Akiteta jambo na baadhi ya watu!
Akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari!
Mhadhiri Maarufu wa Kiisilamu Sheikh Habibu Mazinge (suti nyeusi) akimlaki Sheikh Ponda mara baada ya kuachiwa huru.
Ponda akizungumza na waandishi wa habari.
"Kuna utaratibu umeandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu Tanzania tutawaita tutazungumza kwa pamoja lakini kikubwa ninachoweza kusema kwamba tumeshuhudia uonevu na dhulma tunayofanyiwa waisilamu nanyie ni mashuhuda hapa leo." Alisema.
Safari ikaanza!
Akaingia kwenye gari!
Msafara ukavamiwa na wafuasi baada ya dereva wa gari lake kusimamisha awasalimie wafuasi hao jambo ambalo polisi walikuwa hawalitaki na kuzua mabishano mazito lwenye mataa ya Maktaba Squire.
Wafuasi wakajimwaga barabarani!
Wafuasi wakivamia gari kumsalimia baada ya dereva wagari hilo kulisimamisha huku polisi wakimvamia aliondoe gari hilo haraka.
Waliufukuza msafara huo hadi pale ulipotokomea!
Msafara uliendelea kukimbizwa hadi walipotokomea mbali kwa spidi ya kuwakimbia.
Waumini wa dini ya Kiisilamu ambao walijitokeza kuisikiliza hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wakimbeba juu mmoja wa wafuasi wake ambao walishtakiwa pamoja mara baada ya kushinda kesi hiyo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili.
Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.
Mara baada ya kutolewa hukumu hiyo mahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1. Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya ardhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo la umiliki.
2. Upande wa Serikali haukuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4. Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
5. Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda.
Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu.
Tumewashinda!
Furaha!
Machozi yalitiririka, Jazba na ahawali zikapanda!
Safari ya kuelekea Mtambani Kinondoni Ikaanza.
Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia nduguyake kutokana na kushinda kesi hiyo.
"Pole ndio safari ya kusaka haki" Ndugu alisikika kabla ya kulia.
Wapo waliokuwa kwenye majengo ya karibu wakishuhudia!
Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari endapo lolote litatokea.
Waandishi nao walifanya mahojiano na baadhi ya washtakiwa na ndugu wa washtakiwa hao.
Ulinzi wa Ponda wakati wa kuondoka mahakamani hapo baada ya kuachiwa.
Msafara wa ulinzi ukiondoka Kisutu!
Wazee wa farasi nao walikuwepo
Thursday, May 9, 2013
KIFUNGO CHA NJE MWAKA MMOJA CHAMKABILI SHEIKH PONDA
12:17 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ZILIZOSOMWA ZAIDI
-
ZILE picha za mahaba za msanii wa Hip Hop Bongo, Nay Wa Mitego akiwa na msichana kitandani zimezua balaa kwa mama mtoto wake Siwema Eds...
-
Bondia Pacquiao amerejia nyumbani Ufilipino baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega huko Marekani ambapo pamoja na kushindwa Floyd ...
-
Walter Mguluchuma, Sumbawanga. MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Richard Tha...
-
Staa wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiingia ukumbini na kigauni kilichoacha sehemu kubwa ya kifua wazi. MASTAA wawili Bongo wali...
0 comments:
Post a Comment