Friday, November 28, 2014

MBUNGE WA KIGOMA DAVID KAFULILA AAGA UKAPERA NA KUOA, MBUNGE WA NJOMBE DEO FILIKUNJOMBE AWA MPAMBE *PICHAZ*

MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), ameaga ukapera baada ya kufunga ndoa na Jessica Kishoa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Uvinza, huku akisindikizwa na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), aliyekuwa mpambe.
Akizungumza katika harusi hiyo jana, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto alimpongeza Kafulila kwa kukamilisha ndoa yake na mwenza wake na kumuomba mke wa Kafulila, kuwa mvumilivu katika kipindi hiki kwani hawatakuwa na fungate na mume wake hadi watakapomaliza kushughulikia suala la Escrow lililoko mbele yao.
Naye Filikunjombe alimpongeza Kafulila kwa kukamilisha mchakato wa ndoa yake, licha ya kuwa katika kipindi kigumu cha kupigania maslahi ya Watanzania.
Naye Kafulila alishukuru watu wote waliojitoa kwa hali na mali kuhakikisha harusi yake inafanikiwa, lakini alisema kuwa analo jukumu kubwa katika kuhakikisha tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma kupitia akaunti ya Escrow, linafikia mwisho na kila mmoja anavuna alichopanda.
Harusi hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (Chadema) ambaye alisema kuwa Kafulila ni kaka yake na wametoka mbali kisiasa na kwamba anamuunga mkono katika ajenda wanayoisimamia kwa maslahi ya Watanzania.
Jessica Kishoa akimvisha pete ya ndoa Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila katika ibada ya ndoa Kanisa Katoliki Parokia ya Uvinza mkoani Kigoma.
Chanzo: Habari Leo

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI