Monday, July 11, 2016

''MAFANIKIO YA MSANII NI KIPAJI CHAKE KUSAIDIA JAMII'' - PROF. JAY

Professo-Jay
MBUNGE wa Mikumi na msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amesema mafanikio kwa msanii siyo kumiliki mali nyingi bali ni jamii kuweza kunufaika kutokana na kipaji chake.
Akiongea na Dj Niko Track kwenye kipindi cha Dj Show cha Radio One, Professor Jay alisema kuwa mafanikio ni kitu kile kinachoonekana na kuleta tija na maendeleao kwa watu, lakini pia yanaweza kugawanyika kwa watu wengine siyo ya kwako peke yako.
“Wasanii waliofanikiwa majina yao yanaweza yakatumika kama alama ili kuinufaisha jamii. Wasanii kama Lady Jaydee, Professor, Juma Nature ni wasanii ambao kwa talent zao walizokuwa nazo zimekuwa manufaa kwa wengine. Kama Lady Jaydee amekuwa icon kwa wakina mama ambao wamekuwa strong kuweza kusimama pale. Mafanikio siyo kuwa na nyumba wala gari hapana, talent yangu imesaidia nini jamii yangu,” alisema Professor.
Kama Professa unakuta ana ‘Professor Foundation’ ambayo inasaidia hata wasiokuwa wanamuziki wananufaika kwa kidogo ninachokirudisha kwenye jamii. Wale wote wenye mafanikio ni wale wanaoweza kushare na kuruidisha kidogo walichokuwa nacho kwenye jamii,” aliongeza.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI