Aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.
RAIS
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, leo amemfuta kazi Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar, Othman Masoud Othman na nafasi yake kuchukuliwa na Said Hassan Said.
Rais Shein amefanya uteuzi huo wa Mwanasheria Mkuu
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya
Kifungu 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.
Mhe. Said Hassan Said ameteuliwa kuwa Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar na uteuzi huo umeaza rasmi leo 7, Oktoba 2014.
Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Said Hassan Said alikuwa
Naibu Mwanasheria Mkuu.
Uteuzi wa Mhe. Othman Masoud Othman umefutwa kwa
mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na
kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.
0 comments:
Post a Comment