Friday, October 30, 2015

MUIGIZAJI MOHAMED MWIKONGI 'FRANK' AFUNGUKA KUKOSA KITI CHA UBUNGE SEGEREA

Msanii wa filamu za kibongo Mohamed Mwikongi ‘Frank’
Baada ya wasanii mbalimbali kujitokea katika kingang’anyiro cha kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu na baadhi yao kufanikiwa kutwaa nafasi hizo na wengine kukosa, Frank afunguka kukosa kwake.
Msanii huyo wa filamu nchini Tanzania, Mohamed Mwikongi ‘Frank’, alijitokeza kugombea Ubunge jimbo la Tabata Segerea, kupitia tiketi ya ACT-Wazalendo lakini kutokana na kura zake kuwa chache hakufanikiwa kuwa mshindi wa jimbo hilo.
Amesema kuwa alikuwa mgombe ubunge jimbo la Segerea kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, ingawaje hakuwa mshindi lakini ana imani wananchi wa Segerea, wamempokea vizuri mshindi Bonnah Kaluwa na kudai kuwa hata yeye amekubali matokeo hayo.
Amedai kuwa bado anaona kuwa ana deni kwa wananchi waliompigia kura kama wawakilishi wa wana Segerea, hivyo kuna baadhi ya mambo yaliyo ndani ya  uwezo wake atayafanya kwa wananchi wake.
Ameongeza kuwa kulikuwa na changamoto nyingi, ingawa anajipanga upya mwaka 2020 kugombea tena Ili kuweza kusaidi matatizo kama tatizo la maji, ujasiriamali, ajira, michezo na Afya

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI