KATIKA vitu ambavyo wanadamu wengi wa karne hii hukumbana navyo ni suala la maadili ya kazi kuporomoka kwa kiasi kikubwa.
Sio kama mambo haya ni mapya…hapana toka enzi na enzi mambo haya yamekuwepo lakini kwa sasa kusema ukweli yamezidi.
Na hi si kwa manesi na madokta tu, bali ni kwa huduma na kada mbali mbali kama vile; Waandishi wa habari, wanasheria, watumishi wa umma katika sekta mbali mbali n.k.
kuliangalia hili kwa sura mbali mbali ndipo nikaamua kuangalia katika bronchure ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania KUFANYA KILICHO SAHIHI…
Nikaona nikuchekie vipengele vichache tu kuhusu maadili kazini, kwa watumishi wa Umma lakini pia watumishi wa mashirika binafsi wanahusika.
Hebu nawe visome, uvielewe na utoe maoni yako hapo chini:
Kuzingatia utaalamu maana yake ni nini?
Kuzingatia utaalamu maana yake ni kutoa huduma kwa viwango vya juu kabisa kwa:
*Kutoa huduma bora
*Kufanya kazi kwa bidii
*Kutokuwa na upendeleo wakati wa kuwahudumia watu *Kutumia taarifa za kazi ipasavyo.
Kuwa Mwaminifu maana yake ni nini?
Kuwa mwaminifu maana yake ni kuitunza na kuitumia ipasavyo amana uliyopewa. Mtumishi mwaminifu hutambuliwa kutokana na matendo yake:
Kwa kufanya kazi kwa uadilifu.
Uadilifu maana yake ni nini?
Uadilifu ni uwezo wa mtumishi kuwa na maadili kama vile kuzingatia taaluma, kuwa mwaminifu na kuwa mwajibikaji. Haya yote hukufanya uwe mtumishi mwadilifu.
Maadili ni nini?
Maadili ni mwenendo mwema, ni vile anavyofanya mtumishi mwaadilifu, ni kufanya kilicho sahihi.
Mtumishi mwadilifu, hazungumzii kinadharia tu kuhusu maadili kama kuzingatia taaluma, kuwa mwaminifu
na kuwa mwajibikaji, bali hutenda.
na kuwa mwajibikaji, bali hutenda.
0 comments:
Post a Comment