NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Wednesday, December 31, 2014

ALI KIBA AFUNGUKA: AWATUPIA LAWAMA MASHABIKI KWA UBOVU WA VIDEO YAKE *VIDEO*

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQDukfrTzXLjMmJHlFUqzd46ggt0qjl1mXHradPpf5KCoa2-rx2-_2FsEToVh-crOe1VhR_P-1fMBw-I1NjWjUy0DBjhaLDP3wB_j8JXKIjXL0PID9qGKTSWPAqi9lniXKCf_AbKgd9J4/s640/alikiba1.jpg 
Hatimaye Alikiba ameamua kuwajibu baadhi ya wapenzi wa muziki walioikosoa video ya wimbo wa ‘Mwana’ wanaodai kuwa haiendani na kile kinachoimbwa.
Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds FM, Alikiba amesema alichokifanya alimaanisha hivyo kuleta picha mpya kwenye vichwa vya watu.
“Utofauti wa video ndio uzuri wake kwa sababu kila mtu kwenye mind yake amejenga video, ame-create video itakuwa vipi,” amesema. Kwa sababu nyimbo imeelezea vitu vingi ni pana kama unavyoona na ina vitu vingi madawa, ma-prostitute, ukabaji, wizi, vitu fulani vingi sana nisingeweza vyote kuweka katika video kwa sababu kila mtu anamind yake. Kwahiyo nilivyofanya utofauti nili-concetrate kwenye dancing na kucheza na feeling za kuimba. Video nyingi zimeshafanyika duniani sio ya kwangu tu, kwahiyo watu wasishangae vitendo havikuwepo nimemaanisha sio nimefanya ili tu nitoe video.”
“Ule utofauti uliokuwepo ndo uzuri wa video yenyewe. Professionals walifanya hiyo video kwa sababu ni production kubwa iko na watu ambao wali script vile vile kwahiyo tulishauriana na tuka appreciate kufanya hicho kitu. Dancing style inaitwa Kalila. Choreographer wangu ndio alifanya hiyo yote kila kitu.”

SAMFROD MEDIA WISHES YOU, HAPPY NEW YEAR *VIDEO*

SAMFROD Media ambao ndio wamiliki wa mtandao huu wanakutakia kheri na baraka katika mwaka huu wa 2015.
Tafadhali endelea kuwa nasi na kutumia huduma zetu.
HAPPY NEW YEAR TANZANIANS!

IFAHAMU NYUMBA YA KIFAHARI ANAYOIMILIKI MSANII LADY JAY DEE, HUMO NDANI NI SHIDAAAAH.. *PICHAZ*

LADY jay dee ni msanii mkongwe sana na mwenye maendeleo makubwa pia ameweza kulinda heshima yake tangu kipindi anaanza mpaka hii leo,
muziki umeweza kumpatia mafanikio makubwa ikiwemo kupata tuzo kibao kimataifa na kimataifa,
mbali na hilo pia jay dee anamiliki band inayoitwa machozi bendi, naa pia mgahawa wa kisasa unaoitwa nyumbani lounge, hii leo tunkuletea exclusive picha ya nyumba ya kifahari anakokaa mwanadada huyo,
Picha zote ziko hapa shuka nazo…..



KUMBE T.B JOSHUA ALITABIRI KUPOTEA KWA NDEGE YA AIRASIA QZ8501 YA INDONESIA... USHAHIDI WA VIDEO HUU HAPA!


NABII T.B. Joshua mapema leo kupitia YouTube channel yake inayojulikana kwa jina la Emmanuel TV ametoa video akionyesha utabiri wake kuhusu kupotea kwa ndege ya indonesia  AirAsia  8501 kwenye Video hiyo haya ni baadhi ya maneno yake na nukuu 


"I have a message for the nation, Indonesia,” Joshua is seen telling congregants in the video. “When it comes to this disaster issue, I don’t want to mention it,”

“It looks so nasty to me to mention - a situation where it will cost a lot of lives, suddenly,” he went on. “This is a crash. Why should this continue to happen there?”

Na kweli ilipofika jumapili december 28 2014, ndege ya AirAsia iliyokuwa imebeba abiria 162 ilipoteza mawasiliano kutoka kwenye chumba cha mawasiliano ambapo ndege iyo ilikuwa ikielekea Singapore.

“We pray that God would strengthen the friends and family members of all those involved in this tragic incident,” Joshua wrote at the end of the YouTube clip.

T.B. Joshua ametabiri matukio makubwa mawili moja likiwa hili la ndege ya Indonesia na lile la Flight MH17 ambayo ilikuwa ikitokea Ukraine kuelekea Russia, Video yake akitabiri iko hapa chini.

VANESSA MDEE AWATOA KIMASOMASO WASANII WA KIKE BONGO


Mwanadada anayefanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee.
******
MWANADADA anayefanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee kwa mara ya kwanza amewatoa kimasomaso wasanii wa kike Bongo kwa kutwaa tuzo ya kimataifa za All Africa Music Awards ‘AFRIMA’ nchini Nigeria.
Akizungumza na paparazi wetu Vanessa ambaye amepata tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki alisema anawashukuru mashabiki kwa kuwa wameonesha moyo wa kumpigia kura mpaka kuwashinda wasanii wengine wa Uganda na Kenya kama vile, Wahu, Size 8, Kaz (wa Kenya) na Jackie Chandiru wa Uganda.

“Nina furaha sana kwani ni mara yangu ya kwanza kupata tuzo ya kimataifa pia nimewatoa kimasomaso wasanii wenzangu wa kike, kikubwa nawashukuru mashabiki wangu kwa kunipa sapoti kubwa ya kunipigia kura, ninawaahidi kwamba nitaendelea kufanya muziki mzuri ambao wataupenda na kuwa mwanamuziki wa kimataifa zaidi,” alisema Vanessa.

Tuzo hizo zilizotolewa usiku wa Desemba 27 huko Lagos, Nigeria pia msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ alipata tuzo katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki huku msanii Peter Msechu ambaye naye alikuwa kwenye kinyang’anyiro hicho akikosa.

KUMBE JAY Z NDIYE ALIYEMTOA BIKRA BEYONCE.. MPWA WAKE AVUJISHA SIRI.. SOMA HAPA..!

TAARIFA za staa Jay Z  ambazo zinasambazwa na Mpwa wake kuwa alitelekeza familia yako baada ya kuwa na mahusiano na Beyonce.
Kwenye tweets ambayo hiyo akaunti imefungwa sasa, Ndugu huyo wa Jay Z alikaririwa kwenye moja ya tweets zake akisema akimlaumu ndugu yake kuwa alidata kwa kuwa ndiye alimvunja bikra Beyonce hii ni moja kati ya tweets zake.
You changed man. Your life ain't the same since that bitch came in. Now you think your family is Tina, Solo, Julez. We aren't let in your home.
You won't fogive Aunt Mickey, but you forgave your bitch's drunk sister. After she hit you like a bitch - man for the world to see.
Because she doesn't want you around your family and you say "yes" like you're some puppet. You spend your birthday in Iceland so we wouldn't get invited.
Shit Mama Gloria doesn't find it weird. She likes that bitch [Beyonce]. She tells TT and crew not to be immorial in school. She says 'be like Beyonce. She lost her innocence to your uncle'. Wait until your 21. Maybe that's why you're still in?I de-virgined over 4 chick.s. No strings attached.

BI. FATMA SALIM AZINDUA VITABU VYAKE VITATU VYA SIMULIZI ZA KALE *PICHAZ*

Mtunzi mkongwe wa vitabu Zanzibar Bi. Fatma Moh’d Salim (Jinja) akionyesha vitabu vya hadithi za kale alivyovitunga, katika sherehe za uzinduzi wa vitabu hivyo zilizofanyika nyumbani kwake Chukwani Zanzibar.
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa vitabu hivyo wakimskiliza Bi. Fatma Jinja (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo juu ya utunzi wa vitabu hivyo .
Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano na mtunzi wa vitabu Bi. Fatma Jinja huko nyumbani kwake Chukwani Zanzibar baada ya uzinduzi wa vitabu vyake.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

WEMA AFUNGA MWAKA KWA KILIO *PICHAZ*

 Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam akilia huku akibembelezwa na shost yake Aunt Ezekiel.
************
OHOOOO! Wakati pazia la mwaka 2014 likifungwa leo, mama la mama, Wema Sepetu ‘Madam’ ameuaga mwaka huo kwa staili ya kilio cha nguvu, mchapo hatua kwa hatua huu hapa... 
Tukio hilo lililozua maswali mengi bila majibu, lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 29, mwaka huu kwenye shoo ya Madam ya kuuaga mwaka 2014 (Say Good Bye To 2014) iliyofanyika katika Klabu 71, Tegeta-Kibaoni jijini Dar. 
Kabla ya kukutwa na kisanga hicho kwenye shoo hiyo ambayo Madam aliiandaa chini ya Kampuni yake ya Endless Fame, shoo mbalimbali kutoka wasanii kibao wa Bongo Fleva kama Barnaba, Izo Business, Bob Junior na wengine wengi zilihusika kisha baadaye Wema alipanda jukwaani na kumtambulisha msanii wake mpya ajulikanaye kwa jina la Ally Luna. 
“Ally Luna atasimamiwa shughuli zote za kimuziki na mimi chini ya kampuni yangu Endless Fame, na atapata huduma zote za muhimu kama inavyofanyika kwa msanii wangu wa zamani, Mirrow,” alisikika Wema. 
Mara baada ya shoo hiyo iliyoambatana na bethidei ya mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown kumalizika, Wema alikutwa na mapaparazi nje ya ukumbi huo akiangua kilio cha nguvu ambacho hakikujulikana moja kwa moja ni cha nini.
Akiwa mwenye huzuni mkubwa.

 MAUMIVU YA MAPENZI?
Hata hivyo mnyetishaji mmoja aliwatonya waandishi wetu kuwa huenda Wema analia na maumivu ya mapenzi hususan akifikiria gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa kwenye siku yake ya kuzaliwa na kusababisha aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alitilie shaka.
“Huenda huyu ana maumivu yake ya mapenzi si bure, pengine ni hili gari alilokuja nalo ndilo linamtesa vilevile,” kilisema chanzo hicho.

AUNT AMBEMBELEZA DK 13
Mapaparazi wetu walimshuhudia shosti wa  wa damu wa Madam, mwigizaji Aunt Ezekiel akitumia dakika 13 kumbembeleza staa huyo ambaye juzikati alikuwa nchini Ghana kurekodi sinema na mwigizaji kiwango nchini humo, Van Vicker.

ASEMA KABANWA NA MLANGO

Ili kutaka kujua sababu za Madam kuangua kilio kwa muda mrefu, baada ya kunyamaza, mapaparazi wetu walimvaa Wema na kumuuliza kulikoni? Msikie alivyofunguka:

UNAAMBIWA DIAMOND PLATNUMZ NA ZARI 'THE BOSS LADY' NDIO KIM NA KANYE 'KINYE' WA AFRIKA *PICHAZ*

Kabla ya kukutana na Diamond Platnumz, Zari the Bosslady alikuwa tayari ni mwanamke maarufu nchini Uganda. Utajiri na urembo wake ulimfanya aitwe Kim Kardashian wa Uganda.
Zari anamiliki msululu wa magari ya kifahari yakiwemo Range Rovers, Bentley, Limousine, Mercedes Benz, Chrysler na mengine ambapo mengi kati yake yana plate number za jina lake.
Anamiliki mijengo kibao pamoja na biashara mbalimbali kikiwemo chuo kikubwa kilichopo nchini Afrika Kusini.
Kukutana na Diamond Platnumz ambaye ukubwa wake tunaufahamu, umemfanya msichana huyo mwenye watoto watatu kuwa na nguvu zaidi na ndio maana couple yao inaweza kufananishwa na ya Kanye West na Kim Kardashian.
Kama ilivyo kwa Kimye, Zari na Diamond wana sumaku ya skendo.
Ni hivi juzi tu mkanda wa ngono wa Zari ulisambaa mtandaoni ambao uliisha kulikuza tu jina na umaarufu wake.
Kwa sasa wawili hao wameanza kuongozana kama kumbikumbi.
Baada ya kumsindikiza Diamond kwenye tuzo za Channel O kisha kuwa pamoja kwenye ‘Ciroc All White Party’ jijini Kampala, wawili hao wapo pamoja tena kwenye ziara ya Diamond ya Burundi na Rwanda.
Kwa ukubwa wao kila mmoja, wawili hawa sasa ni miongoni mwa couple zenye nguvu zaidi katika burudani barani Afrika.

RAYUU AANIKA UKWELI KUHUSU PICHA ZAKE ZA KIMAHABA ZILIZOGAA MTANDAONI JANA! *PICHAZ*

Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.
MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amezua gumzo baada ya picha zake zinazomuonesha akiwa chumbani na mwanaume kuenea mtandaoni, hukukijana huyo akionekana kujichora tatoo yenye jina la mwanadada huyo.
Kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Brown hakuweza kupatikana ili kuthibitisha uhusiano wake na mrembo huyo, lakini Rayuu alikiri kuwa ingawa picha iliyowekwa mtandaoni ilionyesha wakiwa kikazi zaidi, huyo ni mpenzi wake wa siku nyingi.
Hizo picha ni sehemu ya vipande vya kwenye wimbo wa huyo mwanaume, ukweli ni mpenzi wangu wa siku nyingi na anataka kunioa, ndiyo maana kafikia hatua ya kujichora jina langu, sina kipingamizi, tunaomba Mungu atufanikishe tufunge ndoa,” alisema.

YAFAHAMU MATUKIO MAKUBWA YALIYOITIKISA TANZANIA 2014 *PICHAZ*

Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mshindi wa shindano la Big Brothers Idris.
MWAKA 2014 unafikia tamati leo. Kwa Watanzania, kuna matukio mbalimbali yaliyojitokeza ambayo yameacha kumbukumbu kubwa kwao. Hata hivyo, yafuatayo ndiyo mambo yaliyotia fora zaidi.
Viungo vingi vya binadamu vikiwa vimetupwa katika machimbo ya kokoto yaliyopo Bunju, Dar.
VIUNGO VYA BINADAMU VYASHTUA 
Jumatatu ya Julai 21, 2014, nchi ilipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kusambaa kwa habari kuwa viungo vingi vya binadamu vilikutwa vikiwa vimetupwa katika machimbo ya kokoto yaliyopo Bunju, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Watu wengi waliamini viungo hivyo vimetokana na mauaji ya halaiki, hasa baada ya kukutwa kwa mabaki ya mikono, miguu, mafuvu, viganja na vingine vingi. Lakini baadaye ikaja kuthibitika kuwa viungo hivyo vilitupwa kimakosa na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), ambacho pia kinaendesha hospitali.
Viungo hivyo mbalimbali vya binadamu vilikuwa vikitumiwa kimasomo na madaktari wanafunzi, ambavyo vilipaswa kuteketezwa baada ya matumizi. Kitendo hicho kilisababisha serikali kukisimamisha kwa muda chuo hicho kutokana na uzembe huo. Viungo hivyo vya binadamu, hupatikana katika maiti mbalimbali zinazokosa ndugu wa kuwazika na hutolewa na hospitali ya Taifa Muhimbili.
UKAWA.

KUZALIWA KWA UKAWA
Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuridhia zoezi la uandikwaji wa Katiba Mpya, Tume ya kukusanya maoni chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba ilifanya kazi yake vizuri na mwaka huu katiba hiyo ilipelekwa Bungeni ambako Bunge Maalum la Katiba lilikutana ili kupitia vifungu vyake kabla ya kuipeleka kwa wananchi kwa ajili ya kuipigia kura ya kuikubali au kuikataa. 

Kulitokea malumbano makali kati ya wajumbe wa Bunge hilo juu ya vipengele kadhaa, hasa muundo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano. Wajumbe waliotokana na Chama Cha Mapinduzi, walipendezwa na muundo wa serikali mbili kama ilivyo hivi sasa, wakati wapinzani walitaka serikali tatu. 

Misimamo hiyo ilileta utengano mkali kiasi kwamba wajumbe wa upinzani wakiongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuamua kususia vikao hivyo, wakipinga kile walichokiita uchakachuaji wa rasimu ya katiba ya Jaji Warioba. Ususiaji huo ulisababisha kuanzishwa kwa kundi lililoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Jaji Warioba Kuanzishwa kwa umoja huo uliovihusisha vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, kulisababisha kundi hilo kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja katika chaguzi zijazo, wakianzia na uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika katikati ya mwezi huu. 

JAJI WARIOBA APIGWA
Baada ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kumaliza kazi yake na kuikabidhi katiba pendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete tayari kwa ajili ya kuipeleka kwa wananchi ili kupigiwa kura ya maoni, kulikuwa na mkanganyiko miongoni mwa watu juu ya kilichomo ndani ya katiba hiyo, baadhi wakipinga kuondolewa kwa vifungu vingi vilivyokuwa na masilahi kwa nchi.
Miongoni mwa wanaoongoza harakati za kupinga kuondolewa kwa baadhi ya vifungu vilivyowasilishwa na Tume hiyo, ni Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere ambayo mara kadhaa imeandaa mijadala ya wazi, lakini wakimtumia Jaji Warioba kama msemaji wake mkuu.
Kitendo hicho kimesababisha Warioba kuonekana kama yupo katika mgogoro na chama chake na siku aliyofanyiwa fujo na kupigwa katika ukumbi wa mikutano wa Ubungo Plaza, wanaodaiwa kuwa makada wa CCM wanatajwa kuhusika.
Aliyekuwa mshindi wa miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu kabla ya kuvuliwa taji. Kitendo hicho pia kilikosolewa na wachambuzi wa habari za kisiasa wakidai ulikuwa ni udhalilishwaji wa mtu aliyewahi kuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania na hivyo kuhoji ulinzi wake.

MISS TANZANIA YAFUNGIWA MIAKA 2
Shindano la Miss Tanzania limejijengea heshima kwa muda mrefu tokea lilipoanza tena mwaka 1994. Ingawa kumekuwa na malalamiko ya chinichini juu ya kuwepo kwa hila, safari hii lilijikuta likipata aibu kubwa, baada ya mshindi wake wa mwakahuu, Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri hivyo kuibua sauti zilizotaka kunyang’anywa kwa taji hilo.
Baada ya skendo hiyo kuchachamaa, Baraza la Sanaa la Taifa liliendelea na uchunguzi wake dhidi ya malalamiko mengi yaliyowahi kuripotiwa na katika tukio ambalo halikutarajiwa, shindano hilo limesimamishwa kwa miaka miwili kutofanyika na sababu nyingine iliyosababisha hatua hiyo, ni kugundulika kuwepo kwa rushwa ya ngono katika hatua mbalimbali za shindano hilo linaloanzia vitongojini.
Aliyekuwa msanii mkongwe katika uchekeshaji maehemu Said Ng’amba ‘Mzee Small’. 

VIFO VYA WASANII WA MUVI NA MUZIKI
NI mwaka mwingine ambao wasanii wengi, wakiwemo wacheza filamu na wanamuziki walifariki dunia. Mei 27 mwaka huu, msanii wa Bongo Muvi, Rachel Haule alifariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alikwenda hospitalini kwa ajili ya kujifungua, lakini baada ya kitendo hicho hali yake ilibadilika ghafla ambapo alihamishiwa ICU na hali yake ilizidi kuwa mbaya kabla ya kupoteza maisha.
Recho alifariki wiki moja baada ya muigizaji mwingine maarufu, Adam Kuambiana kufariki ghafla. Baada ya hapo, msururu wa wasanii ulifuata akiwemo prodyuza George Tyson, msanii mkongwe katika uchekeshaji Said Ng’amba ‘Mzee Small’, mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’, Side Mnyamwezi, Yesaya Ambilikile ‘YP’ , Maalim Gurumo, Amina Ngaluma, Aisha Madinda na Shem Kalenga. 

6. TEGETA ESCROW NA BILIONI 306
DAVID Kafulila, mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alianza kama utani, akiwatuhumu vigogo wa serikali kuhusika na wizi wa shilingi bilioni 306, mali ya umma katika akaunti ya Tegeta Escrow. Mwanasheria Mkuu wa serikali wakati huo, Jaji Fredrick Werema akamdhihaki kwa kumuita Tumbili kabla ya kumtishia kumkata kichwa. Dhihaka zikaendelea kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kuziita nyaraka alizokuwa nazo Kafulila kuwa ni makaratasi ya kufungia vitumbua.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila. Kadiri muda ulivyokuwa unakwenda, ikaja kuthibitika kuwa ni kweli kulikuwa na uchotwaji wa fedha hizo isivyo halali, kitu kilichosababisha nchi kuingia katika kashfa nyingine ya mabilioni ya fedha, ukiacha EPA, Richmond, Rada na Ndege ya Rais. 

Mshindo wa skendo hiyo umeondoka na vigogo watatu, waliotanguliwa na Jaji Fredrick Werema aliyejiuzulu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka aliyeondolewa na Katibu Mkuu Maswi, aliyesimamishwa ili kupisha uchunguzi dhidi yake. 

HOMA YA DENGUE
Ni ugonjwa mpya ambao uliingia na kumshtua kila Mtanzania, kufuatia kasi yake ya kuua na utata wa tiba yake. Uliwafanya watu kuogopa na kuitaka serikali kuhakikisha tiba yake inapatikana mara moja ili kuondoa hofu miongoni mwa wananchi. 
8. 

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
INGAWA umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitano, lakini uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu ulipata hamasa kubwa na kufuatiliwa kwa karibu na watu wengi. Ingawa kama ilivyotegemewa, Chama Cha Mapinduzi kuibuka na ushindi, lakini hata hivyo, matokeo yake yalionyesha dalili za kuimarika kwa vyama vya upinzani baada ya kushinda viti takribani 3000 vya uenyekiti wa serikali za mitaa.
‘Diamond platnumz’. Uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI) iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, ulikuwa na dosari kadhaa zilizomlazimisha Waziri wake, Hawa Ghasia, kuwasimamisha kazi Wakurugenzi, kuwafukuza na wengine kupewa onyo, kufuatia uzembe wao katika kusimamia zoezi hilo muhimu nchini.

DIAMOND, IDRIS WANG’ARA
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ mwaka 2014 aliwaongoza wenzake kuing’arisha Tanzania kimataifa baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo tano barani Afrika. Hizo ni pamoja na tatu kutoka kituo cha televisheni cha Channel O, jijini Johannesburg na The Future Awards Africa iliyofanyika Lagos, Nigeria.
Ushindi wake huo ulimfanya kupata mapokezi makubwa ya aina yake alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na mashabiki walimsindikiza hadi ukumbi wa Escape One kwa miguu, umbali wa zaidi ya km 20.

Aidha kijana Idris Sultani alikuwa Mtanzania wa pili kushinda shindano la Big Brother, baada ya Richard Bezuidenhout kuibuka kinara mwaka 2011. Idris, aliyeshinda Big Brother Hotshots alijinyakulia kitita cha dola 300,000 baada ya kumbwaga Tayo Faniran wa Nigeria.

MMMH: WEMA SEPETU NA EX WA ZARI 'IVAN' KUNAAANIII???

HIVI Karibuni Wema Sepetu alimuomba urafiki katika mtandao IVAN ambaye ni ex wa Zari 'The Boss Lady' baada ya kuanza kwa kulike picha ya mkaka huyo….
Mmmmmh! Kwa nnavyohisi hii ni couple nyingine in town…!  Yetu Macho.

DIVA ANAYESUMBUA KWA SHAPE BONGO MOVIE WELLU A.K.A 'MATILDA' ATUNDIKWA UJAUZITO

Msanii wa filamu Bongo mwenye shepu ya hatari sana, Wellu Sengo, ‘Matilda’. (Wapili toka kushoto)
******
IMEVUJA! Msanii wa filamu Bongo, Wellu Sengo, ‘Matilda’, licha ya kuwa na mtoto mdogo ambaye hajafikisha hata mwaka, inadaiwa tayari amenasa ujauzito mwingine.
Chanzo makini kinaeleza kuwa ujauzito huo ni wa mmoja wa wasanii wenye majina maarufu hapa nchini, ambao wamekuwa katika uhusiano kwa muda mrefu sasa.
Katika mawasiliano kwa njia ya simu, Wellu baada ya kubabaika, alikiri kuwa na ujauzito na kumtaja msanii huyo kama ndiye mwenye mzigo, lakini jina lake linahifadhiwa kwa sasa kwa vile mwenyewe hakupatikana ili kuzungumzia madai hayo.
“Haa, wewe nani kakuambia habari hizi, lakini aah, ni kweli bwana nina ujauzito na mwenyewe ni (anamtaja jina). Si unajua tena mambo ya kawaida haya,” alisema muigizaji huyo. 
Msanii huyo anayetajwa kuhusika na jambo hilo, ambaye hata hivyo ni mume wa mtu, amekuwa akionekana kuwa Wellu karibu katika maeneo mengi ya starehe na kijamii akiwa. Baadhi ya wasanii wamekuwa wakimdhihaki mwanaume huyo kwa kumuona kuwa haendani kimuonekano na mwanadada huyo.

ICHEKI EXCLUSIVE VIDEO YA VANESSA MDEE FT. BARNABA, AIKA, NAHREAL, AVID - WCD


SOMA WALICHOJADILI MASHABIKI KUHUSU VIDEO YA ALIKIBA ‘MWANA’, KUHUSU VIDEO KUTOFUATA NA MAUDHUI YA WIMBO

WIKI moja baada ya video ya Alikiba ‘Mwana’ iliyofanyiika Afrika Kusini na kuongozwa na Godfather, itoke, kumekuwa na maoni tofauti kuhusiana na video hiyo. Baadhi yao wameonekana kuifurahia na wengine wameonekana kutoridhishwa na baadhi ya vitu.
Baadhi ya waliotoa maoni wamesema kuwa walitegemea kuona video yenye script inayoendana na maudhui ya wimbo ili kumuwezesha hata mtu asiyejua kiswahili kuweza angalau kuelewa kwa kutazama vitendo, huku wengine wakitetea kuwa si lazima kila video iwe na story inayoendana na wimbo.
Haya ni baadhi ya maoni ya walioitazama video hiyo kupitia channel ya Alikiba Youtube ambayo hadi sasa ina views 185,005:

king dady
video iko swafi sn, ila k2 kmoja cha kurekebsha, ujue bana music ni luga ya wote, yan kwmba wimbo ukiwa sawa na baadhi ya matukio ya kweny videoo kidg inasaidia ht km wacojua swahil wanaelewa ulichoimba kw kutizama video, hapo kw wacojua ulichoimba wataona swafi, ila kw tunaojua ulichoimba kiuukwe bnafsi ckutegemea km hii video ingekuja kuw hivi… NLICHOPENDA NI KWAKUA UMEENDA KUFANYA KWNY PRODUCTION KUBWA, ila hukukua na maelewano mazuri kat yawew na director wa hii video .. next time try 2 do somthing better, yt ya yte mzik wa africa lzm ukue

john senior
kiukweli video ni kali kwa alikiba na anajitahd kulitafta soko la kimataifa ila maudhui ya wimbo hauonekani kabisa kwenye video yaan kwa mtu asiyejua kiswahili ukimwambia hii nyimbo ina ujumbe mkali lazima apinge nimegundua ali alikamia sana kuifanya video hii ndo maana yametokeA all in all ni mtazamo wangu kama shabiki

mchikirwa ndelejai
Those who want the video to have a story line the same as the song,this aint a movie bana…….Hayo yalipitwa na wakati,u sit n enoy the video, and stop comparing diamond to kiba or vice versa,they are their own artists n they all have reache where they are by merit!!

Eloi Laban
THE FACT IS WHOEVER DOESN’T UNDERSTAND SWAHILI… ENJOY THE DANCE. PERIOD! THIS VIDEO QUALITY I CAN SAY IS THE BEST EVER DONE

IBRAHIM PRIVATUS
HAPO NDIPO KILA SIKU ALIKIBA UNAKOSEA NA UNAONEKA BADO SANA KWANINI UNAKURUPUKA? UNAWAUMIZA MASHABIKI WAKO NA KUWAANGUSHA VIBAYA SANA YAANI HUU WIMBO SI WA DANCE HUU WIMBO ULITAKIWA UWE NA VITENDO NDANI YAKE YAANI MAUDHUI YAMEPOTEA KABISA NA UMEFANYA VIDEO IONEKANE

Geofrey Adroph
Uzuri wa wimbo ni tofauti sana na mwonekano wa video maana nilitegemea kuona binti ambaye anatumia madawa na istoshe tena analewa hapo ndo ningeona dhima ya huu wimbo inabidi ujipange sana Bro

athuman gullam
Watu wabadilike na kuweka chuki zao mbali, huu ni music sio movie ambayo inaonyesha kila tukio lililoandikwa…ebu angalien video za wanamuziki wakubwa dunian wanafanya nn sio kulaumu na kukosoa msivyo vijua …eti video haiendan na maudhui ya nyimbo nk. Angalieni video kama NEW FLAME, SHOULD HAVE KISS YOU,ROYAL hizo ni mfano tu wa videos za Chris brown na zinabamba kila kona ya dunia …Alikiba u did well with ur btful video n everything inside it is good .toeni video zenu tuone # HATERS #

alex mbuli
Honestly…hii video siwez angalia Mara mbili..inaboa.. kwa msanii mkubwa kama wew tunatarajia mambo makubwa pia toka Kwako…Ila kwa hapa umekurupuka sana kaka..kipaji cha kuimba unacho..Ila wew sio msanii..video yako haiendani na maudhui..Ingawa quality ni nzuri…kwa ushauri tu naomba mshirikishe diamond na ukubali yeye kakuzidi kiusanii..mtatoa Kitu Kizuri sana

IDP MUZIQ
I am a musician n ur number one fan from Kenya,honestly u tried but hata hivyo still theme ya song haimbatani na video if i were u ninge do away with this video n do it again before its too late.halafu pia fanyia video kama hii TZ coz south Africa hata hawelewi unachozungumzia kisha ungewashirikisha wale madancers wako wa serengeti fiesta otherwise competition ni noma

Julius Mbungo
BIG UP ALI KIBA.. video ni kali sana.. wanaosema haijaendana na maudhui ya wimbo hawajielewi na wanaongea kwa ushabiki.. acheni mambo ya diamond hapa.. yeye anafanya yake na kiba mwachen afanye yake.. nyie wapumbavu ndio mnaoleta fitna kwa kulinganisha watu.. the video is nice.. angalien nyimbo kibao mbele sio lazima ziendane na maudhui mfano mzuri ni loyal ya chris brown mnaona maudhui kwenye video pale au?? shut yo mouths kama hamna cha kuongea

hyme chicco
Video nzuri sana…Maana ya hii video ata wasio elewa kiswahili wa enjoy the dance,kwasababu nyimbo ni ya kuchezeka!

Dotto Kahindi
Wimbo unamzungumzia binti aliyeloweza Dar halafu video inaonyesha mitaa ya Afrika Kusini, unajua hawa maproducer wa video wasiwafanye wasanii wa bongo kuwa watumwa, yaani nimeumia sana, nilitegemea kumwona huyo binti na mikasa iliyomkuta lakini kiukweli umeniangusha sana

deo alphonce
Nice video ,japo watu wnalalamika hakuna story but creativity ya pale club. Iko poa sana

Imani Tutu
Mchizi video iko bomba sana ila Naona bado unazunguka palepale, nikiiyangalia Iyo video nikama na iyangalia ile ya ommy dimpoz (ndagushima) japokuwa ni idea tofauti. fanyagarama alafu kitu kionekane ila sio kwasababu umefanyia nje ya nchi tu!!

fred eugene
Tusiwe wazee wa kukariri Video NZURI,HApo Hamjaona Story Ndo Maana mmeona mbaya Hamjui kwel yan….@VANESSA MDEE-HaMJUI Mbn Story Haijaendana AU…
Tusiwe WANAFKI……Pia Shabikia MZIKI Sio Mimi @Team Kiba Mimi @Team Diamond UFALA Huo…Aya Bhasi Next Time Direct wewe.
Penda au Usipende Nzuri.

nicolas jonathan
Ushauri tu kwa wanaotaka maudhui. “sikuizi mziki ni mpana sana na maigizo ya kibongo ni mmziki wa zamani,, skuizi tunatka kitu unique ambacho hawajfnya watu weng ndo kitutoe. Kwaiyo we kma ulikua unasubiri movii imekula kwko afu usitake mtu atoe video unayoitaka weee…. By the way its butful video

Piter Asifa
Video iko poa tatizo ppl wame kariri sio lazma iende kwa matukio sio movie hiyo hiyo ni Video ya nyimbo as friend apo # omonyi alivo ongea

ibrahim masoud
kiba ndio amekosea hii video, lakin uaweza ukaotea uelekeo wa iyo vdeo. kma angefkiria kuweka mtoto wa iringa alie kimbilia dar ingekua nibonge ya uupuz goal nikuiona mtv, trace na channel kubwa ulimwenguni. chukulia hii ni moja ya zile video ambazo huelew znaongelea nn ila tunazpenda, kma ngapi mnajua maana ya skelewu lakin cheki kideo hutaki kujua amnongelea nn

neysha keys
video iko kawaida mo than the expectations. ukwel usemwe kwan yy nan bna. vdeo nying ambazo haziendan n maudhui labda za kizungu co za kiswahil o africa probably zA RAP. quality iko poa mmevaa fresh lkn content 0. muandika scripts hajakua ideas vzr. but ucjali utafka level zile jikakamue hlf kaa na walio top utafanikiwa 2

Henry Tudor
Mnataka maudhui yapi sasa izo ni video za kizaman mtu anavuta madawa ya kulevya anaoneshwa au mnataka iwe kma mac muga anaonekna ana kula bata sauz?mbna dimond kvaa kma shakazulu kwny vdeo ya mdgmdgo na wakat wmbo ni maadhi ya tz sio sauz kjaza na wazngu tu mle kitolondo cjui ndo yle mzngu ata atumwon,videeo kali bhana alikiba pop it in niqqa

Annarisa Peter
video nzuri sana,, baada ya watanzania kusifia vitu vizuri si ndo wa kwanza kwa majungu! let us support what is ours tuache chuki binafsi kwenye maendeleo! ukiulizwa kwa nini unamchukia m2 jibu huna! if you don’t like someone omba Mungu akusaidie umpende cyo kuendeleza chuki haijengi, hautafika mbali kamwe. Go kiba Mungu atakupigania.

Abdulaziz Raha
Let me tell you mtu anapofanya kitu na kinapokuwa hakipo sw na ukampa ushauri haimaanishi kwamba unamchukia… kusema kweli quality, mavazi vyote vipo poa tatzo maudhui hayaendani na nyimbo… ali kiba ni msanii wetu waTanzania ss anapokosea sisi tusipomrekebisha tutakuwa hatumjengi… Tanzania one

FARAJI MWANJA
sasa tunaangalia quality video angalia video nyingi za nje sikiliza kwa makini alafu angalia na video kama zinaendana mambo ya kizamani hayo ndugu

kazungu mabeyo
wimbo huu haujatendewaa hakii , video ya kawaidaa sanaa, sikutegemeaaa kama itakuwaa ya kawaidaa namnaa hiii, but it is the good start let hope for best videos in future… always on yourside king kiba.

Airborne Films
ALI KIBA HAS DONE IT GREAT. THIS VIDEO DESERVES AN AWARD. IT WAY MUCH ABOVE STANDARDS. ITS YOUR RESPONSIBILITY AS A VIEWER TO RELATE TO IT. BUT DONT EXPECT ALI KIBA TO DO SOMETHING ACCORDING TO WHAT TANZANIANS WANT. UNDERSTAND THAT MUZIK IS AN ART AND NOT LIMITED TO CREATIVITY AND QUALITY.
SO PEOPLE NEED TO THINK FIRST BEFORE ARGUING ON A VIDEO YET THEY ARE NOT EITHER FILM MAKERS OR VIDEO DIRECTORS.
GOOD STUFF ALI KIBA. I GIVE IT 10/10. U R GONE INTERNATIONAL AND THATS THA WAY IT SHOULD BE.

Alex Kasangaya
Video ni mzuri and ofcoz inachezeka kiclub and anywhere… ila ukisema chrbrwn katoa loyal vdeo wth no content thn unataka alikiba afanye hvyohvyo while yeye kiba anatafuta int market utakuwa wakasoea…… CB z arleady knwn worldwide…… ushauri wangu on vdeo re do it bong0 with content in it and great dancers esp ladies

Clarence John
IT IS ONE OF THE BEST VIDEO from KIBA ever been before!… tunakosea sana tunapomlaumu Kiba kwa suala la SCRIPT..mi nadhani ni makosa ya DIRECTOR!….angeimba OFF KEY hapo tungemlaumu kiba kwa kutojua kuimba!…lakini suala la VIDEO anaetakiwa kulaumiwa kwanza ni DIRECTOR..alafu sio kila kitu kiwe kwenye SCRIPT sio BONGO MOVIE hiyo…Aliyemshauri akafanye video kwa GODFATHER ndio alimuingiza choo cha kike..huwezi kwenda kwa rafiki wa ADUI wako ukategemea atakushauri vizuri ili umuangamize adui yako ambae kwake ni swaiba!..

claudy muhala
Wengine wameelewa wengine hawajaelewa, ila yote ni taswira halisi ya jinsi ulivyofanya vizuri na jinsi ulivyoboronga. Sisi humu wengi ni mashabiki wako na kikubwa sio tu ni mashabiki lakini tunakupenda na kutaka kuona unatoa kitu kizuri. Unajua hii nyimbo imetoka kitambo na watu wanaifanhamu na waliisubiri kitambo sana ila walitegemea kuona dhima halisi ya nyimbo

Rasheed Rai
The song is great…I just feel that Kiba would have done better than this on the video.
I like the audio more than the video. GodFather lacked some creativity on the concept of this video. I don’t see the subject of the song in this video.

MAGESA JOSEPH
Kichupa kipo poa sana af umekuja na style yako mpya safi kiba ila maudhui na chupa vpo opposite bro huu mziki co wako ni wataifa zima xo ww unatuwakilisha na tunataka uwakilishe vyema zaidi

Cecy Steve
Ni mbayaaa haiendani kabisa na maudhui mara mia angefanya kama story kidogo ndani kucheza kwenyewe hajui

Lelo kaka
WABONGO HATUELEWI MAANA YA MAUDHUI. AND THEN HATUNA MAAMUZ YASIYO SAHIHI HIVI MTU KAKAKURUPUKA TU AND THEN ATOE KITU KIBOVU EMB KUWEN WAELEWA VIDEO INA UJUMBE ILA SISHANGAI SHULE NI NDOGO NIKAMA WATOTO KILA KITU MTAFUNIWE. MSIKURUPUKE FATILIEN KWAMAKIN MJUE ANACHOKIMAANISHA

Azeez S.A
Script mbovu…hii video itaupoteza wimbo. Wimbo ni mkali sana kuliko video. Halafu huyu God Father ambaye watanzania wengi wanamkimbilia huko South mbona wa kawaida tu. Tunajua ana connection na vituo vikubwa vya TV Afrika na pia ana quality nzuri picha. Kama hizo ndo sababu za kumkimbilia basi wasanii wanapaswa kuandaa script wenyewe. Wasanii mnapaswa kutake control ya video zenu, maana zikiharibika hasara kwenu.

Tariki magowa
Halafu siyo kila k2 muige kwenda kwa GODFATHER vingene fanyeni hapahapa home na itapendwa2. sio mnakwenda kuwasumbua wa2. wanaacha kazi zao za maana mnapeleka ujinga. ole wenu mludie tena na sio ww2 brather kiba bali ni wale wote wanao taka kwenda kupeleka ujinga kwa GODFATHER. sory ni mtazamo2

Mwinjuma Lukwar
kiukweli nisiwe mnafiki huyo mwana sijamuona anaye semwa hapo maana sioni uhusiano wa wewe kujiangalia kwenye kioo na kumtaja mwana aliye pagawa na anasa za mjini ,,hey kaka badilika ndugu uadui tuweke pembeni kubali kujifunza maana inaelekea hutaki kujifunza na ndo maana hata instagram hujafollow mtu hata mmmoja hiyo imejidhihirishaa ona sasa unatuangusha mashabiki wako good quality but contentlessss

ASHER OMONDI
This guy Godfather production Im yet to understand why East African musicians rush to him for the video productions! Look, the video runs for 2 minutes before you see any lady figure who should have been the main character here.The theme in the song is way sooooo different from what is in the flick!! It is all about Ali Kiba and the theme “LOVE” in it is lost.BORINGLY BORING!!!
Wewe una maoni gani? Andika chochote hapo chini.

Chanzo: Bongo5

ZILIZOSOMWA ZAIDI