NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Monday, May 25, 2015

AINA 10 ZA WANAWAKE WANAOPENDWA NA SANA NA WANAUME

WAPENDA USAWAAina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi niwanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu yakifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamiikwa asilimia 50 kwa 50
WANAOJUA MAPENZIWanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa niuwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwasita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaumebila kujali sifa zao za nje au za ndani 
MARAFIKI Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume.Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida naraha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani 
WAPENDA UWAZI Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo nawapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwakisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hiiwamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katikauelewa wa mambo. 
WANAOJITEGEMEA Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina‘naomba vocha’ kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leohawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza stareheza upande mmoja. 


WASIO NA PRESHANikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vituvitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe nakazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi

MARIDADI Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafina kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini pia ni waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano. 

WANAORIDHIKA Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwawanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzikwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutokajuu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke 

WA MMOJA Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kilaaina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziadazaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana.“Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.”Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
#DODOMA CLAN

SENTENSI TISA ZA NAPE NNAUYE KUHUSU ISHU YA MWIGULU NCHEMBA KUOMBA KUPUMZIKA NAFASI YAKE CCM!!

nnauye-607x360
Naibu Waziri wa Fedha, Lameck Mwigulu Nchemba jana jina lake liliingia kwenye headlines baada ya kutangaza kujivua kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara.. hiyo ishu ilichukua nafasi kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii kuanzia siku ya jana May 24 2015, leo anayeingia kwenye headlines ni Nape Nnauye, Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM amezungumzia kuhusu ishu ya Mwigulu Nchemba alivyojitoa kwenye nafasi yake hiyo ndani ya Chama.
>> “Tumejadili  mambo mengi nikaona hili moja nilitoe mengine tutaendelea kupeana”>>> Nape Nnauye.
>>> “Mwishoni mwa kikao Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara ndugu Lameck Mwigulu Nchemba ameomba kwa Halmashauri kuu ya Taifa kupumzika kwa sababu ya nia yake ya kuomba kuteuliwa na CCM kuwa mgombea wa nafasi ya Urais”>>> Nape Nnauye.
>>> “Ametumia busara na wajumbe wameridhika, wamepongeza busara yake”>>>
>>> “Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa akamteua Rajabu Luhavi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Halmashauri Kuu ikampitisha kuwa Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Tanzania bara.. amekuwa msaidizi wa Rais Ikulu mambo ya siasa sasa anahamia kwenye chama”>> Nape Nnauye.
Kama unataka kuisikiliza sauti ya Nape Nnauye unaweza kuplay hapa umsikie akimzungumzia Mwigulu Nchemba.

ORODHA MPYA YA WANAMUZIKI MATAJIRI AFRIKA! JE, DIAMOND PLATINUMZ KAINGIA?! TAZAMA HAPA!!! *PICHAZ*

Diamond Platinumz, msanii inayesemekana ndiye mwenye pesa nyingi zaidi Tanzania kwa sasa lakini vipi kwa Afrika kaingia katika top 10?! Tazama list hiyo kamili hapa chini... Africa is blessed with beautiful landmarks and unique geographical composition apart from that Africa is blessed with
lots of talents from athletes to artists range from upcoming to legends,As presented by Capital Fm from Kenya below is the list of 10 most rich music artists from Africa.
1.Youssou N'dour- Senegal 
Youssou N'dour 

2.P.square-Nigeria 

P.square 

3.D'banj-Nigeria 
D'banj 
4.Koffi Olomide-DRC 
Koffi Olomide 
5.Salif Keita-Mali 
Salif Keita 
6.Fally Ipupa-DRC 
Fally Ipupa 
7.2face Idibia-Nigeria 
2face Idibia 
8.Hugh Maskela-South Africa 
Hugh Maskela 
9.Banky W.-Nigeria 
Banky W 
10.Jose Chameleon-Uganda 
Jose Chameleon

UPUUZI ULIOFANYWA NA MSANII SHILOLE UBELGIJI, BARAZA LA SANAA TAIFA LAMTOLEA UVIVU KUKOMESHA TABIA ZA WASANII KUONYESHA UTUPU JUKWAANI

Na Elizabeth Edward


Niwapongeze Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kuonyesha wazi kusimama kidete kulinda utamaduni wa Mtanzania na sanaa kwa ujumla. 

Nikiwa kama mdau wa burudani kwa muda mrefu, nimekuwa nikishuhudia vitu vya ajabu kwenye sanaa ambavyo vinaonekana wazi kwenda kinyume na utamaduni wetu. 

Uamuzi wa hivi karibuni wa Basata kuvunja ukimya kuhusiana na kuzagaa kwa picha za kudhalilisha za msanii Shilole umeibua matumaini mapya kwa Watanzania wengi ambao walianza kuhisi kuwa chombo hicho hakifanyi kazi yake ipasavyo. 

Katika hali ya kawaida ilikuwa lazima kauli itolewe kuhusiana na picha hizo ambazo licha ya kumdhalilisha Shilole zimedhalilisha utu wa mwanamke. 

Mbaya zaidi zimekwenda mbali na kuwadhalilisha wasanii wa Tanzania na taifa kwa ujumla kwani zilipigwa akiwa stejini nchini Ubelgji. 
Kumradhi kwa muonekano wa picha za msanii Shilole, zinazomdhalilisha msanii huyo na wanawake kiujumla ambapo wasanii wa kike wamekuwa na tabia ya kuviweka viungo vyao vya siri hadharani.

Mithili ya upepo, picha hizo zilisambaa kwa muda mfupi kwenye mitandao ya kijamii na kuwafikia Watanzani ambao wengi wao walionyesha kukerwa. 

Basata kama chombo kinachoangalia mwenendo wa sanaa na wasanii nacho kimeonyesha kusikitishwa na picha hizo hata kufikia uamuzi wa kumtaka aeleze sababu za kufanya udhalilishaji huo. 

Kwa mujibu wa Basata, ilishawahi kumuita na kumuonya msanii huyo kutokana na tabia yake ya kutokujiheshimu awapo jukwaani na kuahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo chafu. 

Hata hivyo, kuendelea kwake kufanya matukio hayo na kwa sasa katika ardhi ya nchi nyingine ni uthibitisho kwamba hajabadilika. 

Kutobadilika huko kunamfanya aonekane kwamba ameendelea kuidhalilisha sanaa na wasanii wa Kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi hiyo. 

Nashindwa kuelewa tunaelekea wapi maana taratibu wasanii wa Tanzania wanaonekana kuachana na maadili yao na kuiga tamaduni za magharibi. 

Hili limeonekana sana kwa sababu siku hizi dunia imekuwa kama kijiji ni rahisi kujua kinachoendelea mahali popote tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Inawezekana Shilole ndiye amekumbwa na fedheha hii ya kuonekana lakini hii ni tabia ya wasanii wengi wa kike ambao hujifanya wamechanganyikiwa wapandapo jukwaani. 

Mara nyingi huwa najiuliza hivi muziki hauwezi kuchezeka au kunoga mpaka ukae nusu utupu au uonyeshe maumbile yako. 

Hatukatazwi kuiga vitu kutoka ughaibuni lakini ni vyema tukawa tunachuja na kuangalia tunavyoviiga vinaweza kuwa na madhara gani. 

Inawezekana wasanii wa Tanzania bado hawajajitambua kuwa wao ni kioo cha jamii, watoto wanawaangalia na kujifunza vitu vingi kutoka kwao. 

Jamani wakati mwingine tunapaswa kuweka kando umaarufu na kuangalia utu na maadili maana ndiyo nyenzo pekee zitakazokufanya uheshimike. 

Kila kukicha tunajiuliza kwa nini wasanii wa kike hawafiki mbali tunahangaika kumtafuta mchawi lakini tunasahau kuwa hali hiyo tunaisababisha sisi wenyewe. 

Unafikiri ni watu wangapi wanaweza kuvumilia tabia hizi taratibu unajikuta unapoteza mashabiki hivyo soko la kazi zako litaporomoka. 

Binafsi siamini kama utupu wa msanii unaweza kuwa chachu ya kuwavutia mashabiki wakapenda au kufurahia kazi zako. 

Sitaki kuamini kama usanii au umaarufu wenu unawafanya mjione kuwa siyo wanajamii hata muishi kana kwamba mpo sehemu ambayo hakuna anayewaangalia.

BAADA YA KUMPONDA DIAMOND THE PLATNUMZ DESIGNER MKUBWA WA MAREKANI ABADILI MANENO YAKE NA KUMKUBALI DIAMOND THE PLATNUMZ

Mbunifu wa mavazi toka Marekani anaeitwa Roper amelalamika sana kupitia Instagram kwamba Diamond kamuibia design yake...
Raper anayewavalisha wasanii wakubwa Marekani kama August Alsina, Future, Meek Mill nk ameandika hivi.

MSANII WA MUZIKI WA INJILI FROLA MBASHA AKIMBILIA CHADEMA!!! *PICHA*


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhElQ51ZK5AdH_abrBsM2SgmZkwR9RmsufJAlV-U9GDER9kYp7D9PHXqVgsh7v4-vMjFU1NIByTGlijjfdfiMnY_du4EcR6486UyO-y_Q_Yy8842iHnatDDHHq3aYKc1IUohWNxSBUubS5z/s1600/DSCN8831.JPG 
Msanii wa muziki wa Injili Frola mbasha.

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio.

” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee.

Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti.

Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata habari.

” Siku Serikali ikiwasilisha Muswada wa Vyombo vya Habari,mimi na wabunge wangu tutafanya vurugu hadi unaondolewa bungeni,” alisema Mbowe.

Naye Naibu Katibu Mkuu- Bara, John Mnyika alisema Jiji la Dar es Salaam lina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko licha ya kuwepo kwa wizi mkubwa kura wakati wa uchaguzi.

” Idadi kubwa ya wasanii nchini wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM Vila ya kupata mafanikio ya aina yoyote, hivyo basi Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee.

Sunday, May 24, 2015

DROGBA KUONDOKA CHELSEA

Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba anaihama klabu hiyo kwa mara ya pili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alisajiliwa na klabu hiyo mwaka 2004 na amefunga mabao 164 katika mechi 381.
Ningependa kucheza tena kwa msimu mmoja zaidi na kwa hilo kufanikiwa itabidi nihamie kilabu nyengine aliuambia mtandao wa Chelsea.
Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho alimsajili kwa mara ya pili Drogba kwa kandarasi ya mwaka mmoja baada ya kuondoka Galatasaray.

ALICHOKIFANYA DIAMOND PLATNUMZ MWANZA NI SHIIIIIIIDAH!!!!! *VIDEO*


RAIS JAKAYA KIKWETE AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR,SEIF SHARIFF HAMAD AMBAYE PIA NI KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) KATIKA IKULU NDOGO, DODOMA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jana, Jumamosi, Mei 23, 2015 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Seif Shariff Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Ikulu Ndogo, Dodoma.Picha Juu Rais Kikwete akimwaga Mheshimiwa Hamad baada ya kumalizika kwa kikao hicho.Picha na Freddy Maro-IKULU

WASHUHUDIE MBOWE, GWAJIMA, PROFESA J, FLORA MBASHA NA CHADEMA WALIVYOITIKISA TANZANIA LEO *PICHAZ*

Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo chadema mh FREMAN MBOWE akizindua kikosi maalimu cha ulinzi katika jimbo la kawe maarufu kama RED BRIGDED ambao wamekuwa na kazi ya kulinda usalama wa viongozi wa chama chao.
****
Mwenyekiti wa chama cha chadema FREMAN MBOWE amesema kuwa endapo sheria ya kuvitaka vyombo vyote vya habari Tanzania kuonyesha Taarifa ya Habari moja kutoka shirika la utangazaji TBC itafikishwa bungeni basi bunge hilo halitamalizika na badala yake wataamua kufanya fujo za maksudi kwani sheria hiyo ni sheria ya kuuwa kabisa uhuru wa mtanzania kupata habari.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa kawe waliojitokeza katika mkutano wa hadhara muda huu Jijini Dar es salaam Amesema kuwa kuna sheria ambayo chama cha mapinduzi kimejipanga kuifikisha katika bunge ambayo inazitaka stesheni zote za tv na redio kujiunga na TBC kwa ajili ya kupata taarifa ya habari,sheria ambayo amesema kuwa ni muendelezo wa kuwabana watanzania baada ya ile sheria ya mtandao kupitishwa kinyemela.
Swala la BVR

Mwenyekiti huyo amesema kuwa anamtaka mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi kuongeza siiku za kuandikishwa daftari hilo kwani siku saba zilizowekwa katika kujiandikisha hazitoshi na ni mpango wa kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanakosa fursa ya kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka wenyewe.
Mbowe ameongeza kuwa hakuna ubishi kuwa serikali ya chama cha mapinduzi imechoka na ni lazima mwenzi wa kumi wafanye maamuzi ya kuiondoa madarakani kwa lengo la kupata serikali nyingine ambayo inaweza kusikiliza shida zao


Picha zikimuonyesha mwenyekiti mbowe akizindua kitabu maalum cha HALIMA MDEE ambacho kinaelezea mafanikio ya mbunge huyo katika jimbo lake
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili flora mbasha akitumbuiza pamoja na waceza shoo wake
FLORA MBASHA akitumbuiza nyimbo yake mpya aliyotunga kwa ajili ya kumpongeza mbunge halima mdee kwa kazi kubwa aliyofanya.


Askofu gwajima akiwasili katika viwanja hivyo


Viongozi wa kikosi cha ulinzi kawe wakitoa heshima kwa kamanda mbowe kabla ya kukagua gwaride hilo
Msanii profesa J akiwasha moto kwenye jukwaa ambapo aliwarusha mashabiki wake kwa nyimbo mbalimbali za muziki wa kizazi kipya


Wingi wa wananchi waliojitokeza katika mkutano hu

ZILIZOSOMWA ZAIDI