Saturday, March 5, 2016

KILA MTU ANA WAJIBU WA KUBRAND MALI ASILI ZETU ZISIPOTEE

HARAKATI katika mitandao ya kijamii zimekuwa zikionekana sana tangu wiki iliyopita baada ya msanii Witnesz a.k.a Kibonge Mwepesi kuanzisha kampeni ya utunzaji wa Mali asili zetu nchini zisipotee.

Akiongea na XXL ya Clouds Fm, Witness amesema, ''Kubrand maliasili zetu ni jukumu la kila mtanzania na siyo kwa serikali peke yake, nchi nyingine wananchi wake wanajitahidi kutangaza mali asili zao mpaka wanapitiliza mipaka kwa kuiongopea dunia kwa kusema baadhi ya vitu vyetu vipo nchini kwao.''

Sakata hili la kutangaza mali asili za Tanzania limekuja juu baada ya kuonekana kipande cha video ikimuonesha mwanadada aliyejulikana kama Rosemary Odinga ambaye ni mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya akisema kuwa Olduvai George ipo nchini Kenya.

Lakini pia mtandao mmoja wa habari ambao ulisha wahi kuandika kuhusu nyimbo ya ushirikiano ya msanii Diamond na AKA na kusema kuwa Diamond Platnumz ni msanii toka Kenya.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI