Friday, November 25, 2016

CALISAH - 'NIPO TAYARI KUFUNGWA ENDAPO ITAJULIKANA NILISAMBAZA VIDEO YA KIMAHABA NA WEMA SEPETU'

CALISAH ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali katika kipindi cha Weekend Gossip kinachorushwa na kituo cha runinga cha TV1 siku ya jumamosi (19 Nov, 2016).
Katika kipindi hicho kinachoruka hewani kila jumamosi saa 3:30 usiku, mtangazaji Mimi Mars alimuuliza kuhusu mkanda wa video uliosambaa unaomuonesha akiwa katika wimbi zito la mahaba na mwanadada huyo maarufu nchini wakinyonyana ndimi.

''We do have pictures me and her, and those pictures nilikuanazo mimi na yeye, only two of us, kwahiyo isingekuwa rahisi wema kama wema kuleak zile picha'' alisema.

Calisah akaendelea kwa kusema kuwa yeye mwenyewe pia hakuvujisha kwa makusudi zile picha kama inavyosemekana na watu wengi.
''Mimi pia sijaleak zile picha na hamna mtu yeyote niliyemuachia simu yangu''

Calisah akaenda mbali zaidi kwa kusema yupo tayari kufungwa endapo itabainika kuwa yeye ndiye aliyesambaza picha na mkanda huo wa video.

Msikilize Calisah akihojiwa hapo chini kisha tupe maoni yako kuhusu sakata hili.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI