Tuesday, November 22, 2016

CHIKUNE WA NAMIBIA AMTAJA MSANII WA BONGO FLEVA ALIYEFANYA NAYE KOLABO

MSANII Chikune kutoka Namibia amethibitisha kufanya kolabo na msanii wa Bongo Fleva.
Muimbaji huyo ambaye amefanikiwa kushinda tuzo ya Afrimma mwaka huu ameiambia Bongo5 kuwa tayari ameshafanya kolabo na msanii mmoja wa kike kutoka Tanzania ambaye anatarajia kupata connection za huku.
“Kwa kuanzia nimeshafanya kolabo na Kleyah. Ni msanii wa pekee sana na anaangalia zaidi biashara na naamini ana nafasi kubwa ya kwenda sambamba kwenye tasnia ya muziki iliyotawaliwa na wanaume. Lakini pia tumeweza kuunganisha elimu kwa pamoja,” amesema Chikune.
Chikune ameongeza kuwa ana mipango ya miaka mitatu mbele ya kuitangaza brand yake Afrika na kuufanya muziki wa Namibia kujulikana zaidi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI