Sunday, November 8, 2015

LEMBELI AKANUSHA KUMILIKI MTANDAO WA TWITTER UNAOISHAMBULIA SERIKALI YA RAIS MAGUFULI

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama mkoani Shinyanga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Radio Kahama FM, James Lembeli amekanusha kumiliki akaunti ya mtandao wa Twitter ambayo imekuwa ikitumiwa na watu wenye nia  mbaya na yeye kutoa taarifa za uchochezi na uchonganishi.

Lembeli amesema taarifa zote zinazotolewa kupitia akaunti hiyo yenye jina la "James Lembeli" na picha yake akiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema kupitia mwavuli wa UKAWA Edward Lowassa ni za uongo.

HUU HAPA CHINI NI UJUMBEA UJUMBE ULIOTUMWA JANA KWENYE AKAUNTI HIYO INAYOTUMIA JINA LA JAMES LEMBELI.
Amewataka watu wanaoguswa na taarifa hizo kuzipuuza, huku akiwaonya waliofungua akaunti hiyo waache mara moja na kwamba akiwabaini atawashitaki kwa mujibu wa sheria.

Lembeli ameliomba jeshi la polisi kupitia kitengo cha Intelligensia kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mitandao kumsaka mtu aliyefungua akaunti hiyo na kumtia nguvuni.


Hata hivyo Lembeli amesema hajawahi kujiunga na mtandao wowote wa kijamii ikiwemo wa Twitter na wala hana mpango wa kujiunga na mitandao hiyo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI