Tuesday, November 22, 2016

MAUA SAMA - 'KUONDOKA KWA RUBY HAKUJAIUA PROJECT YA BUTTERFLY'

MAUA SAMA amedai kuwa licha ya kuondoka kwa Ruby THT, kundi lao la Butterfly halijafa.
Maua ametoa taarifa hizo kupitia kipindi cha Vibe la Kitaa cha ABM Radio ya Dodoma kinachoendeshwa na Dj Rodger. Amedai kuwa kwa sasa kila member anafanya kazi zake za solo na amesema hivi karibuni kulikuwa na mambo mengi ikiwemo Fiesta.
“Project bado ipo hai na inaendelea na wakati wa msimu wa Fiesta tulikuwa tunaendelea kuipa promo kama kawaida na kulikuwa kuna project ya Kipepeo ambayo tulikuwa tunatembea kila shule katika mikoa tuliyopita kwenye Fiesta kwaajili ya kuwahiza wanafunzi ,” amesema Maua.
“Kwahiyo haimaanishi kuwa sababu Ruby ameondoka THT basi na project ya Butterfly imekufa, hiyo sio kweli,” amesisitiza.

Kundi hilo sasa limebakiwa na Maua, Nandy na Alice.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI