Wakali wa vipaji vya mziki kupitia shindano la Airtel Trace Music lililozinduliwa na kampuni ya Airtel Tanzania Mwaka Jana mwezi wa kumi
na kushirikiksha washiriki mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali nchini ambapo fainali ya kumsaka mshindi ilifanyika mwanzoni mwa mwezi wa februari na kumwezesha Mayunga kuwashinda washindani wengine watano na katika fainali hizo na kuondoka na kitita zawadi ya shilingi million 50.

Akiongea wakati wa kukabithi bendera hiyo, Mkurugenzi wa ukuzaji sanaa na Masoko wa BASATA bi Nsao Shalua alisema”  kwanza tunachukua fulsa kuwapongeza Airtel kwa kuanzisha shindano hili na kwa kufata taratibu
zote za kuratibu mashindano.
 Airtel leo wameonyesha mfano kwa kumleta mshindi hapa ofisini, kuaga rasmi na kupatiwa kibali cha kusafiri
kutoka baraza la sanaa Tanzania kitu ambacho hakifanywi na makampuni mengi na hata wasaani wengi nchini. Huu ni mfano wa kuigwa na natoa
wito kwa watu wote wanaoondoka nchini kwaajili ya kwenda kufanya shughuli za sanaa kuhakikisha wanafata utaratibu kwa kutufahamisha na kupata hati maalumu ya kushiriki shughuli na kuiwakilisha nchi yetu nje ya nchi.

Aidha napenda kumpongeza Mayunga kwa kuibuka kuwa mshindi na kupata nafasi ya kuwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Afrika, tunapenda kumwomba atumie fulsa hii vizuri na kwa kufanya hivyo basi tunaamini
atafanya vyema. Tunamtakia safari njema na mashindano mema, tunaamini Mayunga atatuwakilisha vyema na kutangaza nchini yetu katika angaza za muziki kwa ujumla

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga alisema” Leo tunamuwezesha Mayunga kwenda kushiriki na kuiwakiisha nchi yetu katika mashindano ya Afrika Tunamwezesha kujiwekea umaarufu na kuonyesha kipaji chake kwa wadau wa ndani na nje ya nchi, pamoja na Mayunga
tunawawezesha vijana wengi barani Afrika kwa ujumla kuzifikia ndoto zao. Mashindano haya yatafanyika siku ya Jumamosi , jijini Naivasha Kenya ambapo washiriki kutoka nchi 13 barani Afrika watachuana vikali.
Mshindi wa Airtel Trace Afrika atapata nafasi ya kwenda nchini marekani na kupata mafunzo kutoka kwa mwanamuziki wa miondoko ya R&B , Akon na kuweza kurekodi nyimbo zake.

Natoa wito kwa watanzania kumpigia kura Mayunga kwa ku  tuma SMS, yaani ujumbe mfupi andika neno YUN kwenda 15594,  Alhamisi ni siku ya
mwisho ya kupiga kura, asiliimia 25 ya ushindi inatoka kwenye kura yako hivyo kura yako ni ya muhimu sana. Aliongeza Aneth.

Akiongea mara baada ya kukabithiwa bendera Malimi Mayunga alisema”
namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufikia hatua hii, nawaahidi watanzania kuwawakilisha vyema, pamoja na hayo nawaomba sana
watanzania waniunge mkono kwa kunipigia kura ili nipate nafasi ya kuweza kuibuka kuwa mshindi. Hii kwangu ni nafasi ya pekee sana na namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha na

Airtel kwa kuwawezesha vijana kama mimi kuonyesha vipaji vyao na kuzifikia ndoto zao kupitia mashindano mengi kama haya Mashindano ya Airtel Trace Music Star yalianzishwa kwa lengo la kuonyesha vipaji vya vijana kimuziki na nakuwapatia fulsa ya kukua
kimuziki


MWANAMUZIKI SUMA LEE AKATA SHAURI AAMUA KUACHA MZIKI, AAGIZA NYIMBO ZAKE ZIFUTWE NA REDIO WASIZIPIGE TENA

HIT MAKER  wa ‘Hakunaga’, Suma Lee amesema kuwa hatafanya tena muziki kwasababu ameachana kabisa na maisha hayo na ameamua kusomea dini ya kiislam Suma ambaye alitengeneza pesa nyingi kupitia hit yake ya ‘Hakunaga’, amesema kuwa hana mpango wa kuzitoa nyimbo zake zilizoko studio ambazo hazijatoka.
“sifanyi tena muziki na nimeachana kabisa na maisha hayo, na nyimbo zote zilizobaki studio nimezisimamisha zisitoke baada ya kuzilipia, “ Alisema Suma.
“kuna wimbo mmoja nimefanya na Cp ambao ndio ulikuwa wa kurudisha kundi la Parklane, pia nimeuzuia, labda Cp auchukue yeye.
Kilichobaki ni kuwaombea wazazi wetu waliotutangulia, wengine walikuwa hawataki tufanye kazi hizi, kwa kuwa hawapo na hakuna wakutukataza tena, bora tukae na kuwaombea.”

UNYWAJI WA MAZIWA HUZUIA MARADHI YA AKILI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOWTuzjrEuPPV5PSF1u9aT0Xee2l4pMbkWeYNLKl4UGIJrj01FgANYkSZpnNtsKReGJhyphenhyphencp3Cp66VbU6Eml7pi_0_UMd50oIkY5MFn-AT76KpcDJAwEWNKNp2qQ7qATb64Kza4E7l0SBtb/s400/Chef+Issa+yogurt+(2).jpg 
Maziwa huimarisha seli za ubongo

Wanasayansi wagundua chembechembe za glutathiona katika maziwa ambazo hulinda ubongo kuharibika


Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wanasayansi kutoka nchini Marekani ni kwamba unywaji wa glasi 3 za mawiza kwa siku hulinda na kudumisha seli za ubongo wa binadamu.


Wanasayansi wamefahamisha kuwa, chembechembe za glutathiona zinazopatikana katika maziwa hulinda seli za ubongo na kusababisha maziwa kupunguza madhara yanayoweza kuukumba ubongo na kusabaisha akili kudhurika.


Chembechembe hizo hupunguza kasi ya ugojwa wa Alzheimer na Parkinson kumsibu binadamu.


Dr. Debra Sullivan, mmoja wa waanzilishi wa mradi kuhusu utafiti huo alisema kuwa, kwa muda mrefu tunafaham kuwa maziwa ni muhimu kwa mifupa na misuli ya binadamu ila kwa sasa tumegundua pia kuwa maziwa ni muhimu kwa ubongo.


Ili kufaanikisha utafiti huo, wanasayansi hao walifuatilia lishe ya bongo za watu wazima wenye afya njema na kugundua kuwa watu wanaokunywa kwa uchache glasi 3 za maziwa kwa siku walikutwa na idadi ya kuridhisha ya chembechembe za glutathiona.


Utafiti huo ulichapishwa katika gazeti la "American Journal of Clinical Nutrition".

Monday, March 30, 2015

15 MBARONI KWA NJAMA ZA KUTAKA KUMTOROSHA MCHUNGAJI GWAJIMA

KUJARIBU KUMTOROSHA MCHUNGAJI GWAJIMA KUTOKA HOSP. YA TMJ MIKOCHENI.
Mtoa taarifa ASP Pamphil Mholery OCS Kawe akiwa ni ofisa wa zamu mkoa Kinondoni,trehe 29.3.2015 majira ya 0300hrs alipata taarifa kutoka vyanzo vya taarifa kwamba kuna njama za kumtorosha mtuhumiwa.
Akiongozana na makachero majira ya 03:30hrs walifika eneo hilo na kukuta kweli kuna hali sio ya kawaida kwa kuwepo kundi la watu kwa usiku ule.
Wakawakamata watuhumiwa 15 na mmoja wao aitwae Ekomia Diagare alikutwa na begi ambalo lilikutwa na vitu vifuatavyo alivyokuwa akipelekewa Gwajima.

1.Silaha pisto Bereta no CAT 5802 ikiwa na risasi 3.

2.Risasi 17 za shortgun.

3.Vitabu check viwili

4.Passport ya kusafiria yenye jina Gwajima Mathias Joseph no AB544809.

5.Kitabu cha Equity Bank in check.

6.Document mbali mbali za kampuni ya Puma.

7.Charger ya simu na tablets

8.Suruali mbili,makoti mawili,singlend moja,socks pea mbili na boxer moja.
Watuhumiwa wote wako police Oyster kwa mahojiano.

HAWA NDIYO MISS TANZANIA WALIYOJITOKEZA NA KUJITANGAZA HADHARANI KUWA WANASUMBULIWA NA GONJWA HATARI..!!

MISS TANZANIA wawili, Happiness Millen Magese (2001) na Angela Damas (2002), wamejitokeza na kujitangaza wazi kuwa ni miongoni mwa mamilioni ya wanawake duniani wanaosumbuliwa na tatizo liitwalo ‘endometriosis’ ambalo huwafanya wapate maumivu makali wakati wa hedhi na pia kuwafanya wasiwe na uwezo wa kushika mimba. Tatizo hilo husababisha seli hai zinazounda mji wa mimba kukuwa/kuota nje ya mji wa mimba. “To all the ladies who have to live with the sufferings of endometriosis- May sharing our messages make us realize we are not alone, and may the sharing allow us to look for ways to help us live with less pain,” ameandika Angela Damas.
Happiness Millen Magese (2001)
Ujumbe huo umemvutia, Happiness Magese ambaye naye aliamua kujitangaza wazi kuwa na tatizo hilo na kuanzisha kampeni ya ‘endometriosisafrica’.
“Praying for more women to speak out and share their stories .Wow this made my day
….thank you my darling Angela(Miss Tz 2002) for sharing your story .I feel better that we all finally speak out . Insta fam Angela Damas was actually the next queen after me in Wow this made my day ….thank you my darling Angela(Miss Tz 2002) for sharing your story .I feel better that we all finally speak out . Hi sisters Angela Damas was actually the next queen after me in Tanzania . How would Could one tell this amazing ,smart n beautiful person has this battle # endo power #we can do this together emojiemojiemoji @skinkissedbird we can save one’s happiness n pains. Let’s speak out cc @ladivamillen Tanzania.”
Angela Damas (2002)
Millen anasema ameshafanyiwa upasuaji mara 12 hadi sasa Wakati wa kutangaza kuwa na tatizo hilo, March 16 mwaka huu, Millen aliandika kwenye Instagram:
It took me 17 years of struggle ,12 surgeries ,blocked Fallopian tubes ,1digestive system surgery,1ovary failure ,1miscarriage and still in pains I don’t know when it will stop.For the help of @ritadominic awareness and padma Lakshimi my friends @funminewyork @byanakusophy @adhiamboml n my family . I’m able to come out today and say this “I wear Yellow for me and all women from all over the world who struggling with Endometriosis . It’s ok to talk about our menstrual pains . You’re all warriors #speak about it #Dont ask for sympathy ,ask for help before it’s too late #March 2014 millions women walk for endometriosis #Dont loose hope. By rising this awareness we could help the cause to be able to give us free or reasonable price which can help all women to afford the treatment.#teamendometriosisafrica#Tanzania

MSANII KEISHA ASIMULIA ALIVYONUSURIKA KIFO *PICHAZ*

Msanii wa Bongo Fleva, Khadija Shabani’Keisha’
Akizungumza na Clouds Fm alisema kuwa alikuwa akitoka chuoni CBE na kwamba alikuwa akimfuata mumewe alipofika maeneo hayo ndipo lilipotokea gari na kumuovateki na kuligonga gari lake.
Msanii wa Bongo Fleva, Khadija Shabani’Keisha’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali maeneo ya Maktaba, Posta jijini Dar.
Aidha alisema kuwa alisikia maumivu na alipokwenda hospitali kufanyiwa vipimo vilionyesha hakupata majeraha kwa ndani. ‘’Nashukuru Mungu nilipimwa hospitali vipimo vilionyesha sikupata madhara yoyote kwa ndani kwani nilikuwa na wasiwasi labda niliumia kwa ndani,’alisema Keisha.

PANYA NI BONGE LA KITOWEO….TAZAMA AKIPIKWA HAPA!

KUNA tamaduni nyingine hutumia nyama ya mbwa kama kitoweo na wakati mwingine huamini ina faida kubwa mwilini tofauti na nyama ambazo zimezoeleka kuliwa na binadamu.
Hii imetokea huko India baada ya mwanamke mmoja kumalazimisha mtoto wake kula nyama ya panya kama kitoweo cha asubuhi kwa madai watamsaidia kumpatia nguvu.
Mtoto huyo aitwaye Chen alizua majibizano kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuweka picha ya panya hao ambao alitengewa na mama yake huku mama huyo akumuhimiza kuhakikisha anamaliza kabla ya yeye kuondoka kwenda kazini.
Awali mtoto huyo alidhani hawakuwa panya bali sungura lakini alipokuja kuujua ukweli alikataa kula lakini mama yake aliendelea kumlazimisha.
Alimsisitiza kuwa panya mmoja ana uwezo wa kumpatia  vitamini mwilini sawa na kula kuku watatu.

Saturday, March 28, 2015

Wednesday, March 25, 2015

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATANGAZA UFADHILI WA MASOMO NCHINI CHINA KWA MWAKA 2015

 Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud akizungumza na wanahabari.
  Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu ufadhili wa masomo nchini China kwa mwaka 2015. Kulia ni Ofisa Habari wa Maelezo, Fatma Salum.
 Mwanahabari Salome Kitomari kutoka gazeti la Nipashe, akiuliza maswali katika mkutano huo.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Hapa mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale

WIZARA ya Nishati na Madini imetangaza nafasi za masomo kwa vijana wa Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa China kwa kipindi cha mwaka 2015.

Hayo yalibainishwa na Msemaji wa Wizara hiyo Badra Masoud Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.

Alisema nafasi hizo za masomo ni ngazi ya Shahada ya Juu ya Uzamili katika fani ya gesi katika Chuo Kikuu cha Jiosayansi cha China ambapo muda wa kutuma maombi hayo umeongezewa hadi kufikia Machi 30 mwaka huu.

Alisema waombaji wa ufadhili huo wanatakiwa kuwa na Shahada ya Sayansi ya Ardhi au Uhandisi kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali, na muombaji awe na miaka kati ya 35 na 40.

Katika hatua nyingine Masoud alisema mitambo ya kuchakata gesi imekamilika kwa asilimia 96.

Alisema kukamilika kwa mitambo hiyo inamanufaa makubwa ikiwemo umeme wa uhakika na gharama nafuu kwani utekelezaji wa mradi huo utaliwezesha taifa kuokoa trilioni 1.6 kwa mwaka zinazotumika kununua mafuta kwa ajili yua kuzalisha umeme.

Masoud  alisema kukamilika kwa mradi huu kutachochea  maendeleo ya viwanda nchini kwani viwanda vingi vimeonyesha nia ya kutumia nishati  ya gesi asilimia  katika  kuendesha mitambo  yake  ya uzalishaji.aidha umeme wa uhakika utapunguza gharama za uzalishaji na kufanya  bidhaa za tanzania kukuzika katika masoko mbalimbali duniani.

Alisema tatizo la ajira nalo litapungua kutokana na kukamilika kwa mradi huu ambao utapelekea ajira  mpya  nyingi  kupatikana na kutokana na kuwepo kwa umeme wa kutosha na uhakika katika viwanda ambapo  viwanda  vingi vitaanzishwa vilevile umeme utakwenda mashambani na kwenye biashara nyingine hivyo kwa namna moja ama nyingine ajira  zitaongezeka. 

Alisema gesi hiyo asilia pia hutumika kama malighafi katika viwanda mbalimbali kama,mbolea, kemikali,aluminiamu pamoja na kutengeneza vifaa vya plastiki uanzishaji wa viwanda vipya kutokana na matumizi ya gesi  asilimia kutachochea 

kukua kwa uchumi  wa nchi yetu na kwa upatikanaji wa ajira mpya nyingi kwa vijana wetu. 

Aliongeza kuwa Serikali kupitia wizara hiyo chini ya Mradi Endelevu wa Usimamizi wa Rasilimali Madini (SMMRP), inakaribisha maombi ya Ruzuku Awamu ya pili kwa wachimbaji wadogo nchini.
#habari za jamii

CHEKI ZARI NA DIAMOND PLATINUMZ WAKICHAKALIKA MJEMNGONI MWAO *PICHAZ*

Friday, March 20, 2015

FUMANIZI: NEY WA MITEGO AFUMA MAMA WATOTO WAKE AKICHEPUKA CHUMBANI..AZUA TIMBWILI ...CHEK HAPA!!!

KABAANG! Mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, amedaiwa kumfumania ‘laivu’ mchumba wake Siwema akiwa kitandani na ‘serengeti boy’ wake ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, Ijumaa lina full stori.

NI MWANZA
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mwanzo mwisho, tukio hilo lilichukua nafasi Machi 15, mwaka huu maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza ambako mrembo huyo alikuwa akiishi, baada ya Nay kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa mrembo huyo usiku wa Machi 14 alionekana akiponda raha ndani ya klabu moja iliyopo katika jengo la Hoteli ya Golden Crest.

“Wambeya walimpenyezea habari Nay, kesho yake asubuhi sana akatimba Mwanza kwa ndenge na kumkuta laivu Siwema akiwa na seregeti boy wake kitandani,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

AMPOKONYA SIMU, AWAPIGA PICHA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, Nay baada ya kuwakuta wawili hao wakiwa katika hali ya taharuki katika chumba cha nyumba hiyo ambayo alimpangishia Siwema, alimpokonya simu mpenzi wake huyo na kuwapiga picha za ushahidi wawili hao kisha akamchukua mwanaye kurudi Dar.

SIWEMA ATOKA NA KANGA MOJA
“Siwema baada ya kuona Nay amempokonya simu, alikurupuka akiwa na kanga moja kisha kumfuata ili arejeshewe simu yake, Nay aligoma na kukwea teksi akamuacha Siwema akilalama,” kilidai chanzo hicho.

NAY MSTARABU?
“Kiukweli Nay ni mstarabu sana maana hakuonyesha hasira za aina yoyote pamoja na kwamba aliwafuma laivu, alitoka taratibu, hakufanya ugomvi wowote kama watu wengine wanavyofanya pindi wanapofumania,” kilizidi kudai chanzo chetu.

NAY AKWEA PIPA, ARUDI DAR
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya Nay kufanikiwa kumuacha Siwema na jamaa yake, alikwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupanda ndege kurejea maskani kwake jijini Dar.
“Jamaa (Nay) hakutaka kuuweka usiku, alichokifanya ni kukwea pipa na kichanga chake hadi jijini Dar na kwenda kumkabidhi mama yake,” kilisema chanzo hicho.

Siwema.

NAY ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu baada ya kuzinyaka habari hizo, alimvutia ‘waya’ Nay ambapo alipopatikana na kusomewa mashtaka ya kwenda kumfumania mchumba wake, alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa undani lakini akadai amemchukua mwanaye mikononi mwa Siwema kutokana na mchumba wake huyo kuzidiwa na mambo yake.

“Sitaki kuzungumzia chochote kwa sababu sitaki kuonekana mbaya, ila kiukweli nilienda Mwanza na kumchukua mwanangu na hapa ninapozungumza na wewe, mwanangu yupo chini ya uangalizi wa mama yangu mzazi,” alisema Nay.

SIWEMA KAFUATA SIMU YAKE
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, chanzo kilicho karibu na wawili hao kilipenyeza ubuyu kuwa Siwema ameibuka jijini Dar kwa lengo la kufuata simu yake ikidaiwa kwamba eti ina siri zake nyingi.

SIWEMA HAPATIKANI
Jitihada za kumpata Siwema kupitia simu yake ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake ilikuwa mikononi mwa Nay, jitihada zinaendelea ili na yeye afunguke ukweli wa tukio hilo.

TUJIKUMBUSHE

Nay na Siwema wamedumu kwenye uhusiano kwa takriban miaka mitatu ambapo wamefanikiwa kupata mtoto huyo mmoja. Awali, Nay aliwahi kuingia kwenye mgogoro na kigogo mmoja ambaye alikuwa akimtaka mrembo huyo lakini alifanikiwa kumuweka mikononi mwake kabla ya kumfumania na serengeti boy

KIM KARDASHIAN AONYWA NA WATAALAMU APUNGUZE KUFANYA MAPENZI *PICHAZ*

Kim Kardashian.
MADAKTARI wamemuonya mwanadada Kim Kardashian kuacha tabia yake ya kufanya mapenzi mara nyingi kwa kuwa ni hatari kwa afya yake.
Kanye na mkewe Kim.
Mrembo huyo ambaye ni mke wa mwanamuziki Kanye West alikiri katika sehemu ya 10 ya kipindi chao cha familia kinachoruka runingani kuwa yeye na mumewe wanafanya mapenzi mara 15 kwa siku wakijaribu kupata mtoto mwingine.
Wanandoa hao tayari wana mtoto mwenye miezi 20 aitwaye North West na sasa wanataka kupata mdogo wake.
Kwa mujibu wa kituo cha E!News, Kim ameeleza kuwa madaktari wamemshauri kupunguza tabia yake hiyo ya kufanya mapenzi mara nyingi kwani siyo suluhisho la kushika mimba.
Mrembo huyo anashangaa kwa nini watu wasiohitaji kupata watoto ndiyo hupata mimba haraka.
"Wasichana wa kati ya miaka 13-19 hupata mimba ndani ya sekunde. Inashangaza. Kama huitaji kupata ujauzito, ndipo unashika mimba." alitania Kim

DIAMOND PLATNUMZ: ETI NINI???.. MIMBA YA ZARI IMETOKA!!!?


DIAMOND PLATNUMZ akana uvumi unaozagaa mitandaoni kuwa mimba ya mpenzi wake Zari imeharibika. 
Diamond aliyasema hayo baada ya kuongea na paparazi wa mtandao mmoja wa kijamii.
Diamond akasema:
Hee! Eti mimba ya Zari imetoka! Wanaosema hivyo walaaniwe. Mbona Wabongo wazushi sana, itakuwaje hivyo halafu nisijue. Zari yuko fiti na mimba inaendelea vizuri, ona picha za kitumbo (anamuonesha paparazi picha za Zari kwenye simu yake).
Kuna wapuuzi wachache tu wanakaa na kujitungia mambo yao ili wajenge mada zao, niliona sana watu wakijibizana na kubishana juu ya hilo, lakini nikutoe wasiwasi kuwa hakuna taarifa kama hizo.”

ITAZAME NA UIPAKUE VIDEO YA JENNIFER LOPEZ – FEEL THE LIGHT


MHUDUMU WA BAR AFIKISHWA POLISI BAADA YA KUDAGANYA JINSIA YA MWANAMKE KUMBE NI DUME

UGUMU wa maisha unaongeza ubunifu, ubunifu mwingine unakuweka pabaya.. huu wa huyu jamaa
sidhani kama tunaweza kuuita ni ubunifu ila jamaa aliamua tu atumie njia hii ili apate tu njia ya kupata mkate wa siku.

Mmiliki wa Bar ya Siaya, Kenya alimshtukia jinsia ya mmoja ya wahudumu wake wa Bar kwamba jinsia yake
sio ya kike.. Akatoa taarifa Polisi kuhusu mhudumu huyo, walipokuja kumpekua jamaa alijitetea kwamba ana jinsia mbili.

Jamaa huyo anaitwa Michael Obiero alikamatwa baada ya kufanya kazi kwa siku mbili kwenye Bar hiyo
akijitambulisha kwa jina la Brenda na pia alikuwa akilala chumba kimoja na wahudumu wengine wa kike

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. GODBLESS LEMA (MB)

UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu, familia yangu na viongozi wangu wa chama na wananchi wa Jimbo langu. Nawashukuru pia maadui zangu kwa dhati kwani uadui wao, hila zao, na mbinu zao chafu dhidi yangu zimeendelea kuiimarisha imani yangu na tumaini langu siku hadi siku, katika vita hii muhimu tunayopigana ya kulikomboa taifa hili.

Mheshimiwa Spika,Muswada huu wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi unaletwa katika Bunge lako tukufu wakati ambapo nchi hii iko katika mtanziko mkubwa ambapo matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yamekithiri; mauaji ya raia kwa kutumia silaha za moto yameongezeka; matukio yenye sura ya ugaidi ya utekaji na utesaji yameshuhudiwa hapa nchini, matukio ya uvamizi na uporaji wa silaha katika vituo vya polisi yanashamiri na uhamiaji haramu umekuwa ukiongezeka pia kwa kasi hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Ni ukweli usiopingika kwamba matukio yote haya yametokea huku kukiwa na sheria ya Usimamizi wa Silaha na Risasi ambayo itafutwa na muswada huu kama utapitishwa na Bunge. Hii ni dhahiri kwamba tatizo kubwa la nchi hii sio sheria na matumizi yake, bali ni uongozi uliokosa fikra chanya na utu katika kutawala. 

Ndio maana leo, Serikali inafikiri kupambana na janga la Mauaji ya Albino ni kuwatenga Albino na jamii kutoka kwenye makazi yao ya kawaida wakati tatizo la msingi ni imani potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba; huwezi kuipinga imani kwa kutumia silaha isipokuwa kwa habari njema (imani inayojali utu) kuwafikia watu wote. 

Mheshimiwa Spika,Pamoja na nia njema ya Serikali ya kuleta Muswada huu, Kambi Rasmi ya Upinzani inaamini kwamba, kama Serikali itajali utu, usawa, haki na demokrasia ya kweli pengine hakungekuwa na hofu ya matumizi mabaya ya silaha miongoni mwa wananchi na hivyo kusingekuwa na na haja ya kuleta sheria za kudhibiti silaha na kuweka masharti magumu kwa wananchi kumiliki silaha, hasa kipindi hiki ambacho kumekuwa na matukio mengi ya kigaidi, ya uvamizi, utekaji na utesaji ambapo kimsingi wananchi wanahitaji ulinzi wa Serikali na ulinzi binafsi zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Mheshimiwa Spika,Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ifikapo Oktoba mwaka huu wa 2015. Matumizi bora ya sheria za kulinda amani nchini ni muhimu sana wakati huu. Lakini mambo muhimu na ya msingi yakipuuzwa amani inaweza kutoweka licha ya sheria ngumu za udhibiti ikiwemo ya udhibiti wa silaha kuwepo: Masuala hayo ni kama yafuatayo: 

i. Kuchezea haki ya mwananchi kujiandikisha kuwa mpiga kura:

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza kwamba, mzaha katika jambo hili hautavumilika. Aidha, ijulikane kwamba wananchi watakapotambua kuwa hawawezi kuwapata viongozi wao wanaowataka kupitia sanduku la kura, basi wanaweza kutafuta haki yao kwa njia nyingine hali ambayo inaweza kuliingiza taifa katika machafuko kwani haki haiombwi ila inadaiwa. 

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura ili waweze kuamua nani atakuwa kiongozi wao kwenye uchaguzi Mkuu unaokuja. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inamkumbusha kila mwananchi atambue kwamba “Kura yako ni Maisha yako, Nenda Kajiandikishe Sasa” 

ii. Kufanya Mzaha na uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi:

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaionya Serikali kutofanya Mzaha na jambo hili kwani linaweza kuiingiza nchi katika machafuko makubwa. Mheshimiwa Spika, Viongozi wa nchi hii wamekuwa wakifanya mizaha kuhusu maisha ya wananchi kwa mambo mengi, yakiwemo ufisadi uliokithiri. Kwa mfano wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika, uliwahi kumwomba Mheshimiwa Andrew Chenge kutoa mwongozo wa kutengeneza maazimio ya Bunge kuhusu watuhumiwa wa wizi wa fedha za Escrow wakati yeye mwenyewe alikuwa ni mtuhumiwa. 

Huu ni mzaha mkubwa ambao kwa tafsiri inaonyesha kwamba watawala wanawaona watanzania kuwa ni wajinga. Kambi Rasmi ya Upinzani inaonya kuwa mizaha kama hii ikiletwa kwenye suala la uwepo wa tume huru ya uchaguzi, taifa hili linaweza likasambaratika. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinataka Tume Huru ya Uchaguzi, si kwa sababu inataka kushinda uchaguzi bali ni kwa sababu inataka kujenga na kulinda Imani ya Mpiga Kura ili kulinda amani ya nchi yetu”. 

iii. Matumizi ya Kisiasa ya Jeshi la Polisi:

Mheshimiwa Spika, kwa vile imethibitika pasipo shaka yoyote kwamba Polisi mkatili na mkorofi dhidi ya Upinzani anapandishwa cheo, ni dhahiri kwamba kitendo hiki kimejenga msingi (precedence) wa polisi kuwaonea, kuwadhalilisha na kuwafedhehesha viongozi wa Upinzani kwa matarajio kwamba watapongezwa na kupandishwa vyeo na Serikali.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani imepigia kelele sana suala hili la matumizi mabaya ya Jeshi la Polisi ya kulinda maslahi ya kisiasa ya watawala kwa miaka yote. Viongozi, wanaharakati na wananchi wanaounga mkono mageuzi wamepita kwenye bonde la uvuli wa mauti kwa muda mrefu. 

Mheshimiwa Spika, Hatukuonewa kwa sababu sisi ni wanyonge, ila ni kwa sababu tumeendelea kuwa wavumilivu. Nina mashaka kama uvumilivu huo utandelea kuwepo kama uonevu na ukandamizaji utaendelea. 

Mheshimiwa Spika, Mwenyezi Mungu, pamoja na upole wake, ukarimu wake, upendo wake, rehema zake kwa watu wote lakini bado ametenga Jehanamu kwa watenda dhambi ambao amewaumba yeye mwenyewe. Tusisubiri wananchi wachoke kuvumilia, bali hekima ya Mungu ituongoze ili kuliepusha taifa letu na majanga ya uvunjifu wa amani pindi watu watakapokosa uvumilivu wa mateso. 

iv. Ulinzi wa Raia na Mali zao:Mheshimiwa Spika,

Kukosekana kwa ulinzi na usalama wa raia na mali zao kunaweza kuliingiza taifa katika machafuko. Matukio ya kuuwawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi – Albino, mauaji ya vikongwe na wanawake kutokana na imani za kishirikina yamekithiri sana katika nchi yetu licha ya kuwa na vyombo vya ulinzi na usalama. 

Hali hii imefanya wananchi kukosa imani na Serikali kwa kuwa bado yanaendelea licha ya kampeni nyingi kutoka kwawanaharakati mbalimbali kupinga mauaji ya Albino. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitahadharisaha Serikali kutodharau kundi la Albino kuwa ni dogo na kutolipatia ulinzi wa kutosha.

Mheshimiwa Spika,Baada ya utangulizi huo, sasa naomba nijielekeze kwenye muswada wa Sheria uliopo mbele yetu unaohusu Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi.

Mheshimiwa Spika,Matukio yote niliyoyataja hivi punde, ni matukio ambayo kwa kiasi kikubwa yamedhoofisha hali ya usalama hapa nchini. Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kwamba muswada huu umekuja wakati muafaka kwa kuwa matukio niliyoyataja hapo juu ambayo yamekuwa yakiongezeka hapa nchini, ni matukio ambayo utekelezaji wake unahitaji silaha. Na kwa kuwa matukio hayo ni ya kihalifu, ni dhahiri kwamba hata silaha zinazotumika, hazina uhalali. 

Hivyo sheria bora itakayoweka udhibiti na usimamizi wa matumizi ya silaha hapa nchini inaweza kufanikiwa kupunguza matukio ya kihalifu ikiwa itatungwa kwa nia njema ya kulinda usalama wa raia wote na sio kwa lengo la kukandamiza kundi fulani la watu ili kukidhi matakwa ya kisisasa ya kundi la watu wachache.

MAONI NA MAPENDEKEZO YA JUMLA 

Mheshimiwa Spika,Kabla sijaanza kuchambua vifungu vya muswada huu, naomba nitoe maoni ya jumla ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu utekelezaji bora wa muswada huu pindi utakapokuwa sheria kama ifuatavyo: 

i. Serikali iimarishe ulinzi wa raia na viongozi sambamba na matumizi ya Sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha na risasi. Itakuwa haina maana sana kuweka sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha na risasi kama wananchi na viongozi watakuwa hawana ulinzi dhidi ya watu wanaotumia silaha kwa malengo ya kihalifu. 

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa ninapowasilisha maoni haya ya Kambi ya Upinzani kuhusu muswada huu, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawana ulinzi wa Serikali. Ni ajabu kwamba Mbunge ambaye kimsingi kazi zake zinamfanya awe na maadaui ambao ni wahalifu na mafisadi anakuwa hana ulinzi wowote wa serikali. 

Kwa mfano maisha ya Mhe. David Kafulila aliyeibua sakata la wizi wa Escrow na kusababisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mawaziri kufukuzwa kazi yako hatarini kwa kuwa hana ulinzi wowote. Lakini wakuu wa Wilaya ambao kazi zao ni kupokea mwenge, kusoma taarifa za UKIMWI na njaa wilayani na kupokea wageni wa kitaifa wana ulinzi majumbani mwao.

Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge mtakumbuka tukio la kuvamiwa na kuchomewa nyumba kwa wabunge wenzetu. Wabunge hawa wangekuwa wamepatiwa ulinzi wa polisi wenye silaha yamkini uvamizi ule ungeweza kuepukika. 

Kwa mantiki hii Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuanzia sasa kutoa ulinzi kwenye nyumba za wabunge na viongozi wengine wanaostahili huduma hiyo kama ambavyo Serikali ya Kenya imefanya kwa wabunge na viongozi wake. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutofanya ubaguzi wa ki-ulinzi kwa viongozi katika mihimili mitatu ya Dola (yani Serikali, Bunge na Mahakama). 

ii. Wabunge wote na viongozi wote wenye hadhi ya kidiplomasia (Diplomats) wawe na sifa za moja kwa moja (direct entitlement) za kumiliki silaha kwa ajili ya kujilinda mara tu wanapopata hadhi hiyo ya kidiplomasia. 

Utaratibu wa kuwatambulisha kwa msajili wa Silaha ili kupatiwa leseni ya umiliki wa silaha ufanywe na taasisi wanazozitumikia. Lengo hapa ni kuepusha mlolongo mrefu wa kuwajadili viongozi walioaminiwa na wananchi walio wengi (kama Rais na wabubunge) au viongozi walioaminiwa kwa kiwango cha juu na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadiliwa na ngazi za chini za uongozi katika vitongoji na mitaa kama ambavyo sheria ya sasa inavyoelekeza. 

Kitendo cha kuruhusu viongozi wakuu walioaminika kujadiliwa na ngazi za chini kama wana sifa au hawana sifa za kumiliki silaha ni udhalilishaji wa itifaki (humiliation of protocol) 

iii. Ulinzi na Usalama ni pamoja na kutambua hadhi na Itifaki.Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutambua hadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya siasa ambao si wabunge lakini vyama vyao vina uwakilishi Bungeni na kuwapa hadhi ya kidiplomasia. Mheshimiwa Spika haiingii akilini kuona kiongozi wa Kitaifa kama Profesa Ibrahim Lipumba ambaye chama chake kina wabunge wengi bungeni na kinaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Zanzibar anakuwa hana hadhi ya ki-diplomasia. 

Kwa upande mwingine inashangaza kuona kiongozi wa kitaifa kama Dkt. Wilbroad Slaa ambaye chama anachokiongoza kinaunda Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pia anakuwa hana hadhi ya kidipolmasia wakati wabunge walioko chini yake wana hadhi hiyo.Mheshimiwa Spika, viongozi wakuu wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi mkubwa bungeni ni viongozi wa Serikali watarajiwa. 

Hivyo kupuuza itifaki na ulinzi wao ni kuiweka nchi katika mtanziko na mashaka. Hili si jambo ambalo mnaweza kuliunga mkono kwa sasa lakini ni jambo muhimu kwenu kuelewa. 

MAONI NA MAPENDEKEZO YA VIFUNGU MAHSUSI

Mamlaka ya Msajili wa Silaha

Mheshimiwa Spika,Mamlaka na majukumu ya Msajili wa Silaha yametolewa chini ya kifungu cha 8(2) cha muswada huu wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha. Lakini kifungu hicho, hakijatoa mwongozo au mipaka ya utekelezaji wa majukumu ya Msajili wa Silaha. Matokeo yake ni kwamba katika maeneo mbalimbali ya sheria hii, Msajili amepewa mwanya mkubwa wa kuamua anavyotaka (discretion). 

Kwa mfano kifungu cha 17 (1) na (2) kinampa Msajili wa Silaha mamlaka ya kutoa kibali cha kumiliki silaha kwa mtu yeyote kwa kipindi ambacho ataamua yeye mwenyewe na kuweka masharti ya kibali hicho yeye mwenyewe. Aidha, Msajili anaweza katika muda wowote kufuta kibali cha umiliki wa silaha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inamtazamo kwamba, ni bora zaidi masharti ya utoaji kibali cha muda, masharti ya muda au kipindi ambacho kibali hicho kitakoma na masharti ya kufuta kibali yakawekwa na sheria na sio kutegemea utashi wa Msajili wa Silaha. Kwa kufanya hivyo, mianya ya rushwa au upendeleo au uonevu wa aina yoyote katika utekelezaji wa majukumu ya Msajili wa silaha inaweza kuzibwa na kuepukwa.

Watu wasio na Sifa ya Kumiliki Silaha 

Mheshimiwa Spika,Katika kifungu cha 26(1) cha muswada huu ipo orodha ya mambo au tabia zinazoweza kumkosesha mtu sifa ya kumiliki silaha. Miongoni mwa tabia hizo ni pamoja na Ukorofi.Kwa kuwa tafsiri ya neno ukorofi ni subjective , na kwa kuwa kila mtu anaweza kutafsiri ukorofi kwa namna yake, hivyo msajili wa Silaha anaweza kuwa na tafsiri yake ya ukorofi kutokana na hisia zake na kumnyima mtu leseni ya kumiliki silaha kwa kisingizio kwamba mtu huyo ni mkorofi. 

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri kwamba neno ukorofi litafsiriwe na sheria hii ili kuondoa mkanganyiko wa tafsiri pindi sheria hii itakapoanza kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, Kifungu 26(2) cha muswada huu kinaeleza kwamba endapo msajili wa silaha ataridhika kwamba kuna sababu za msingi za kuamini kwamba mtu hana sifa ya kumiliki silaha, atatoa notisi ya maandishi akimtaka mtu huyo kufika mbele yake katika muda na sehemu iliyotajwa katika notisi hiyo ili kuonyesha ni kwa sababu gani asitangazwe kuwa hana sifa ya kumiliki silaha. Aidha, ikiwa mtu aliyepewa notisi hiyo atashindwa kuhudhuria katika muda na sehemu iliyotajwa katika notisi, Msajili wa silaha atamtangaza mtu huyo kuwa hana sifa ya kumiliki silaha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kwamba kifungi hiki kina mapungufu. Mapungufu hayo ni pamoja na muda wa kufika mbele ya msajili kutowekwa na sheria na badala yake kuachwa katika utashi (discretion) ya msajili wa silaha; na sharti la kufika mbele ya msajili wa silaha mwenyewe kujieleza kama mtu ana sifa ya kumiliki silaha iwapo kuna mashaka juu yake. 

Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri kwamba muda wa kufika mbele ya msajili uwekwe na sheria ili kuziba mwanya wa uonevu unaoweza kutumika kwa kuweka muda mfupi ili mtuhumiwa ashindwe kufika katika muda huo na kutangazwa kuwa hana sifa ya kumiliki silaha. Aidha, sharti la kufika mbele ya Msajili mwenyewe liondolewe na badala yake sheria iweke wasajili wasaidizi katika mikoa ili kupunguza adha na ghrama za kusafiri kumfuata msajili wa Silaha mmoja ambaye kwa vyovyote vile ofisi yake itakuwa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 26(3) kinasema kwamba cheti cha kuonyesha uwezo, leseni na kibali kilichotolewa kwa mtu aliyetangazwa kuwa hana sifa ya kumiliki silaha vitapoteza uhalali wake kuanzia tarehe ya kutangazwa huko. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inahoji, ni kwa nini Serikali itoe cheti cha kuonyesha uwezo, leseni na kibali kwa mtu ambaye hana sifa? 

Nasema hivi kwa sababu ikiwa Serikali itakuwa makini tangu mwanzo mtu anapoomba leseni au kibali cha kumiliki silaha basi uwezekano mtu huyo aliyekidhi vigezo tangu mwanzo vya kumiliki silaha kupoteza sifa na kutangazwa kuwa hana sifa utakuwa ni mdogo sana vinginevyo awe amekuwa kichaa ghafla.

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 26(4) kinasema kwa pia kwamba mtu aliyetangazwa kuwa hana sifa ya kumiliki silaha, basi atasalimisha katika kituo cha Polisi haraka iwezekanavyo cheti cha kuonyesha uwezo, leseni na vibali vilivyotolewa kwake na silaha pamoja na risasi zilizo katika umiliki wake. 

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kwamba huu unaweza kuwa ni uporaji wa hila wa silaha za wananchi kwa kutumia sheria, kwa kuwa muswada huu haujatamka ni hatua gani zitafuata baada ya mtu aliyetangazwa kuwa hana sifa za kumiliki silaha atakaposalimisha silaha yake na nyaraka za umiliki katika kituo cha polisi. Sheria hii ikiachwa kama ilivyo inaweza kutumika kwa kulipiza visasi au kutekeleza maelekezo yenye nia mbaya.

Utoaji wa silaha na risasi kutoka katika ghala la umma au kituo cha Polisi

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 29(1) cha muswada huu kinaeleza kwamba silaha au risasi zilizohifadhiwa katika ghala la umma, kituo cha polisi au sehemu nyingine yoyote iliyoelezewa na Msajili hazitatolewa humo isipokuwa kwa kibali kilichosainiwa na msajili. Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri kuwe na ugatuzi wa madaraka ili kibali cha kuondoa silaha katika ghala la umma au sehemu nyingine yoyote kiweze kusainiwa na Wakuu wa Polisi wa Mikoa hasa pale kunapotokea dharura mfano ujambazi, uasi, wanyama hatari nk.

Masharti kwa Wauzaji wa Silaha

Mheshimiwa Spika,Kifungu cha 33 cha muswada huu kinampa Waziri mamlaka makubwa ya kutunga kanuni zitakazoweka masharti ya utoaji wa kibali cha muuzaji wa silaha, masharti kuhusiana na eneo la biashara la muuzaji, masharti ya kutolewa upya kwa kibali cha muuzaji na masharti ya kusitishwa, kufutwa kwa muda kwa kibali cha muuzaji wa silaha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza masharti hayo yatajwe na sheria ili kuziba mwanya wa Waziri kutumia madaraka yake vibaya kwa kuweka masharti kandamizi au ya upendeleo kwa baadhi ya makundi ya wauzaji wa silaha.

Upekuzi na Ukamataji wa Silaha

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 54 cha muswada huu kinasema kwamba “Hakuna mashtaka au hatua zozote za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya Msajili au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa anayetekeleza majukumu yoyote chini ya sheria hii kwa lolote atakalolitenda wa nia njema”

Mheshimiwa Spika, Hakuna utendaji bora usiokuwa na mipaka. Kifungu hiki kinaweza kutumika vibaya kwa kuwa kinatoa mwanya mkubwa kwa Msajili au afisa yeyote aliyeidhinishwa kupekua au kukamata silaha kufanya jambo lolote hata kama ni ovu kwa kisingizio cha “nia njema. Hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba sheria hii imtake msajili au afisa aliyeidhinishwa kuzingatia kanuni na taratibu za upekuzi na ukamataji, kwani kumiliki silaha kihalali sio kosa la jinai hivyo upekuzi na ukamataji uzingatie taratibu za kisheria hasa kwa wale wanaomiliki silaha kihalali. 

Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya marekebisho ya baadhi ya vifungu yataletwa katika jedwali la marekebisho wakati wa Kamati ya Bunge zima.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, Imekuwa ni desturi kwa Serikali zilizoko madarakani kuleta miswada ya sheria kwa ajili ya kulinda maslahi yake yenyewe bila kujali maslahi mapana ya wananchi na taifa kwa jumla. Aidha, imekuwa ni desturi sheria nyingi kupitishwa haraka hara bila kupata maoni ya wadau wengi jambo ambalo husababisha sheria nyingi kupingwa kabla hata hazijaanza kutumika. Mfano halisi ni Muswada huu kutoshirikisha wadau ipasavyo. Wadau wengi walilalamika mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kwamba hawakushirikishwa kabisa katika mchakato wa kuandaa muswada huu. 

Kambi Rasmi ya Upinzani inaihoji Serikali ni kwa nini inapuuza wadau katika sheria muhimu kama hii? Je, Serikali haioni kuna athari kubwa kiulinzi na kiusalama kwa kutowashirikisha wadau wakubwa wa silaha na risasi kama vile makampuni ya ulinzi binafsi, na wafanyabiashara wakubwa wa silaha hapa nchini?

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza tena kwamba Amani na utulivu wa nchi hii hautategeme tu uwepo wa sheria ya udhibiti na usimamizi wa silaha na risasi bali uongozi unaozingatia misingi ya utawala bora, haki, usawa, ukweli na usitawi wa jamii nzima kwa jumla. Aidha, ugumu wa maisha unaosababishwa na umasikini uliokithiri kutokana na mfumuko wa bei, elimu duni, maradhi, ukosefu wa ajira, ukosefu wa maji safi na salama nk. ni viashiria vikubwa vya uvunjifu wa amani kuliko silaha na risasi ambazo Serikali inafanya bidii kubwa kutungia sheria.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni bado inaitaka Serikali kukumbuka na kuzingatia barabara masuwala manne muhimu iliyotahadharisha yasichezewe au kufanyiwa mzaha kwani yanaweza kuliingiza taifa katika machafuko. 

Masuala hayo ni kuchezea haki ya mwananchi kujiandikisha kuwa mpiga kura, Kufanya Mzaha na uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi, Matumizi ya Kisiasa ya Jeshi la Polisi na Ulinzi wa Raia na Mali zao hususan ulinzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Mheshimiwa Spika,Baada ya kusema hayo, kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, naomba kuwasilisha.
Godbless Jonathan Lema (Mb)

MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
NA WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI

ZILIZOSOMWA ZAIDI