Thursday, August 14, 2014

ANGALIA PICHA ZAIDI ZA LORI LILOANGUKA KIMARA

Lori la mafuta baada ya kuanguka.
Foleni iliyosababishwa na ajali hiyo eneo la Kimara, Dar.
Polisi wakidumisha ulinzi eneo la ajali.
LORI lililokuwa na shehena ya mafuta lita 34,000 likitoka jijini Dar es Salaam kuelekea mikoani Singida limeanguka asubuhi hii eneo la Kimara Darajani, Dar na kusababisha foleni kubwa baada ya kuziba barabara huku wananchi wakiamua kuchota mafuta kutoka kwenye lori hilo ambalo ni mali ya Nassor Filling Station. 
Jeshi la Polisi liliamua kuingilia kati kuwatawanya wananchi hao waliokuwa wakigombea kuchota mafuta eneo la ajali.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI