WAKATI tukimaliza mwaka 2014, wengi tunakumbuka matukio mbalimbali ya kusikitisha na machache ya kufurahisha, kama Watanzania tunapaswa kufurahia na kuwasapoti mastaa wachache waliofanikiwa kututangaza kimataifa kupitia fani na kazi zao. Wafuatao ni miongoni mwa mastaa hao:
Diamond Platnumz
Jamaa kupitia nyimbo zake amefanikiwa kutwaa tuzo tano za kimataifa kiasi cha kuitangaza nchi yake ndani na nje ya bara la Afrika. Tuzo hizo ni pamoja na tatu za Channel O Africa Music Awards (CHOAMVA) alizozitwaa huko Sauzi kupitia wimbo wake wa ‘My Number One’ aliofanya kolabo na mwanamuziki wa Nigeria, Davido. Tuzo ni tuzo za Future Music Awards ya Nigeria na nyingine ni Reggae & World Music Awards aliyoipata nchini Marekani.
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Mheshimiwa rais anafunga listi ya mastaa waliotutoa kimasomaso nchini baada ya kupokea tuzo ya uongozi bora Afrika kutoka nchini Marekani, ambako aliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Rais alitunukiwa tuzo hiyo kufuatia mchango mkubwa alioutoa kwa maendeleo ya Tanzania na Bara la Afrika kwa jumla.
Idris Sultan
Jamaa hakuwa na jina sana, lakini taratibu alianza kupata umaarufu baada ya kuingia katika mashindano ya Big Brother Africa 2014 ambapo mwishowe aliibuka mshindi wa mashindano hayo akiwapiku washiriki wenzake wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Idris aliyejizolea kitita cha shilingi milioni 510 ameingia katika listi ya mastaa waliotutoa kimasomaso mwaka huu baada ya mara kadhaa akiwa ndani ya jumba hilo kuonesha uzalendo wake wa dhati kwa nchi yake kiasi cha wengi kuitambua Tanzania.
Happiness Watimanywa.
Ni Miss Tanzania 2013 ambaye alituwakilisha kwenye mashindano ya dunia yaliyofanyika mwaka huu Afrika Kusini. Pamoja na kutoshinda taji hilo, Happiness anaingia katika listi ya mastaa waliotupatia sifa Watanzania baada ya kufikia hatua ya kushiriki shindano hilo bila kupata sapoti yoyote kutoka Kamati ya Miss Tanzania.
Mbali na kujitoa huko miss huyo anatajwa kama mrembo aliyekubalika sana nchini kwa kupigiwa kura nyingi zaidi na Watanzania kupitia mitandao ya kijamii.
Dk. Reginald Mengi
Ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP. Kupitia biashara na makampuni yake amepata Tuzo ya Mafanikio ya Kutukuka, Africa Business Leadership Awards (ABBLA) iliyotolewa nchini Afrika Kusini ikiwa ni baada ya kufanya vyema katika kutekeleza maono ya kibiashara katika Bara la Afrika na kuonesha ujasiri katika kuwezesha mafanikio.
Timothy Conrad
Muongozaji huyu wa filamu Bongo kupitia Kampuni ya Timamu African Media, ameshinda Tuzo ya Mashindano ya Silicon Valley African Film Awards zilizotolewa nchini Marekani kupitia filamu aliyoiongoza ya Dogo Masai. Timothy alishinda tuzo hiyo kupitia kipengele cha Filamu Bora ya Afrika.
0 comments:
Post a Comment