NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Wednesday, May 29, 2013

FILAMU MPYA YA KITANZANIA


NYIMBO MAALUMU KWA WENYE FISTULA

KIPAJI TOKA UGANDA, GOLDIE FT NAVIO!!

MTAZAME MAREHEMU NGWEAR KATIKA CLIP HII

BINGWA WA FREESTYLE, ALBERT MANGWEAR ALIVYOZIMA GHAFLA


IKIWA ni siku nyingine tena ambapo taifa hili limekuwa likizidi kupoteza wanamuziki na wasanii wengine wa sanaa mbalimbali, lakini leo majonzi yamewakuta wapenzi wa muziki wa kizazi kipya Almaarufu BONGO FLEVA kwani rapper maarufu ALBERT KENETH MANGWEHA alilipotiwa kufariki dunia huko Afrika Kusini, katika hospital ya St. Hellen huku chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika vizuri.
 
 kijana huyu mwenye asili ya mkoa wa ruvuma, akiwa pia ni mzaliwa wa mkoa wa mbeya mnamo tarehe 16 mwezi wa 11 mwaka 1982 alikua ni mtoto wa mwisho katika familia yao ambaye alipata elimu yake ya msingi huko Dodoma, shule ya msingi Mlimwa na kusoma Shule ya Sekondari na Chuo cha Ufundi Mazengo Mjini Dodoma.
Marehemu Abert Mangwea enzi za Uhai wake
Amefanya nyimbo nyingi ambazo zimepelekea umaarufu wake kama: Kama ni demu Sikiliza akiwa na Lady Jay Dee, Mikasi aliyoifanya chini ya Ludigo na nyingine nyingi zilizokuwa katika album ya Mimi.
Marehemu Albert Mangwea (Kushoto) enzi za uhai wake  akiwa na TID
Wasanii wengi sana wameahirisha show walizokuwa wanatarajia kuzifanya ikiwa ni kuonyesha umoja wao na kuwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi walichonacho, wasanii hao ni pamoja na mwanadada Lady Jay dee, Kikosi cha Mizinga, TID, MwanaFA, Izzo Bussiness.nk 
 
Mungu ailaze roho ya Marehemu, pema peponi.. Ameeen!

Nay wa mitego Ft. Diamond platnumz - Muziki gani (official video)

Thursday, May 9, 2013

KIFUNGO CHA NJE MWAKA MMOJA CHAMKABILI SHEIKH PONDA




  1. Akiteta jambo na baadhi ya watu!

    Akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari!

    Mhadhiri Maarufu wa Kiisilamu Sheikh Habibu Mazinge (suti nyeusi) akimlaki Sheikh Ponda mara baada ya kuachiwa huru.


    Ponda akizungumza na waandishi wa habari.

    "Kuna utaratibu umeandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu Tanzania tutawaita tutazungumza kwa pamoja lakini kikubwa ninachoweza kusema kwamba tumeshuhudia uonevu na dhulma tunayofanyiwa waisilamu nanyie ni mashuhuda hapa leo." Alisema.

    Safari ikaanza!

    Akaingia kwenye gari!

    Msafara ukavamiwa na wafuasi baada ya dereva wa gari lake kusimamisha awasalimie wafuasi hao jambo ambalo polisi walikuwa hawalitaki na kuzua mabishano mazito lwenye mataa ya Maktaba Squire.

    Wafuasi wakajimwaga barabarani!







    Wafuasi wakivamia gari kumsalimia baada ya dereva wagari hilo kulisimamisha huku polisi wakimvamia aliondoe gari hilo haraka.

    Waliufukuza msafara huo hadi pale ulipotokomea!



    Msafara uliendelea kukimbizwa hadi walipotokomea mbali kwa spidi ya kuwakimbia.

    Waumini wa dini ya Kiisilamu ambao walijitokeza kuisikiliza hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wakimbeba juu mmoja wa wafuasi wake ambao walishtakiwa pamoja mara baada ya kushinda kesi hiyo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.



    HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili.

    Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.

    Mara baada ya kutolewa hukumu hiyo mahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.

    Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.

    1. Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya ardhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo la umiliki.

    2. Upande wa Serikali haukuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.

    3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.

    4. Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.

    5. Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda.



    Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu.

    Tumewashinda!

    Furaha!

    Machozi yalitiririka, Jazba na ahawali zikapanda!

    Safari ya kuelekea Mtambani Kinondoni Ikaanza.

    Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia nduguyake kutokana na kushinda kesi hiyo.

    "Pole ndio safari ya kusaka haki" Ndugu alisikika kabla ya kulia.

    Wapo waliokuwa kwenye majengo ya karibu wakishuhudia!

    Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari endapo lolote litatokea.

    Waandishi nao walifanya mahojiano na baadhi ya washtakiwa na ndugu wa washtakiwa hao.

    Ulinzi wa Ponda wakati wa kuondoka mahakamani hapo baada ya kuachiwa.

    Msafara wa ulinzi ukiondoka Kisutu!

    Wazee wa farasi nao walikuwepo
     Chanzo: Jamiiforums

MASHARTI 5 WALIOPEWA WANAFUNZZI WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA (I.A.A) ILI WARUDI CHUO


Wednesday, May 8, 2013

MHE. RAIS JAKAYA KIKWETE ALIPOWATEMBELEA WAHANGA WA BOMU JIJINI ARUSHA


Friday, May 3, 2013

MFAHAMU SUPER STAR ANAYECHIPUKIA KATIKA TASNIA YA FILAMU NCHINI, NI MTOTO WA 'CHUCHU HANSI'

Farihiya katika pozi

Farihiya akiwa katika scen na chek budy

Kwa hakika waswahili husema mtoto wa nyoka ni nyoka na simba hawezi kuzaa swala hili limejidhihirisha wazi kwa mtoto Farihiya mwenye kipaji cha ajabu na anakuja kukimbiza vilivyo katika soko la filamu Tanzania

Mtoto huyu ambaye ni mtoto wa kwanza wa msanii wa filamu nchini chuchu hansi ameonyesha kumrithi na pengine kuja kumzidi mama yake mzazi kwa jinsi alivyoonyesha umakini na uchezaji wa hali ya juu katika filamu hiyo ya inayozalishwa na kampuni ya Rj.


Hapa akiwa na wasanii wenzake kama johari chek budy na crew ya Rj akipokea maelekezo toka kwa Director

Farihiya mtoto mwenye kipaji cha ajabu ameshirikiana na wasanii wakubwa katika kazi hiyo kama Blandina chagula johari,Mohamedy Nurdini Cheki Budy,Stanlay Msungu Senetor,Mzee Masinde,na wengine wengi,wakipiga stori na thesuperstarstz wasanii hao kwa nyakati tofauti wamemuelezea mtoto huyo kuwa ni moto wa kuotea mbali na kuwaasa wasanii watoto kukaa mkao wakula kwani mtoto huyu ni balaa.


Hapa Farihiya katika scen na Chek budy wa pemben aliyeshika bumu ni sound man wa kutegemewa Rj

Mimi ni produser wa filamu na nimefanya filamu nyingi za kuwashirikisha watoto ila mtoto huyu ana kipaji cha ajabu kwanza ushikaji wa script wa farihiya ni balaa pili uchezaji tatu anakijua kingereza vizuri si chakubabaisha hii itamsaidia kuwa msanii wa kimataifa zaidi tofauti na wenzake wanatumia kiswahili tu na kujikuta wanalizunguka zaidi soko la ndani alisema chek budy.

Kwa upande wa johari alisema kampuni yake haibahatishi kwani humlenga mtu kulingana na story pili hata ubora wa picha zetu tumeongoza na tumechukua tuzo nyingi sana za kampuni yenye kutengeneza filamu bora zenye muonekano mzuri kuanzia picha sauti na mwanga.hivyo nachoweza kusema anakuja kwa kasi na ameonyesha makubwa katika filamu hii ya wrong hope alisema johari


Hapa akipozi na Camera man wa Rj company

kwa uapande wa yeye alipohojiwa na thesupestarstz alisema anamshukuru mungu kumpa kipaji hicho na ameahidi kukitumikia mara atakapo maliza shule,Unajua kwasasa nipo shule so nikimaliza shule nitaingia rasmi katika soko la filamu ila nategemea kusomea kabisa filamu ili nichanganye na kipaji alisema




Sifa yake kubwa hapendi kupoteza muda akimaliza scen anauliza kama anashuti kisha huingia kusoma script

Kwa upande wa chuchu ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo alisema kwanza kwake ni faraja kuona amepata rafiki na mtu pekee anayeweza kurithi kipaji chake na anafurahishwa sana na hilo ndio maana anajitaidi kumpa suppot kwa kila kitu anachokitaka kukamilisha ndoto yake,Kusema kweli nafurahi sana kwani nimepata mtu wa kunirithi kipaji changu nitajitadi sana kumpatia malezi bora na kumuonyesha njia pekee za uigizaji ili afikie malengo yake ikiwa ni pamoja na elimu ya kutosha,aliendelea kueleza mama huyo wa watoto wawili.


Hapa akiwa na make up wa Rj

Ama kwa hakika mtoto huyu ameanza vyema kwani thesuperstarstz imezisikia kauli kadha za mastar ambao pia ni ma director wakiongea kumtafutia filamu kali ili acheze,kwa upande wa farihiya mwenyewe alipoulizwa kama annaipenda sanaa alisema naipenda sana ila kwa sasa sitaki tena hadi nimalize shule naipenda shule sana aipohojiwa kama ikitokea akaitwa tena atakuwa tayari aliji kwa kifupi nitakuwa tayari bt iwe haingiliani na shule kama ilivyokuwa hii



Hapa akiwa na Mr creator Steven shoo lightman Director

Nae Director wa movie hiyo Juma Chikoka au Chopa amesema mara nyingi filamu zinazosumbua katika kuziongoza huwa ni za watoto ila amekiri kuwa katika filamu hii hajapata tabu kwani huyu mtoto amekuwa kama msanii mkubwa kwanza anashika script na anacheza katika kiwango cha juu sana hadi mtu unashangaa


Hapa akiwa na Said Baraghash sound man wa Rj

Ama kwa hakika Farihiya anaonyesha kuja juu hivyo wadau mpeni suppot kwani mama yake tu hawezi bila nyinyi wadau thesuperstarstz imeshuhudia filamu hiyo ikirekodiwa maaeneo ya mbezi huku produser wa movie hiyo blandina chagula johari akiongea na thesuperstarstz nakusema kuwa huu ni muendelezo wa projrct ya kampuni yake kudili na movie za watoto toka Rj na lengo likiwa ni kuinua vipaji vichanga ili kukuza sanaa yetu ya tanzania kimataifa zaidi alisema johari.ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Rj company
Chanzo: Tanzania one blog

WEMA: ''BABA NAYE YUMO MTANDAONI, MMEMWONA?''



  Wema akiwa na mzee Sepetu, pamoja na mtu wake wa karibu
Hii imetokea kupitia mtandao wa Instagram, Wema aliamua kutupia picha akiwa na baba yake mzazi, mzee Sepetu, huku pembeni akiwepo mtu wake wa karibu.

ZILIZOSOMWA ZAIDI