Monday, October 6, 2014

MUONGOZAJI WA FILAMU NCHINI INDIA HOMI ADAJANIA AMUUNGA MKONO DEEPIKA PADUKONE

MUONGOZAJI wa filamu nchini India Homi Adajania amesema kuwa anamuunga mkono muigizaji wa filamu nchini humo Deepika Padukone  kupinga kitendo cha gazeti la Time of India kutoa picha ambayo ilionesha kifua chake.

Picha hiyo inayoonesha wazi sehemu za juu za kifua cha muigizaji huyo ilizua mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii mwezi uliopita.
Muongozaji wa filamu
Muongozaji huyu wa filamu maarufu nchini India ya Cockatil amesema kuwa, vyombo vya habari vinatakiwa kutambua kuwa mtu maarufu kama Deepika ni binadamu kama wengine hivyo anahitaji kuheshimiwa pia.
Anasema kuwa kitendo kilichofanywa na gazeti la The time of india si cha kiungwana na kwamba yupo sahihi kusimamia na kuamua kile anachohitaji katika maisha yake.
Mwezi uliopita gazeti maarufu nchini India iliweka sehemu ya video ya zamani ya muigizaji huyo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter iliyokuwa ikionesha uwazi katika sehemu ya juu ya kifua cha Deepika na kusindikizwa na maneno ambayo hayakupendezwa na muigizaji huyo.

Katika kuonesha kuchukizwa na maneno hayo, Muigizaji huyo alijibu kupitia mtandao huo na kuungwa mkono na watu mbalimbali nchini humo kwa kuongozwa na kaulimbiu inayosema  #IStandWithDeepikaPadukone trending kuwa ni kinyume na utaratibu na tamaduni za Kihindi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI