NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Tuesday, June 28, 2016

ANGALIA PRE SEND OFF YA VERONICA MAPUNDA MFANYAKAZI WA TV1 TANZANIA *VIDEO HD*

NDOA ni jambo lá Kheri na wawili wakutanapo na kupendana kwa dhati basi jambo hili kamwe huwa haliepukiki, kwa kuzitambua baraka zilizomo Kwenye ndoa Bw. Lameck Silas Makweta wa Makambako na Bi. Veronica Angelus Mapunda wa Dodoma ambao ni wafanyakazi wa TV Tanzania wameamua kuungana na kuwa mwili mmoja, hapa Kwenye link hii ya blue ni moja ya video kuhusiana na jinsi wawili Hawa walivyokutana na kuamua kufunga ndoa. Enjoy!!!

Ni Part 1 ya PRE SEND OFF VIDEO IHUSUYO MAISHA YA BI. VERONICA MAPUNDA na Bw. LAMECK SILAS ambapo wawili hawa wanatarajia kufunga ndoa mnamo tarehe 2 mwezi Julai 2016 katika kanisa Katoriki Makambako, Njombe.
https://youtu.be/3p-dV8ekLj4

Its a documentary of Ms. Veronica Mapunda from Dodoma Tz who weds Mr. Lameck Silas Makweta of Makambako Tz on 2nd July 2016, as appreciation to these beautiful couples Samfrod Media did a documentary that talks about their lives as lovers who started slowly when they met at TV1 Tanzania company on 2013.
We wish them nothing but endless happiness in their eternal love life.

Thursday, June 23, 2016

NYOTA YA VANESSA MDEE YAZIDI KUNG'AA KIMATAIFA..ATAJWA KUWANIA TUZO NIGERIA

Msanii wa Bongofleva Vanessa Mdee jina lake limeingia kwenye headlines baada ya kutajwa katika moja kati ya tuzo kubwa Nigeria Entertainment, Vanessa ametajwa kuwania tuzo zinazoitwa Nigeria Entertainment Awards.
Jina la muimbaji Vanessa Mdee limetajwa katika kipengele cha kuwania tuzo ya muimbaji bora wa kike, katika kipengele hicho Vanessa anawania tuzo hiyo na wasanii wengine saba kutoka nchi mbalimbali, Nigeria Entertainment Awards zitafanyika New York Marekani, September 4 2016

UGONJWA ULIOZUIA MAHAFALI YA CHADEMA WAJULIKANA

Serikali imesema uchunguzi wa awali wa vifo vya watu wanane mkoani Dodoma umeonyesha kuwa vilitokana na familia kula ugali wa unga wa mahindi wenye sumu kuvu B (aflatoxins B).

Jeshi la Polisi lilizuia mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani Dodoma ambao ni wafuasi wa Chadema yaliyokuwa yafanyike kwenye hoteli ya African Dream, likisema mikusanyiko yote imezuiwa baada ya kuzuka ugonjwa usiojulikana ambao awali uliua watu sita.

Wakati Jeshi la Polisi likizuia mahafali hayo ya Chadema, taasisi nyingine zilikuwa zikiendelea na mikutano kwenye hoteli hiyo, jambo lililowafanya viongozi wa Chadema kulalamikia hafla yao kusambaratishwa na polisi waliokuwa na silaha za moto na gari la maji ya washawasha.

Mbali na kuongezeka kwa idadi ya waliofariki dunia, watu waliougua ugonjwa huo wameongezeka kutoka 21 hadi 28.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Khamis Kigwangalla alisema pamoja na matokeo hayo ya awali, watalaamu wengine wa afya walienda wilaya za Chemba na Kondoa kuchukua sampuli nyingine.

Alisema wataalamu hao wanatoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Alisema sumu kuvu inatokana na fangasi wanaokuwa katika mazao ya nafaka au mahali ambapo mazao hayo yamehifadhiwa.

Hata hivyo, alisema athari za sumu kuvu hizo ni za muda mrefu na inamuweka mtu katika hatari ya kupata saratani ya ini.

Dk Kigwangalah alisema uchunguzi huo umethibitisha kuwa ugonjwa huo si Homa ya Bonde la Ufa wala manjano, ingawa baadhi ya dalili zinafanana.


Jumapili iliyopita Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, alisema wamechukua hatua mbalimbali ikiwamo kuchukua sampuli za maabara kwa ajili ya utambuzi wa ugonjwa na damu, mkojo, kinyesi, matapishi na vinyama vinavyotokana na ini vimechukuliwa. “Sampuli zote zimepelekwa Maabara ya Taifa, Mkemia Mkuu wa Serikali na Maabara ya Kilimanjaro Christian Research Institute (KCRI) iliyopo Kilimanjaro kwa uchunguzi zaidi,” alisema.

''MAVOKO: NITAKIPIGA BRUSH KIMOMBO CHANGU, SITAKI KUUMBUKA KAMA ILIVYONITOKEA LONDON''

Kiingereza ni lugha inayotupa tabu Watanzania wengi na hakuna anayebisha kuwa kimekuwa kikitukosesha fursa nyingi za kimataifa au kujikuta tukiumbuka.
Rich Mavoko ni mmoja wao na amesema atalazimika kufuata njia ya bosi wake, Diamond ili kujinoa zaidi kuepuka kuumbuka siku za usoni.

“Mwaka jana nilienda London, nikakutana na mtu anaongea Kiingereza pale pale lakini mbona kuna vitu sivielewi anavyoongea, alikuwa ni mhindi ambaye amezaliwa kule kule. Anaweza kuuliza maswali mengi ukaelewa matatu,”
“Kizuri ambacho mimi nakijua usilete mbwembwe jibu unachokielewa kwa time aliyokuuliza, kwahiyo kuna umuhimu sana kwasababu hatuwezi kufika bila kujua hicho kitu,” ameongeza.

Rich Mavoko ana elimu ya kidato cha nne na amedai kuwa alishindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu za kiuchumi.

Diamond naye amewahi kusimulia jinsi alivyowahi kuumbuka miaka kadhaa iliyopita wakati Kiingereza chake kilikuwa cha kuchechemea hali iliyomfanya apate hasira ya kujifunza. Leo hii hitmaker huyo anakipiga kimombo kama kawaida!

MHARIRI MKUU WA GAZETI LA DIRA ASIMAMISHWA KAZI

Mkurugenzi Mkuu wa gazeti la Dira Alex Msama, amemsimamisha kazi aliyekuwa Mhariri wa Habari wa Gazeti  hilo la Dira ya Mtanzania Mussa Mukama kutokana na mapungufu ya kiutendaji kwa kuonesha dhahiri kutomudu nafasi hiyo.
Msama pia amemuomba radhi Waziri wa Sheria na katiba, Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa kwenye lake, mbele ya waandishi wa habari Msama amekubali kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani‘ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.
Hivi karibuni Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo zilizochapishwa na Gazeti la Dira  ya Mtanzania la June 20 na la June 23 mwaka huu zililenga kumchafua na kuahidi kulishtaki gazeti hilo kupitia habari hizo mbili.

ZILIZOSOMWA ZAIDI