Tuesday, November 22, 2016

CLEMENT SANGA ATHIBITISHA MZAMBIA GEORGE LWANDAMINA NDIYE KOCHA MPYA

MAKAMU mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga amethibitisha kuwa Mzambia George Lwandamina ndiye kocha mpya wa timu hiyo akichukua mikoba ya Mholanzi,Hans Van Pluijm.
Lwandamina,53,ambaye alikuwa ni kocha wa Zesco United ya Zambia, ataanza kukinoa rasmi kikosi hicho cha jangwani katika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara.
Pia Sanga amesema kuwa Hans Van Pluijm ataendelea kuwa klabuni hapo kama Mkurugenzi wa benchi la Ufundi na kocha msaidizi Juma Mwambusi ataendelea kuwa katika nafasi hiyo mpaka itakapotangazwa vingine.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI