Mwanariadha Haile Gebrselassie
MWANARIADHA nyota wa Ethiopia Haile Gebrselassie ameshindwa kutetea rekodi yake ya mkimbiaji bora aliyevunja rekodi tangu kuanzishwa kwa mashindano haya, kwa kushindwa kutamba katika mashindano yaliyofanyika jana jijini Glassgrow Scotland yakiwa ni nusu marathoni.
Mwanariadha Haile Gebrselassie
Gebrselassie ambaye ni bingwa wa zamani wa Olympic katika mita 10,000 alipatwa na tatizo la kushindwa kupumua mara baada ya kuanza mbio hizo hivyo kulazimika kutoendelea na shindano la jana.
Mashindano haya yalishuhudia mkimbiaji Stephen Mokoka kutoka nchini Afrika kusini akishinda kwa kuibuka bingwa akitumia muda wa saa moja, dakika moja na sekunde 25 katika mbio za nusu Marathoni.
Mkenya Edna Kiplagat alishinda kwa upande wa wanawake kwa kutumia saa moja dakika 7 na sekunde 57 huku mshindi wa mwaka 2013 msikochi Susan Partridge akishindwa kutamba baada ya kushika nafasi ya tano.
Gebrselassie alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume katika mashindano ya mwaka jana akivunja rekodi ya dunia kwa kutumia dakika 61 na sekunde tisa katika mashindano hayo tangu kuanzishwa kwake.
0 comments:
Post a Comment