NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Thursday, July 31, 2014

MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM

1a
MARAIS wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Festus Mogae wa Botswana wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Africa Readership Forum ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia changamoto hizo.
2a
Rais mstaafu wa wa Afrika Kusin Thabo Mbeki akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
3a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini katikati ,Festus Mogae wa Botswana kushoo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa wakiwa wakiongoza mkutano huo.
4a
Baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
5a
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe katikati ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katik mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
6a
Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye kulia ni Mh. Balozi Ali Karume walikuwa ni miogoni wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo pia.

MCHEKI WEMA AKIWA NA "SHEMEEEJI" OMMY DIMPOZ *PICHAZ*


'TUNATUMIA MAITI 25 KWA MWAKA KUFUNDISHIA' - MUHAS

WAKATI sakata la kuokotwa kwa viungo vya binadamu likiendelea kutikisa nchi, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), kimesema kuwa hutumia maiti 25 kwa kuwafundishia wanafunzi kila mwaka.
Pia chuo hicho hakijawahi kuagiza maiti kutoka nje ya nchi na kwamba ni mtu mmoja tu aliyewahi kutaka maiti ya mtoto wake itumike kufundishia.
Kauli hiyo ya MUHAS imekuja siku chache baada ya Serikali kuamua kuifungia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), baada ya kubaini kasoro kadhaa katika utendaji wake.
Juzi, Serikali ilifanya ukaguzi wa kushtukiza IMTU, baada ya hospitali hiyo kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Hata hivyo, wakati Tume ya Watu 15 iliyoundwa na Serikali kuchunguza suala hilo ikiendelea na kazi, Mkuu wa Kitengo cha Anatomy MUHAS, Profesa David Ngassapa amebainisha kuwa chuo hicho hutumia maiti 25 kwa mwaka.
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jana, Ngassapa alisema kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza hutumia maiti 20, huku madaktari wanaorudi chuoni hapo kwa ajili ya mazoezi wakitumia maiti tano.
“Sheria ya mwaka 1963 inatutaka baada ya matumizi tuondoe mwili kwa heshima zote na miongoni mwa vitu ambavyo wanafunzi wanasisitizwa ni kuhakikisha wanaiheshimu miili hadi hatua za mwisho,”alisema Ngassapa.
Alieleza kuwa pamoja na sheria kutoa ruhusa ya kutumia maiti katika mafunzo, bado imeweka vipengele vinavyowataka madaktari kuiheshimu miili ya watu, hadi hatua ya mwisho.
Ngassapa aliongeza: “Sheria inaruhusu kuhifadhi mabaki ya miili kwa njia mbili; kuizika na kuichoma moto, pia hospitali inaweza kuhifadhi mabaki hayo hata kwa miaka mitano.”

HAJAWAHI KUAGIZA MIILI KUTOKA NJE
Akizungumzia utaratibu wa nchi kubadilishana maiti kwa ajili ya mafunzo, Profesa huyo alisema kuwa kwa zaidi ya miaka 30 aliyokuwa katika kitengo hicho, hawajawahi kuagiza maiti kutoka nje ya nchi.
Alisema maiti zilizopo nchini zinatosha kufundishia wanafunzi wote wa udaktari kwa kuwa siyo Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH), pekee inayotegemewa kutoa miili hiyo.
Alisema kuwa siku za nyuma, Serikali ilikuwa ikiagiza mifupa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo, lakini sasa kila kitu kinafanyika hapa nchini.
Ngassapa alisema kuwa miili iliyoharibika kwa ajali au magonjwa haifai kutumiwa kwa kuwa mwanafunzi anatakiwa kujifunza kwenye mwili uliokamilika.

AMKUMBUKA MTU ALIYETOA MAITI YA BINTI YAKE
Alisema kuwa historia ya Tanzania inaonyesha kuwa ni mtu mmoja pekee ndiye aliwahi kujitolea maiti ya binti yake ili itumike kufundishia.
“Alijitolea kwa kuwa binti yake huyo alianza kuugua akiwa na umri wa miaka miwili hadi alipofikisha miaka 12, muda mwingi akiwa amelazwa hospitalini hapa,” alisema.
“Alipofariki dunia mzazi alisema mtoto huyo ni wa hospitali na anamtoa kwa ajili ya matumizi ya hapa. Ibada ya mazishi ilifanyika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti,” alisema Ngassapa.
Alifafanua kuwa hata baada ya kukabidhiwa maiti hiyo, waliendelea kumhifadhi kwa miaka minne, hadi walipojiridhisha kuwa wazazi hawatabadilisha mawazo.
Sheria inayotumika
Mkuu huyo wa kitengo kinachoshughulikia mwili na viungo vyake, alisema kuwa sheria ya Serikali ya mwaka 1963, ndiyo inayoruhusu chuo chochote cha afya kuchukua mwili kama umekaa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa siku 14 bila ndugu kujitokeza.
Ngassapa alifafanua kuwa licha ya sheria kuwataka kuchukua mwili uliokaa katika kipindi hicho, chuo huuhifadhi mwili huo kwa siku 30, ili kujiridhisha pasipo shaka kwamba hakuna ndugu anayejitokeza kuuchukua.
Alibainisha kuwa baada ya hapo, huuweka dawa ili usiharibike, kisha huuacha kwa wiki mbili au tatu zaidi wakisubiri kama ndugu wanaweza kujitokeza.
“Inapothibitika kuwa hakuna anayejitokeza, chuo huuchukua na kuutumia kwenye mafunzo,”alisema.
Alifafanua kuwa sheria pia inakitaka Kitengo cha Anatomy kuandika barua kwa mkuu wa chuo na Mahakama Kuu, kutaarifu kuwa wamechukua mwili kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia juzi aliliambia Mwananchi kuwa miili ni mali ya Serikali na kwamba chochote kinachofanyika kwa binadamu lazima kifuate sheria zilizowekwa na Serikali.
Pia alisema kwamba sheria inaruhusu nchi kubadilishana maiti, lakini hana uhakika kama jambo hilo limewahi kufanyika nchini, ingawa ana uhakika kuwa haiwezekani hospitali zikakosa maiti za kufundishia.
Chanzo: Mwananchi

KWA MWENDO HUU VIGODORO BADO VINAENDELEA PAMOJA NA SERIKALI KUPIGA MARUFUKU

Huku wakiendelea….
Dada huyu ambaye jina lake halikufahamika mara moja akikata mauno huku akionesha nguo yake ya ndani mbele ya kadamnasi bila hata chembe ya haya…!
Picha: The choice

IYANYA AWASHUSHIA UJUMBE MZITO WIZKID NA DAVIDO JUU YA BEEF YAO!

Iyanya atoa ushauri kwa Wizkid na Davido kuhusu beef kati yao
Ingawa wawili hao waliwahi kuonekana katika picha ya pamoja na kutoa ishara ya kumaliza tofauti zao, bado maandishi yao yanaonekana kuwa mwiba kwa kila mmoja.
Mkali wa Kukere ameamua kutoa ushauri wake kwa wasanii wa Nigeria, ushauri ambao unaonekana kumwagusa moja kwa moja Wizkid na Davido ingawa hakuwataja majina.
“Acheni kuongea!!! Tuachie muziki zaidi!!! Tuwaburudishe mashabiki!!! Acheni chuki!!! Maombi yangu ni kwamba wote tufanikishe.”
 

WATU WANNE WAMEFARIKI PAPO HAPO BAADA YA KUDONDOKEWA NA KUFUNIKWA NA LORI LA MIZIGO

 Lori hilo la mizigo likiwa limedondoka Chini ya Mto njia panda ya Ilembula huku  watu wanne wakiwa wamefunikwa.
WATU wanne wamefariki papo hapo Saa kumi usiku leo baada ya kudondokewa na Lori la mizigo , Lililopindukia katika mto njia panda ya kuelekea Ilembula, kutokana na kufunikwa na Lori hilo watu hao wameendelea kuwa chini ya Lori hilo na Kazi ya kuwatoa inaendelea.
 Baadhi ya watu wakiwa wanashuhudia tukio la ajali huku wengine wakijipanga jinsi ya kuwaokoa walifunikwa na kifusi.
 Baadhi ya mizigo ikiwa imedondoka katika mto
 Hivi ndivyo Lori linavyo onekana likiwa limedondoka chini ya mto eneo la njiapanda Ilembula
 Mashuhuda wakiwa wanaongezeka kufika katika eneo la Tukio

 Kazi ya uokoaji ikiwa imeanza 
 Lori la mizigo likiwa limedondoka
 Picha zote na Njombe yetu Blog

UMEONA STAILI MPYA YA UVAAJI WA MSANII CHRIS BROWN AMBAYO IMEKUWA GUMZO MTANDAONI


Staili mpya ya Chris Brown kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa la BET 2014.
Vazi hili lilobuniwa na mbunifu Seth Chernoff na pia staili hii ya kuvaa shati lenye langi nyekundu kiunoni ndio habari ya mjini kwa sasa baada ya mastaa kibao kuanza kuivaa.
Na pia raba kali zilizobuniwa na msanii mwenzake Kanye West zinazojulikana kwa jina la “Nike Air Yeezy Red”
Rihanna nae hayuko nyuma san kwenye Fashion alitupia pia

ZITTO AKOSA IMANI NA UKAWA: ASEMA HANA IMANI KAMA UMOJA HUO UTADUMU

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kwa mara ya kwanza ameibuka na kupingana na harakati za Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). 
Zitto amesema hana uhakika wala hauamini Ukawa kama utakuwa umoja endelevu hadi kufikia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, kwa sababu si mara ya kwanza vyama vya upinzani kuungana na kugawanyika. 
Mbali ya kutokuwa na imani na umoja huo, pia ameitaka Serikali kusitisha mchakato wa Katiba Mpya hadi uchaguzi mkuu utakapomalizika. 
Alisema ni vema mchakato huo ukasitishwa kwa sasa, kwani inaonekana wajumbe wa Bunge hilo wanafuja fedha za umma.
Zitto alitoa kauli hiyo juzi, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds cha jijini Dar es Salaam.
Alisema Watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi na si Katiba pekee.
Alisema siku zote Watanzania wamekuwa wakipenda kuwa na upinzani imara ambao watu wanaweka tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya chama ambacho kinaongoza, lakini haoni kama Ukawa utaendelea hadi kufikia kipindi cha Uchaguzi Mkuu.
Alisema hatua ya kusimama kwenye ajenda moja ya Katiba haitausaidia umoja huo, kwani kipindi cha uchaguzi mkuu kinakuwa na ajenda nyingi.
Alisema wananchi watapenda kusikia masuala ya kushughulikia rushwa, matumizi ya rasilimali, maji, umeme, afya na barabara.
“Mambo haya ndiyo yatakayowafanya wananchi waamue namna gani watakabidhi dhamana ya uongozi, si suala la Katiba pekee,” alisema Zitto.
Alisema tusijitoe ufahamu kwa kudhani kwamba hii ndio mara ya kwanza kwa upinzani kuungana. 
“Kulikuwa na Kamati ya Mabadiliko ya Katiba (KAMAKA) pia katika chaguzi za mwaka 1995, mwaka 2000 wapinzani waliungana vilevile, lakini kila inapokaribia uchaguzi wamekuwa hawaelewani kwa kuwa kila mtu anataka chama chake kipeperushe bendera.
“Lakini kama Ukawa wataweza kuweka ajenda yao mpaka mwisho itakuwa jambo jema kwa wananchi wenyewe. Kwa sababu nchini kwetu tatizo kubwa ni usimamizi na uwajibikaji, kama ajenda itachukua nafasi naamini hali haitakuwa mbaya, lakini bado siamini na sina uhakika kama umoja huu ni endelevu kwa namna ambavyo tunaona, ni umoja ambao unatokana na matakwa ya sasa ya Katiba, wameungana kwa sababu ya serikali tatu, lakini aina gani ya serikali bado hili linaweza kuwagawa,” alisema.
…MCHAKATO WA KATIBA MPYA USITISHWE...
Akitolea ufafanuzi hoja yake ya kusitisha mchakato wa Katiba Mpya, Zitto alisema ni vyema serikali ikausitisha ili kunusuru fedha za umma zisiteketee.
Alisema fedha hizo zinastahili kutumika kununua madawa, kuendeleza miradi ya maji na kusomesha Watanzania, hivyo hakuna sababu fedha hizo kutumika kwa ajili ya kupiga porojo na kutukanana ndani ya Bunge.
“Nashauri tuahirishe mchakato huu mpaka baada ya uchaguzi mkuu mwaka kesho, ndipo hapo tuwe na mamlaka ya kujadili mchakato huu na kumaliza.
“Pia uchaguzi unaweza kuchekecha na ukaondoa baadhi ya watu ambao ni vikwazo katika mchakato kwa sababu uchaguzi hauna muamala, mtu ambaye alikuwa mbunge anaweza kuondolewa,” alisema.
Aidha, alisema kabla ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu, Katiba ya sasa inatakiwa kurekebishwa baadhi ya maeneo ambayo ni vikwazo, kama vile Tume huru ya uchaguzi, kipengele cha wagombea binafsi kiwekwe na maeneo ambayo Zanzibar wamekuwa wakiyahitaji katika Katiba mpya, kwa mfano suala la mafuta na gesi yawekwe.
Alisema hakuna sababu ya kugawa nchi na kutumia rasilimali zilizopo kwa kufanya kazi ambayo haina matunda.

…AMTETEA JANUARY...
Katika hatua nyingine, Zitto, ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisema amesikitishwa na mashambulizi yanayoelekezwa kwa Mbunge wa Bumbuli (CCM), Januari Makamba, baada ya kutangaza nia ya kuwani urais mwaka 2015.
Mbunge wa Bumbuli, Mhe. January Makamba (CCM).
Alisema kila kijana anapojitokeza kwa ajili ya kutaka kushiriki katika mamlaka za nchi, hasa katika nafasi kama hiyo ya urais, kumekuwa na mashambulizi makubwa dhidi yake.
“Ni hatua ambayo sio nzuri kwa sababu kwa mujibu wa takwimu, idadi ya watu asilimia 72 wapo chini ya miaka 30, asilimia 65 ya wapiga kura ni vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 40, hivyo vijana wana haki ya kushiriki katika uongozi wa nchi, tufahamu changamoto za maendeleo ya nchi yetu zinahitaji uongozi mpya wa kizazi kipya.
“Ni dhahiri neno ujana si sifa, lakini neno uzee pia si sifa, hivyo tunatakiwa kuwapima vijana kwa sifa zilizopo, kama vile za kikatiba na zile za ziada, badala ya kusema vijana hawajakomaa… nilisikitika sana na mashambulizi ambayo yalielekezwa dhidi ya Makamba, natoa wito kwamba tuache, kwani wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi.
“Mtu akigombea na kama akitoa sera zake vizuri wananchi wakamwelewa, akichaguliwa ni wananchi wameamua, hakuna mtu mwenye mamlaka kuwa fulani ni kijana, nadhani lazima tubadilishe uongozi na watu wajue nchi hii ni ya vijana, hatusemi wazee hawawezi ila wao wabaki kuwa washauri kama wao walivyokuwa vijana katika kipindi cha Nyerere nao walikuwa na miaka 40. Hivyo kuna haja ya kuweza kufikia hapo, changamoto za nchi ni kubwa, kuna haja ya aina mpya ya uongozi na mimi naamini aina hiyo itatoka kwa viongozi vijana,” alisema.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Zitto, ambaye yuko ndani ya Chadema kwa sababu za kisheria, kuibuka na kuuzungumzia Ukawa.
Mwanasiasa huyo kijana amekuwa kimya kwa muda mrefu, hata kwenye harakati za Ukawa amekuwa aghalabu kuonekana, hali ambayo imekuwa ikiibua maswali yuko upande gani katika mchakato huu wa Katiba Mpya.
Kauli hii ya Zitto inaweza kuibua fikra mpya kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa na imani kubwa na umoja huo unaoviunganisha baadhi ya vyama vya siasa nchini.

UPDATES..!! KUHUSU AJALI YA BASI LA MORO BEST ILIYOTOKEA MKOANI DODOMA!

WATU 11 kati ya 17 waliofariki dunia papohapo katika ajali eneo la Pandambili wilayani Kongwa, Dodoma wametambuliwa na wanne kati yao tayari wamechukuliwa na ndugu zao.
Ajali iliyosababisha watu 56 kujeruhiwa vibaya. iliyahusisha magari mawili ambayo ni basi aina ya Scania mali ya Kampuni ya Morobest lililokuwa likitokea Mpwapwa kwenda Dar es Salaam, ambalo liligongana na uso kwa uso na lori lenye tela, lililokuwa limepakia shehena ya mabomba.
Ajali hiyo ambayo ilisababisha vifo vya madereva wa magari hayo, ilitokea meta chache kutoka mahali ilikotokea ajali iliyosababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime aliielezea tukio hilo lilitokea saa 2 asubuhi kuwa miongoni mwa ajali mbaya ambazo zimetokea mkoani humo katika siku za karibuni.
“Ni watu 17 ambao wamekufa hapa hapa, kati ya hao 12 ni wanaume na wanawake ni watano, majeruhi ni 56, kati yao tisa wana hali mbaya zaidi,” alisema Misime.
Hadi jana jioni maiti za watu kumi na moja walikuwa wametambuliwa na wanne kati yao walichukuliwa na ndugu zao.
Waliotambuliwa ni Gabriel Lemanya (Dereva wa lori) ambaye ni Mkazi wa Ndebwe wilaya ya Chamwino, Said Lusogo (dereva wa basi), Omari Mkubwa (kondakta wa basi) na Mikdadi Zuberi ambaye alikuwa ni utingo wa lori.
Wengine ni Justin Makasi, Gabriel Chiwipe, Marick Masawe na Melina Maliseli, Wilson Sudai (wote wakazi wa Mpwapwa) watu wawili walitambulika kwa jina moja ambao ni Christina (Mpwapwa) na Nasibu mkazi wa Kongwa.
Ilielezwa kuwa amu zilikuwa zimetapakaa katika sehemu kubwa ya barabara ilikotokea ajali hiyo na kwamba magari hayo yalikuwa yameharibika vibaya sehemu za mbele. Kadhalika baadhi ya mabomba yaliyokuwa kwenye lori yalikuwa yamerushwa umbali wa karibu meta 20 kutoka eneo la ajali.
Mashuhuda walisema Polisi wa Kituo cha Kongwa walifika katika eneo la ajali muda mfupi tu baada ya magari hayo kugongana na kwamba walisaidia kudhibiti usalama wa mali za abiria, zikiwamo simu za mkononi zaidi ya 20 ambazo zilikabidhiwa kwa uongozi wa polisi Mkoa wa Dodoma.
MASHUHUDA WAZUNGUMZA
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Christopher Kangoye ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza kufika katika eneo la tukio, alisema chanzo cha ajali hiyo kilikuwa ni uzembe uliofanywa na dereva wa lori ambaye kwa sasa ni marehemu.
“Watu wote niliowahoji walimtaja dereva wa lori kuwa ndiyo chanzo na hata ukiangalia mwenyewe utaona jinsi alivyomfuata mwenzake katika eneo lake, hali ni mbaya sana,” alisema Kangoye.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mpwapwa, Dickson Kimaro alisema dereva wa lori alikuwa akitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake, ndipo ghafla akakutana uso kwa uso na basi.
Kimaro alisema wilaya ya Kongwa mbali na kupokea miili ya marehemu, ilifanya juhudi za kupeleka timu ya waganga pamoja na magari ya kubeba majeruhi ambao waliwahishwa katika hospitali ya Kongwa na wengine Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Mmoja wa majeruhi, Safari Balaigwa alisema kuwa walikuwa katika mwendo wa kawaida lakini ghafla waliona lori likija mbele yao na kugongana na basi uso kwa uso.

HIVI NDIVYO CHRISS BROWN ANAVYOSHI NA MAJIRANI ZAKE KWA SASA!

Picha hii haihusiani na stori hapo chini: Chriss Brown akiwa katika mona ya action alizozifanya katika movie.
MWIMBAJI wa Loyal, Chris Brown ambaye alitoka jela hivi karibuni na kuamua kutafuta amani kwa kuhama nyumba aliyokuwa akiishi kukwepa ugomvi na majirani zake ni kama ameruka majivu na kukanyaga moto.
Kwa mujibu wa TMZ, mwimbaji huyo aliamua kuuza nyumba yake ya kifahari iliyokuwa Hollywood Hills kufuatia ugomvi wa kila siku na majirani zake waliomfikisha kwenye vyombo vya sheria mara kadhaa kwa madai ya kuwanyima raha na familia zao kwa vitendo vyake. Baada ya kuuza nyumba hiyo alinunua nyumba mpya, California.
Kwa bahati mbaya majirani wapya wa mwimbaji huyo wanaonekana kuwa na maamuzi magumu zaidi ya wale wa awali waliokuwa wanampeleka kwenye vyombo vya sheria.
Akiongea na TMZ, jirani mmoja alieleza kutofurahishwa kwake na ujio wa Chris Brown kwenye ujirani wao na kuahidi kuwa endapo atagusa nyumbani kwake atampiga risasi.
“It can be the devil. I can care less.. I don’t care if they are having orgies. It can even be Sadam Hussein for all I care, as long as he doesn’t trespass onto my property. If he does, I shoot him.”
Jumba jipya la Chris Brown lina vitu vya kifahari kama uwanja wa kuchezea tennis, dance studio, club house, commercial ice cream bar na mengine mengi huku eneo zima likuwa na ukubwa wa eneo la mraba futi 8,000 na vyumba sita vya kulala.

ALICHOFANYIWA MICHELLE OBAMA NA MUMEWE OBAMA MMH!!, HATA UWE KAUZU VIPI, LAZIMA UCHEKE *PICHAZ*

Eti huyu ndio mke wa rais wa marekani, Michelle
Mwenyewe Rais Obama.

WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 51 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI MATUNDASI - CHUNYA

MMG23716
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 31.07.2014.
  • WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 51 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI MATUNDASI WILAYANI CHUNYA.
  • MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI JIJINI MBEYA.
  • MTOTO WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA WILAYANI CHUNYA.
  • MTOTO WA MIAKA KUMI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA NA SHOTI YA UMEME.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
 WATU WANNE WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. PAULO MWASANGA (18) MKAZI WA KITONGOJI CHA MATUNDASI ‘B’ 2. WEDI ANGOLWISE (21) MKAZI WA MATUNDASI 3. SALOME MWAKIBETE (13) MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI SAMBILIMWAYA NA 4. OBEDI MWAKAMELA (25) MKAZI WA MATUNDASI WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.595 CHU AINA YA FUSO TIPPER LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA KIPINDUKA KATIKA KIJIJI CHA MATUNDASI WILAYANI CHUNYA.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MATUNDASI “B”, KIJIJI CHA MATUNDASI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA CHUNYA/MAKONGOLOSI.
 GARI HILO LILIKUWA LIKITOKEA KIJIJI CHA SAMBILIMWAYA KUELEKEA KIJIJI CHA MATUNDASI LIKIWA LIMEBEBA WACHEZAJI WA MPIRA WA MIGUU NA MASHABIKI. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 51 WALIJERUHIWA, KATI YAO 26 WALITIBIWA NA KURUHUSIWA NA WENGINE 25 WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA CHUNYA WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

 KATIKA TUKIO LA PILI:
 MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA WILE PETER AMBAYE ALIKUWA ABIRIA KATIKA PIKIPIKIAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI DFP 0036 AINA YA BENZ MALI YA SHIRIKA LA UMEME TANESCO LILILOKUWA  LIKIENDESHWA NA PATRICK MHAGAMA (46) MKAZI WA ILOMBA JIJI MBEYA KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE NA KUSABABISHA KIFO KWA ABIRIA HUYO.
 AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 31.07.2014 MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO NZOVWE, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

 KATIKA TUKIO LA TATU:
 MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITATU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA PASCALIA JIFULA NGASA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KUFUNIKWA NA KIFUSI CHA MCHANGA KATIKA KITONGOJI CHA CHIZYA WILAYANI CHUNYA.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 08:300 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA CHIZYA, KIJIJI CHA MWAMBANI CHINI, KATA YA MWAMBANI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA, MTOTO HUYO ALIKUWA AKICHEZA NA WATOTO WENZAKE KWENYE GEMA LA MCHANGA NA NDIPO KIFUSI KUMUANGUKIA NA KUMFUNIKA.
 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUANGALIA MAZINGIRA YA MAENEO YAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.

 KATIKA TUKIO LA NNE:
 MTOTO WA MIAKA KUMI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JERRY JESTED, MWANAFUNZI NA MKAZI WA MLOWO WILAYANI MBOZI ALIKUTWA AMEKUFA CHUMBANI KWAKE BAADA YA KUPIGWA NA SHOTI YA UMEME.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI BAADA YA MAREHEMU KULAMBA NYAYA ZA UMEME AMBAZO ZILIKUWA KARIBU NA KITANDA CHAKE HALI ILIYOPELEKEA KUPIGWA SHOTI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE.
  KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUANGALIA MAZINGIRA YA MAENEO YAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA MBALI VITU VYA HATARI KWA WATOTO.
Imetolewa na kusainiwa na:
 [BARAKAEL .N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MAUAJI SIKUKUU: AUAWA KWA KUCHOMWA VISU

Binti anayefahamika kwa jina la Salma Khamis (21) aliyechomwa kisu na mchumba wake, Omary Idd.
SIKU mbili kabla ya Sikukuu ya Eid el Fitr, binti aliyefahamika kwa jina la Salma Khamis (21) (pichani), amekumbwa na mauti kufuatia kuchomwa visu mwilini na mchumba wake aliyetajwa kwa jina la Omary Idd. 
Tukio hilo lilitokea Julai 27, mwaka huu katika Kijiji cha Mnemela  wilayani Kibaha, Pwani kufuatia ugomvi wa mara kwa mara wa wawili hao unaosadikiwa ulitokana na wivu wa mapenzi. Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanaume huyo alikuwa akimtuhumu Salma kwamba alikuwa na mwanaume mwingine mwenye gari, hivyo yeye akajiona hana chake ndiyo chanzo cha kuamua kumtoa uhai msichana huyo ambapo alimfuata kwa mama yake mkubwa alikokuwa na kumchoma visu mwilini hadi kufariki dunia. 
Akisimulia tukio hilo la kusikitisha, baba mzazi wa marehemu Salma, Khamis Mbegu alisema kifo cha binti yake kimemuuma sana kwani ameuawa kinyama na siku alipopata taarifa hakuamini.
Ndugu na jamaa wa karibu wakiuaga mwili wa marehemu,Salma Khamis.  
 “Sikutegemea haya yaliyotokea, ni kweli walikuwa na ugomvi, wakaja kwangu kuwasuluhisha ndicho tulichokifanya, lakini  Salma alionesha msimamo wake wa kutokuendelea kuwa na Omary kwa sababu ya mateso na masimango aliyokuwa akimfanyia. “Alishawahi kumpeleka porini na kutaka kumuua kama tu angesema hampendi, ikabidi aseme anampenda ili kuokoa uhai wake, hivyo alikuwa na shaka naye ndiyo maana hakutaka kuendelea na uchumba wao,” alisema baba huyo. Aidha, ilielezwa kuwa mtuhumiwa ni mwenyeji wa Mkoa wa Singida, hivyo hata ndugu wa marehemu Salma hawajui anatoka kijiji gani wala kumtambua ndugu yake yeyote. 
Kufuatia tukio hilo la mauaji, mtu mmoja anayedaiwa ni mshenga wa Omary, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa upelelezi zaidi. Kamanda wa polisi wa mkoa huo, SACP  Ulrich Matei  alisema taarifa za kifo hicho amezipokea ambapo marehemu alichomwa visu sehemu mbalimbali za mwili na mtuhumiwa alikimbia lakini mshenga wake anashikiliwa kwa upepelezi zaidi kwa kuwa ndiye aliyekuwa ameongozana naye.
Chanzo: GP

MWADUI FC YAWAITA WALIOTEMWA SIMBA, YANGA KUFANYA MAJARIBIO LEADERS CLUB DAR

Kocha wa Mwadui fc, Jamhuri Kiwhelo 'Julio'
Na Baraka Mpenja
TIMU ya Mwadui fc ya Shinyanga inatarajia kuanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi daraja la kwanza unaotarajia kuanza mwezi Octoba mwaka huu.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Jamhuri Musa Kiwhelu ‘Julio’ amesema mazoezi hayo yataanza katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa Mwadui watahudhuria.
“Tunaanza mazoezi kesho katika viwanja vya Leaders kwa baadhi ya wachezaji wa Mwadui kuhudhuria. Tunatarajia kuwa na timu bora yenye ushindani mkubwa, kwahiyo Kesho saa kumi jioni tunaanza mazoezi,” Alisema Julio.
Julio aliongeza kuwa klabu yake inahitaji kufanya usajili wa wachezaji wengine kwasababu muda unakimbia sana.
Kocha huyo alibainisha kuwa wameamua kuitisha majaribio ya wachezaji, hivyo kwa wote wanaojiona wana vipaji wafike kesho Leaders.
“Wachezaji walioachwa Simba, Yanga wafike kujaribiwa. Tunawakaribisha watu wote wenye uwezo,” Alisema Julio.

KINGWENDU ATOA KAULI HII BAADA YA MKEWE KUBAKWA YEYE AKIWA SAFARINI

MUIGIZAJI wa filamu za Kiswahili, mchekeshaji Kingwendu yuko katika wakati mgumu baada ya mkewe kubakwa na jirani yake wakati akiwa amelewa pombe.
Muigizaji huyo amesema kuwa alizipata habari hizo wakati ambapo yuko safarini na majirani walimueleza kilichotokea kuwa mkewe na jirani huyo aliyembaka mida ya saa tano usiku wote walikuwa wamelewa.
”Kama ulivyosikia hiyo habari, mimi nilikuwa sipo ndo nimerudi jana, nataka nianze kufuatilia sheria sema sasa hivi nimefiwa na dada yangu tunapeleka msiba kijijini na baada ya hapo ninapumzika kesho tu halafu ninasafiri Nairobi, nikirudi Nairobi tarehe tano kuanzia tarehe sita ndo naanza kufuatilia.” Amesema Kingwendu.
Mchekeshaji huyo ameumizwa na kitendo hicho na ameamua kufuata taratibu za kisheria ili haki itendeke.
“Kutokana na kitendo alichokifanya na mimi nimejisikia vibaya, inanibidi nimtafute huyu bwana nimpate ili nimpeleke mahakamani, mke wangu bado niko naye, sema huyu jamaa aliyefanya unyamaa huu yupo jirani. 
Mke wangu alikuwa amelewa na jamaa naye alikuwa amelewa. Mke wangu sijui alikuwa anatoka wapi saa tano usiku ndo akakutana na huyo jamaa, majirani ndio walivyoniambia hivyo, walinipigia simu wakati nipo Shinyanga huko.”
Chanzo: Bongo5

SHILOLE ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBONI IGUNGA 2015

Shilole si mgeni katika kuota vitu vikubwa. Kutoka kwenye ndoto yake ya kufanya kolabo na Jennifer Lopez, awamu hii ameenda mbali zaidi.
 MUIMBAJI huyo amechoka ‘Kuchuna Mabuzi’ na sasa anataka kuingia mjengoni. Mrembo huyo ambaye jina lake halisi ni Zuwena Mohamed, amepanga kugombea ubunge kwenye jimbo analotokea la Igunga mkoani Tabora katika uchaguzi wa mwaka 2015!
Akizungumza kwenye kipindi na Sizi Kitaa cha Clouds TV, Shilole amesema yupo serious na nia hiyo na kama Mungu akipenda atakuwa mbunge wa jimbo hilo.
“Baada ya Dokta Dalali Kafumu anayefuata ni mimi,” amesema Shilole. 
 “Mimi nadhani napenda jimbo langu na napenda wakazi wangu wa Igunga wananiona toka nakua mpaka sasa hivi, kwahiyo wanafurahi. Sasa wananiambia ‘sisi hatutaki kumpa mtu mwingine kiti hiki sasa wananipa changamoto. 
"Vitu viwili vya kwanza ambavyo nitavifanya nikiingia kwenye lile bunge nikiwa kama msanii, kwanza nitatetea haki za wasanii, cha pili Igunga yangu wapo wakazi wa Igunga vijana wapate kazi, yaani akina mama, wale mama lishe na wengine lazima wawe na kazi zao. Kwahiyo nitawatafutia kazi, nitajenga chuo cha muziki,” alijinadi muimbaji huyo.
“Mimi jimbo langu nalijua na nimekua pale mpaka nimekuwa mkubwa lazima nilitimize sitaki wananchi wangu wapate tabu. Mimi nadhani wanaoenda kugombea majimbo yasiyo ya kwao wanaweza fanya chochote, lakini kama ni wa hapo lazima itakuuma. 
"Lakini unakuta mtu wa Dar es salaam anakwenda kugombea Mtwara huko nani anamjua? Mimi nitaenda kugombea kwangu lazima nitapata kura lazima watanipa! Kwahiyo kaeni tayari Shilole ni mbunge mtarajiwa Igunga,” alitamba.

MAPENZI: NI JINSI GANI UNAMWOMBA MPENZI WAKO MSAMAHA, JE NI KWA KUMPA ZAWADI?

MSAMAHA una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno  hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. 
Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili,Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama; yaishe,basi samahani,umeshinda, sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili).
Jinsi yakutumia samahani kiusahihi.
Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. 
Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali.
Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. 
Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya.
Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .
Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa.
Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya kudai msamaha. 
Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na uwepo wake katika maisha yako. 
Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati unamplease mpenzi wako.
Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa pindi tu unapomletea zawadi. 
Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au umetenda kosa gani tena.
Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba msamaha.
Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi
    Kubali kosa pale ambapo umetenda, (note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza, au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa)
    Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa.
    Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe)
    Usilazimishe kusamehewa, yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine. Hapa itategemea na jinsi mlivyo
Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa  bahati mbaya. 
Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema;''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea.
Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. 
Timiza malengo yako,
jiheshimu, kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU AJALI YA BASI LA MOROBEST KUGONGANA NA LORI ILIYOTOKEA DODOMA

Capture5
JULY 30 imesambaa Taarifa ya ajali ambayo imetokea mapema leo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma ajali iliyosababisha vifo vya watu 17 kati yao wanaume 12, wanawake 5 na majeruhi kwa mujibu wa jeshi la Polisi Dodoma.
Capture4
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 08:00 asubuhi eneo la Pandambili barabara ya Dodoma –Morogoro ambayo imehusisha basi la kampuni ya Moro Best yenye namba T258 AHV ambalo lilikuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam.
Capture3
Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na SAID S/O LUSOGO liligongana na Lori namba T820CKU / T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma likiendeshwa na GILBERT S/O ISAYA NEMANYA.
Taarifa ya kamanda wa Polisi inasema katika ajali hiyo watu 17 wamepoteza maisha kati yao wanaume ni 12 na wanawake ni 5, Pia watu 56 wamepata majeraha mbalimbali na wamelazwa katika Hospitali za wilaya ya Kongwa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma. Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na dereva wa lori hilo pamoja na utingo wake.
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kutokuwa na tahadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita (overtake) gari jingine na kwenda kuligonga basi hilo

KUTANA NA PICHA ZA MWANAMKE MWENYE KIUNO CHEMBAMBA DUNIANI

CATHIE Jung ana miaka 77 na ndiye mwanamke mwenye kiuno chembamba zaidi Duniani. 
Ni miongoni mwa watu walio kwenye kitabu maarufu cha kumbukumbu za Guinness world Hakika hii inashangaza kimtindo.

ZILIZOSOMWA ZAIDI