NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Friday, November 28, 2014

AKAUNTI YA TEGETA ESCROW YAWA KAA LA MOTO KWA WAZIRI WA NISHATI NAA MADINI PROF SOSPETER MUHONGO, KIKAO CHA BUNGE CHAVUNJIKA USIKU, VURUGU ZATAWALA DODOMA.


Wabunge wa upinzani wakiondoka bungeni Dodoma jana usiku baada ya kikao cha Bunge hilo kuvunjika.
Picha na Emmanuel Herman
**************
Dar/Dodoma.
Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana usiku kilivunjika baada ya vurugu kutawala ukumbini humo.

Vurugu hizo zilianza saa 04:42 usiku hadi saa 04:49 usiku wakati Spika Anne Makinda alipolazimika kuahirisha Bunge hadi leo saa tatu asubuhi.

Chanzo cha vurugu ni kutokana na ugumu wa kutokukubaliana na azimio la tisa, lililolenga kumwajibisha moja kwa moja Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Azimio la PAC lilitaka Waziri Muhongo aadhibiwe kwa kufukuzwa kazi kutokana na tuhuma zilizokuwa zinazomkabili ikiwamo kulidanganya Bunge.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge wengi wakiwa wa CCM walitaka waziri huyo asiadhibiwe na Bunge bali achukuliwe hatua na mamlaka iliyomteua.

Wakati ubishani huo ukiendelea, ikiwa imefika saa 4.42 usiku Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisimama na Spika Makinda alimruhusu kuzungumza.

“Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo (jana) kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi,” ilikuwa ni kauli ya Mbowe.

Mara baada ya kutoa kauli hiyo, wabunge wote wa upinzani walisimama na kuanza kupiga kelele kwamba wezi waondoke…tunataka fedha zirudi…tunataka fedha zirudi…vijana msilale…vijana msilale.

Wakati wabunge hao wakiendelea kuimba, wabunge wa CCM wao walikuwa wakizunguka zunguka huku wengine wakitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge.

Hata hivyo, wabunge wa upinzani waliendelea kusimama, kuimba na kupiga makofi, huku wabunge wa CCM wakimpongeza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kwa kuruka kihunzi alichokuwa amewekewa na kamati ya PAC.

Kutokana na hali hiyo wabunge wengine walisimama vikundi vikundi, huku Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, na Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka walikuwa wakiwasihi wabunge wa upinzani wasiondoke bungeni.

Spika Makinda alisimama na kusema, “Mheshimiwa Mbowe kuondoka mapema ni mambo ya kitoto, semeni mnataka Bunge lifanye nini.”

Hata hivyo, kauli hiyo ya Makinda haikuwafanya wabunge hao kuacha walichokuwa wakikifanya, bali walibaki ndani ya ukumbi wakiwa wamesimama hadi ilipofika Saa 04:49 usiku wakati Spika Makinda aliposimama na kusema, “Waheshimiwa wabunge naahirisha kikao cha bunge hadi pale tutakaposhauriana.”

Kuvunjika kwa kikao hicho kinaweka njia panda hatima ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ambao Bunge lilikuwa halijafikia kufanya maazimio ya hatima yao.

Hoja ya baadhi ya wabunge wa CCM walikuwa wakitaka mapendekezo yaliyotolewa na Mbunge wa Bariadi (CCM), Andrew Chenge kuhusu hatima ya Pinda na Werema yapite.

Chenge alipendekeza kuwa, “Kuhusu suala la Waziri wa Nishati na Madini lifikishwe kwa mamlaka ya uteuzi kwa hatua zaidi (wakimaanisha Rais).”

Pendekezo ambalo lilipingwa na upinzani kwa kile walichoeleza kuwa Bunge linaweza kuwawajibisha kama ambavyo limewahi fanya hivyo. Spika Makinda akijibu hoja ya Bunge kuwawajibisha alisema; “Mnajua waheshimiwa wabunge huko nyuma mawaziri walikubali wenyewe, lakini hawa wamekataa ndiyo maana tunaona haya yanatokea.”

Awali, Bunge hilo limemwachia Rais Jakaya Kikwete kufanya uamuzi wa kuwawajibisha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi baada ya kuadhimia kuwa suala lake lifikishwe kwa Rais kwa hatua zaidi.

Mjadala wa kuchukuliwa hatua kwa Maswi uliwagawa wabunge na kuwafanya kujadili kwa zaidi ya dakika 30, kufikia uamuzi huo ambao hata hivyo ulipingwa na baadhi ya wabunge.

Hata hivyo, Bunge limemwokoa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kwa kuona kuwa kauli yake aliyoitoa haikuwa na madhara yoyote hivyo hahusiki kwa vyovyote vile kwenye sakata hilo.

Hatua ya kuwashughulikia viongozi hao na wengine kuokolewa ilifikiwa baada ya mvutano mkali wa pande mbili ndani ya Bunge katika kukubaliana na mapendekezo ya kamati ya PAC.
Baada ya muda wabunge na mawaziri walioanza kuingia kwenye magari yao na kuondoka bila kujua nini kitaendelea leo.

Hata hivyo, Spika Makinda ambaye alikuwa amezungukwa na askari wa usalama akisindikizwa ofisini kwake alisikika akiwaambia baadhi ya wabunge kuwa kikao kitaendelea leo saa tatu.
Taarifa kutoka kwa baadhi ya maofisa wa Bunge zimeeleza kuwa kikao cha Bunge kitaendelea leo.

Awali, Bunge lilikubali mapendekezo ya PAC kwamba viongozi wa umma waliofaidika na fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wachukuliwe hatua za kinidhamu ya kuvuliwa nyadhifa zao.
Wengine ni Naibu wake Stephen Masele na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi nao wawajibishwe.

PAC ilieleza kuwa wakati Jaji Werema ameonekana kutoishauri vizuri Serikali na pia kuagiza fedha hizo zitolewe kwenye akaunti hiyo, mwenzake Profesa Muhongo hakuchukua hatua wakati akijua kuwapo kwa sakata hilo, huku Naibu wake, Stephen Masele akitiwa hatiani kwa kulidanganya Bunge.

Vilevile, Bunge limependekeza kuwa viongozi wa umma waliopewa fedha zitokanazo na Akaunti ya Tegeta Escrow na hawakutangaza kupokea zawadi kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma nao wachukuliwe hatua akiwamo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Viongozi wengine wanaotajwa kupewa fedha hizo ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na baadhi ya majaji na watumishi wa Serikali.
Chanzo: MWANANCHI

MPASUKO : ESCROW WABUNGE WAGAWANYIKA

Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msangi (katikati) akiwasihi Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (kushoto) na Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy wasigombane kwenye Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana. 
(Picha na Emmanuel Herman)Dodoma. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo jana alipangua hoja zilizotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), kuhusu ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuacha wananchi njia panda kwa kutokuelewa nani anasema ukweli kati yake na kamati hiyo, inayoongozwa na Zitto Kabwe. 
Juzi, kamati hiyo ya Zitto iliwasilisha ripoti yake kuwa imethibitisha kuwa Profesa Muhongo amekuwa mara kwa mara akilipotosha Bunge na Taifa kwa ujumla kwamba ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha za umma. 
Kamati hiyo ilieleza kuwa imebaini kuwa Profesa Muhongo ndiye aliyekuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Singh Sethi na James Rugemalira tena katika ofisi ya umma na pengine hilo ndilo lilikuwa sababu ya upotoshaji. 
Akiwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu hoja hiyo, Profesa Muhongo alianza kupangua hoja moja baada ya nyingine ingawa katika mjadala wa baadaye, zilihojiwa na wachangiaji wengine waliohoji uhalali wa vielelezo alivyotoa. 
Kutaifisha mitambo
Jana, alieleza kuwa pendekezo la Kamati ya PAC kutaka mitambo ya IPTL itaifishwe si sawa kwa kuwa kulingana na mkataba wa PPA kati ya Tanesco na IPTL, majukumu ya IPTL yalikuwa ni kujenga, kumiliki na kuendesha (Build, Own and Operate – BOO). Hivyo, kutaifisha mtambo huo ni kukiuka makubaliano katika mkataba wa PPA wa Mei 26, 1995. 

“Ukiukwaji wa aina hii ukitokea unaweza kuingiza Serikali katika mgogoro mkubwa ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kwenye Mahakama za kibiashara za kimataifa. Aidha, utaifishaji wa miradi ya uwekezaji binafsi itakuwa ni njia ya kufukuza wawekezaji.” 

Gharama za uwekezaji

Kuhusu taarifa ya kamati ya PAC kwamba mwaka 2004 Tanesco ilifungua shauri katika Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro ya Kiuwekezaji (ICSID 2) kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya gharama za uwekezaji, Profesa Muhongo alisema suala hilo si kweli. 

Alifafanua kuwa Tanesco haijawahi kufungua shauri lolote ICSID ya London au Mahakama yoyote dhidi ya Benki ya Standard Charterd kupinga kiasi kikubwa cha Capacity Charge kama inavyoelezwa na PAC. 

“Shauri la ICSID 2 lilifunguliwa Oktoba 31, 2010 na Standard Chatered Bank Hong Kong (SCBHK) kwa ajili ya kudai malipo ya deni ililonunua kutokana na mkopo uliotolewa na mabenki ya ushirika ya Malaysia kwa IPTL. Wahusika katika shauri hilo la ICSID 2 ni SCBHK na Tanesco na wala siyo Tanesco na IPTL.” 

Alisema Februari 12, ICSID ilitoa uamuzi kuhusiana na shauri la SCBHK na Tanesco na kuwashauri wakae kukokotoa upya malipo ya Capacity Charge. Hata hivyo, ilikuwa vigumu kwa pande hizo kutekeleza uamuzi huo kutokana na pande hizo kutokuwa na mkataba wa kibiashara baina yao.

“Vilevile, kupitia shauri la madai Na. 60/2014, lililofunguliwa na IPTL katika Mahakama Kuu ya Tanzania Aprili 4, ilizuia utekelezaji wa maelekezo hayo,” alisema. 


Uwekezaji wa Sh50,000
Profesa Muhongo alisema kuhusu madai ya PAC kuwa mtaji wa uwekezaji katika mtambo wa IPTL ni Sh50,000 na kwamba huo ndiyo ungetumika kukokotoa gharama za uwekezaji ili kulipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa, maelezo hayo siyo sahihi. 

Alisema ukweli ni kwamba kutokana na uamuzi ya ICSID 1 ya Julai 12, 2001, gharama za ujenzi wa mtambo wa Tegeta ni Dola za Marekani 127.2 milioni kama ilivyoelezwa na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). 


Profesa Muhongo alisema katika taarifa hiyo, pia imeelezwa kuwa ilikubalika kuwa uwiano wa deni na mtaji utakuwa 70:30 ikiwa na maana kwamba, deni ni Dola za Marekani 89.04 milioni na mtaji ni Dola za Marekani 38.16 milioni na kwamba uamuzi huo haujabadilishwa na Mahakama yoyote au mtu yeyote. 


“Tunakubaliana kwamba fedha iliyopokewa kutoka mabenki ya ushirika ya Malaysia kama mkopo ni Dola za Marekani 85.86 milioni ambazo kati ya Dola za Marekani 105 milioni zilizokuwa zimeidhinishwa,” alisema na kuongeza:
“Swali la kujiuliza je, mtambo huo ulikamilikaje kwa gharama ya Dola za Marekani 85.86 milioni, huku gharama halisi ya ujenzi wa mtambo wa Tegeta ikawa Dola za Marekani 127.2 milioni? 

Alisema ni dhahiri kwamba kuna matumizi ya zaidi ya Dola za Marekani 38.16 milioni ambazo pia zimetumika kwenye uwekezaji na kwamba Kamati ya PAC haikuonyesha fedha hizo kuwa sehemu ya uwekezaji. 


PAP na umiliki wa hisa saba
Profesa Muhongo alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa za Brela za Desemba 31, 2013, uhamishaji wa hisa saba za Mechmar katika IPTL kwenda PAP ulisajiliwa hapa nchini. Kwa maana hiyo, PAP ni mmiliki wa asilimia 70 za IPTL. Alisema Kamati ya PAC imeeleza kuwa PAP siyo mmiliki halali wa hisa saba za Mechmar katika IPTL lakini kamati imethibitisha kwamba nyaraka za mauziano kati ya Mechmer na Piper Link zilipokewa na Harbinder Singh Sethi ambaye pia ndiye mmiliki wa PAP.
“Kwa uthibitisho huo, kamati inakubali kuwa hisa za Mechmer katika IPTL zinamilikiwa na PAP,” alisema Profesa Muhongo. 

Akana kuwa dalali 

Profesa Muhongo alisema taarifa ya Kamati ya PAC kwamba yeye ndiye aliyekuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Harbinder Sethi na James Rugemalira siyo sahihi kuwa tangu Novemba 9, 2011, Rita iliitisha mkutano na kuwakutanisha wadau wote wa IPTL wakati yeye alikuwa hajateuliwa kwenye wadhifa huo. 

“Mimi kama ni dalali, udalali wangu ni kupeleka umeme vijijini. Mimi kama ni dalali udalali wangu ni kusaidia wachimbaji wadogo wa madini na kupeleka Watanzania kusoma masters (shahada ya pili) duniani kote.” 


Serikali kutokuchukua tahadhari
Waziri alisema Kamati ya PAC, imeeleza kuwa Serikali haikuchukua tahadhari ya kutosha dhidi ya madai mengine yanayoweza kujitokeza kabla ya kutolewa kwa fedha kutoka akaunti ya escrow kitu ambacho alidai si kweli. 

Profesa Muhongo alisema kinga iliyochukuliwa inakidhi matakwa ya kisheria na imezingatia athari yoyote ambayo ingeweza kutokea baadaye kutokana na kutolewa kwa fedha katika akaunti ya escrow.
“Kwa hiyo, siyo kweli kwamba Serikali haikuchukua tahadhari kama ilivyodaiwa na PAC.” 

Madai ya Sh321 bilioni
Profesa Muhongo alisema hoja ya PAC kwamba imejiridhisha kuwa madai ya Tanesco ya Sh321 bilioni yana uhalali japo usahihi wake utapatikana baada ya kutekelezwa kwa uamuzi wa ICSID 2 na Tanesco na IPTL kukubaliana kiwango sahihi cha Capacity Charge haina nguvu. 

“Madai ya kwamba Tanesco inaidai IPTL Sh321 bilioni msingi wake ni dhana kwamba mtaji wa IPTL ni Dola za Marekani 100, sawa na Sh50,000 kwa wakati huo. Dhana hii ilipuuza ukweli kwamba Dola za Marekani 38.16 milioni ziliwekezwa kwenye mradi wa Tegeta,” alisema. 


Profesa Muhongo alisema Bodi ya Tanesco imekana kuyatambua madai hayo ya Sh321 bilioni... “Kimsingi hata vitabu vya hesabu vya Tanesco ambavyo vimekuwa vikikaguliwa na CAG, havionyeshi kuwapo kwa deni hilo.”

RAIS KIKWETE AMTUMIA MKUU WA MKOA WA TANGA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Jakaya-Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Rajabu Rutengwe kuomboleza vifo vya watu 11 ambapo wengine kadhaa walijeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea tarehe 27 Novemba, 2014.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Mkanyageni Mkoani Tanga baada ya basi dogo aina ya Toyota Coaster Na. T 410 BJD iliyokuwa ikitoka Tanga Mjini kuelekea Lushoto kugongana na Lori aina ya Scania Na. T 605 ABJO.
 “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kupotea ghafla kwa maisha ya watu 11 na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea katika Mkoa wako wa Tanga”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake na kuongeza:
 “Naomba upokee salamu zangu za rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kutokana na vifo hivyo, na kupitia kwako, naomba salamu za pole ziwafikie watu wote waliopotelewa na ndugu na jamaa zao kwenye ajali hiyo”.

Rais Kikwete amesema anawaomba wote waliopoteza ndugu na jamaa zao kwenye ajali hiyo wawe watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, na amewahakikishia kuwa yuko pamoja nao katika kipindi chote cha maombolezo.
“Kwa wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo, namwomba Mungu awajalie ahueni na wapone haraka, ili warejee tena katika hali zao za kawaida. Namwomba Mola azipokee na kuzilaza mahala pema peponi Roho za Marehemu wote, Amina”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika Salamu zake.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
27 Novemba, 2014

MAGAZETI YA LEO IJUMAA 28/11/2014























HATIMAYE LADY JAY DEE AKIRI KUMUACHA MUMEWE GADNER HABASH - MSIKILIZE HAPA *AUDIO*

Hatimaye Lady Jaydee amethibitisha kwa kauli yake mwenyewe kuwa ndoa yake na mtangazaji mkongwe wa redio, Gadner G Habash imevunjika.
Akiongea leo kwenye Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha Times FM, Jaydee amesema ni yeye ndiye aliyeamuacha Gadner.
Kwenye mahojiano hayo, Jide alizungumzia kuwa kwenye uhusiano na mtu aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gadner lakini alisema alikuwa akiteswa.
Kabla ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa siku zote amekuwa akiepuka kuongea masuala yake binafsi kwenye vyombo vya habari.“Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu ambaye huwa napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye media, kwenye magazeti au wapi,” alisema. “Na ndio maana lolote ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye maisha yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu wanaongea chochote wanachohisi, chochote wanachotaka kusema. Ninavyofikiria mtu anayenipenda mimi alinijua sababu ya muziki na waendelee kuliheshimu hilo, kwasababu kila mtu ana haki ya kuwa na privacy.
Ingekuwa kila mmoja angekuwa anatoka kwake anaanza kuelezea mambo yake, mama yake jana walishinda njaa, au mume wake alimfanya hivi, sidhani kama kuna mtu yeyote anapenda kuelezea maisha yake, hata matatizo yake mbele za watu.”
“Kwahiyo mpenzi wako Gadner bado mko naye,” aliuliza mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho na mchekeshaji, MC Pilipili.
“Swali nafikiri hujalijibu, umemtosa, hujamtosa?,” aliuliza Fadhil Haule, mtangazaji mwingine wa show hiyo.
“Nimemuacha,” alijibu Jide. “Huyu (Gadner) tumeshamalizana.”
Isikilize interview hiyo hapo chini.

SHEIKH PONDA ASHINDA RUFAA YAKE *PICHAZ*

  Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo huku wakipaza sauti baada Sheikh Ponda kushinda rufaa ya kupinga hukumu ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, Mei 9, 2013. (Picha na Francis Dande)
 Wafuasi wa Sheikh Ponda.
 Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakitoka Mahakamani.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (wa pili kushoto) akitoka katika chumba cha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza wakati  akitoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam. 
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
  Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.
Mfuasi wa  Sheikha Ponda akitoka Mahakamani.

 Ulinzi ukiwa umeimarishwa nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam wakati wa kesi ya Ponda.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakiwa wamelizunguka basi la Magereza alilokuwa amepanda Sheikh Ponda wakati akielekea mahabusu ya gereza la Keko.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakilifukuza basi la Magereza alilokuwa amepanda Sheikh Ponda wakati akielekea mahabusu ya gereza la Keko.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakitoka Mahakamani.
 Gari la Polisi.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti.

MAJANGA: MABOMU YARINDIMA NIGERIA, WATU 25 WAFARIKI WAKIWAMO ASKARI!

TAHARUKI ya mabomuWatu wapatao ishirini na watano wamekufa kufuatia shambulio la bomu katika jimbo la Adamawa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.Imetaarifiwa kwamba wote waliouawa katika shambulio hilo ni raia na askari watano.
Tukio hilo limetokea karibu na mji wa Mubi ambao mwezi huu ulikuwa ukishikiliwa na vikosi vya serikali ya nchi hiyo baada ya kuukomboa kutoka katika himaya ya wanamgambo wa kikundi cha kiislam cha Boko Haram.
Kuna matukio kadhaa ya mashambulizi yanayofanywa na kundi la Boko Haram katika siku za hivi karibuni ikiwemo na matukio mawili ya kujitoa muhanga kaskazini Mashariki mwa mji wa Maiduguri, shambulio ambalo liligharimu uhai wa watu nane.

MCHEZAJI WA CRICKET TOKA AUSTRALIA PHILLIP HUGHES AFARIKI DUNIA..! SOMA CHANZO!

MCHEZAJI wa cricket kutoka australia Phillip Hughes afariki duniana baada ya kupigwa shingoni na mpira  wa mchezo huo na kusabibishwa kutokwa na damu nyingi kichwani ilio sababisha kifo chake.
Hughes alikua akijiandaa kupiga mpira uliorushwa na timu pinzani kati ya mechi ya South Wales na South Australia siku ya jumanne baada ya mpira huo kumpiga upande wa kushoto wa shingo yake.
Phillip mwenye umbri wa miaka 25 anaechezea timu ya South Astralia  baada ya kupigwa na mpira huo alibaki  akisimama kwa mda mchache na baadaye alianguka chini na  kuzimia ambapo mapema jana alifariki dunia.
Daktari wa timu ya South Australia  Peter Brukner alieleza kua kupigwa kwake na mpira wa shingo na kutokwa na damu  nyingi kichwani ni tatizo la kushangaza maana ni nadra sana kutokea na kusababisha kifo cha mtu.
Kuna kesi 100 zilizowai kuripotiwa juu ya mchezo huu lakini hii ambayo ni adimu kutokea ni mara ya kwanza kuripotiwa.

FAHAMU JINSI WATANZANIA WANAVYOUMIZWA NA UFANYAJI MAPENZI KWA NJIA MDOMO

MKURUGENZI wa Idara ya Kinga kutoka taasisi ya Saratani Ocean road Julius Shija amewataka watanzania waache tabia ya kuiga mambo yasiyo ya msingi kama kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo tendo ambalo amelitaja kuwa linaweza kusababisha kansa ya koo.
Shija alisema kwamba hali katika kipindi cha hivi karibuni imebadilika kulinganisha na kipindi cha miaka ya tisini ambapo walikuwa wanapokea wagonjwa 200 hadi 300 tofauti na kipindi cha sasa ambacho wanapokea wagonjwa 500 hadi 600 ambao wanagundulika kuathiriwa na kansa iliyosababishwa na ufanyaji mapenzi kwa kuhusisha midomo.
"Watanzania wasipende kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya mapenzi kwa kuhusisha mdomo,  saratani ya mdomo ipo na nyingine zinasababishwa na zinaa," alisema Shija.
Aliongeza kuwa wanapokea wagonjwa wapya kila siku kwenye taasisi hiyo wagonjwa waliopata saratani hiyo mdomoni na kwenye njia ya juu ya hewa baada ya kujamiiana kwa njia ya mdomo.
"Kufanya mapenzi na kuhusisha mdomo kunaleta saratani kupitia mdomo na sehemu ya juu ya hewa, virusi hivi vikifika kwenye sehemu ya juu ya hewa na mdomoni na vikakuta kuna mchubuko au uwazi wowote vitaingia kwenye hizi chembechembe za fizi kwenye ulimi na kwenye njia ya juu yahewa, vitapenya ndani na kuharibu zile chembechembe na zitaanza kukua na kusababisha saratani," alieleza Shija.

MBUNGE WA KIGOMA DAVID KAFULILA AAGA UKAPERA NA KUOA, MBUNGE WA NJOMBE DEO FILIKUNJOMBE AWA MPAMBE *PICHAZ*

MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), ameaga ukapera baada ya kufunga ndoa na Jessica Kishoa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Uvinza, huku akisindikizwa na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), aliyekuwa mpambe.
Akizungumza katika harusi hiyo jana, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto alimpongeza Kafulila kwa kukamilisha ndoa yake na mwenza wake na kumuomba mke wa Kafulila, kuwa mvumilivu katika kipindi hiki kwani hawatakuwa na fungate na mume wake hadi watakapomaliza kushughulikia suala la Escrow lililoko mbele yao.
Naye Filikunjombe alimpongeza Kafulila kwa kukamilisha mchakato wa ndoa yake, licha ya kuwa katika kipindi kigumu cha kupigania maslahi ya Watanzania.
Naye Kafulila alishukuru watu wote waliojitoa kwa hali na mali kuhakikisha harusi yake inafanikiwa, lakini alisema kuwa analo jukumu kubwa katika kuhakikisha tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma kupitia akaunti ya Escrow, linafikia mwisho na kila mmoja anavuna alichopanda.
Harusi hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (Chadema) ambaye alisema kuwa Kafulila ni kaka yake na wametoka mbali kisiasa na kwamba anamuunga mkono katika ajenda wanayoisimamia kwa maslahi ya Watanzania.
Jessica Kishoa akimvisha pete ya ndoa Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila katika ibada ya ndoa Kanisa Katoliki Parokia ya Uvinza mkoani Kigoma.
Chanzo: Habari Leo

ZILIZOSOMWA ZAIDI