Friday, November 25, 2016

RAIS MAGUFULI - 'WATU KIBAO WAMEKIMBIA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI'

Na Emmy Mwaipopo
RAIS Dkt John Pombe Magufuli amesema zoezi la uhakiki wa vyeti litaendelea nchini na kudai kuwa wakati limeanza wengi walikimbia.
Dkt Magufuli aliyasema hayo jana wakati wa Mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) yaliyofanyika Kampasi Kuu iliyopo Bungo, wilayani Kibaha, Pwani.
“Wakubwa wenu wa section kule ambapo mnapangiwa kazi wahakikishe wanawapa promosheni mara moja kwasababu kama ni elimu mmeshapata wasiwatafutie visingizio. Nyinyi mmetoka, wapo watu kule hawana hata vyeti na ndiyo maana tulipoanza zoezi la ukaguzi wengine walichukua malikizo ya moja kwa moja,” alisema.
“Nilitegemea watachukua likizo ya kuja kusoma wamepotea, na zoezi hili la kukagua vyeti lazima liendelee ili wasomi kama nyie mliosotea elimu yenu mkafaidi matunda ya elimu yenu,” aliwapa moyo.
“Haiwezekani wewe uliyesoma hapa unakwenda mtu anayekuongoza kumbe ni kilaza hana chochote, kwahiyo ndiyo maana nawapongeza sana wahitimu. Mmefanya kitu kizuri, mmeamua vizuri na serikali itahakikisha inawasimamia kuhakikisha mnakwenda vizuri na hiki ndicho tunachokitaka.”
“Tunataka mtu kama una elimu yako ya form four sema mimi ni form four kama ni form six sema ni form six, kama ni graduate sema ni graduate sio kwamba udanganye kwa mavyeti ya kuprin, nenda na wewe ukasome ukaone shida yake.”

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI