Wednesday, May 29, 2013

BINGWA WA FREESTYLE, ALBERT MANGWEAR ALIVYOZIMA GHAFLA


IKIWA ni siku nyingine tena ambapo taifa hili limekuwa likizidi kupoteza wanamuziki na wasanii wengine wa sanaa mbalimbali, lakini leo majonzi yamewakuta wapenzi wa muziki wa kizazi kipya Almaarufu BONGO FLEVA kwani rapper maarufu ALBERT KENETH MANGWEHA alilipotiwa kufariki dunia huko Afrika Kusini, katika hospital ya St. Hellen huku chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika vizuri.
 
 kijana huyu mwenye asili ya mkoa wa ruvuma, akiwa pia ni mzaliwa wa mkoa wa mbeya mnamo tarehe 16 mwezi wa 11 mwaka 1982 alikua ni mtoto wa mwisho katika familia yao ambaye alipata elimu yake ya msingi huko Dodoma, shule ya msingi Mlimwa na kusoma Shule ya Sekondari na Chuo cha Ufundi Mazengo Mjini Dodoma.
Marehemu Abert Mangwea enzi za Uhai wake
Amefanya nyimbo nyingi ambazo zimepelekea umaarufu wake kama: Kama ni demu Sikiliza akiwa na Lady Jay Dee, Mikasi aliyoifanya chini ya Ludigo na nyingine nyingi zilizokuwa katika album ya Mimi.
Marehemu Albert Mangwea (Kushoto) enzi za uhai wake  akiwa na TID
Wasanii wengi sana wameahirisha show walizokuwa wanatarajia kuzifanya ikiwa ni kuonyesha umoja wao na kuwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi walichonacho, wasanii hao ni pamoja na mwanadada Lady Jay dee, Kikosi cha Mizinga, TID, MwanaFA, Izzo Bussiness.nk 
 
Mungu ailaze roho ya Marehemu, pema peponi.. Ameeen!

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI