Tuesday, April 29, 2014

YALIYOJIRI BARCELONA KWENYE MISA YA MAZISHI YA KUMUAGA MPEDWA WAO TITO VILANOVA

 Kutoka kushoto, Victor Valdes, Carles Puyol, Xavi na Andres Iniesta wakiwa katika ibada ya kuuaga mwili wa Tito VilanovaSKWADI zima la Barcelona usiku wa jana limeuaga mwili wa aliyekuwa kocha wao, Tito Vilanova kabla ya mazishi yake. Wachezaji wa kikosi cha kwanza walihudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu katika kanisa la Cathedral mjini Barcelona na kutoa heshima zao za mwisho kwa Vilanova, aliyefariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 45 baada ya kusumbuliwa na maradhi saratani. 
Mkewe na watoto wao wawili wa kike pia walihudhuria pamoja na mtoto wao kiume, Adria, anayechezea akademi ya Barca, na binti yake Carlota, alilia sana.
Dani Alves (kushoto) na Neymar kulia
Lionel Messi alikuwepo pia kumuaga Vilanova
Pumzika kwa amani: Tito Vilanova amefariki akiwa kijana wa miaka 45
Ibada hiyo iliongozwa na Mchungaji wa Barcelona, Lluis Martinez Sistach. 
Marais wa zamani wakiwemo Joan Laporta na Sandro Rosell walikuwepo kanisani, pamoja na Wajumbe wa bodi walioongozwa na Rais wa sasa, Josep Maria Bartomeu. 
"Leo tunamuaga mpendwa wetu,"alisema Bartomeu. "Nakuahidi, daima atadumu katika mioyo yetu na hatutamsahau milele,"aliongeza. 
Kwaheri: Gerardo Martino (kushoto) na Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu pia walikuwepo 
Waombolezaji mbalimbali wakiwa kanisani jana
Kipa wa Barca, Victor Valdes akiwasili na 'magongo' yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti aliloumia

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI