Sunday, November 8, 2015

MBUNGE PROF. JAY KUENDELEA NA MUZIKI BAADA YA KUPATA UBUNGE

Prof. Jay (Kulia) akiwa na Mbunge wa Mbeya mjini 'Sugu'.
Mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule aka Professor J, amesema baada ya kushinda kiti cha ubunge atafanya muziki wake kwa ufanisi kushinda kipindi cha nyuma.
Jay amesema umefika wakati wa yeye kufanya collabo na wasanii wakubwa. “Naendelea kufanya sanaa yangu na huenda nikaifanya kwa ufanisi mkubwa zaidi,” Jay aliiambia East Africa Radio wiki iliyopita.

“Unaweza ukasikia watanzania wanafanya kazi na akina Eminem na Jay Z, kwahiyo nategemea kufanya kwa next level kwa sababu naamini exposure nitakayoipata watu wategemee vitu vizuri zaidi. Nitafungua milango, kwenye muziki wa Bongo Flava tunaenda kufungua ukurasa mwingine kwa ajili ya watanzania.”

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI