Sunday, October 4, 2015

MAPACHA 5 WAZALIWA NCHINI MAREKANI!! *PICHAZ*

Bi. Danielle Busby akifurahi kuwaona wanawe baada ya kujifungua mapacha watano wote wakiwa hai.
Wakunga wakiwatazama watoto waliozaliwa.
Mmoja kati ya watoto hao akiwa kwenye mtambo maalum wa kumsaidia kupumua kwakuwa watoto hao wamezaliwa kabla ya miezi tisa kutimia.
Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Danielle Busby amejifungua mapacha watano wote wakiwa ni jinsi ya kike katika hospitali moja ya wanawake mjini Texas nchini Marekani. Wauguzi katika hospitali hiyo wamesema kuwa, uzazi huo kutokana na mimba moja ni rekodi mpya ambayo haijawahi kutokea Marekani.
Danielle ambaye ndiye mama wa watoto hao ambao amewapa majina ya Olivia Marie, Ava Lane, Hazel Grace, Parker Kate na Riley Paige amesema kupata watoto hao wote wakiwa wazima kwake ni baraka ya hali ya juu. Inasemekana watoto wengi sawa na hao waliwahi kuzaliwa mara moja huko London Uingereza, mwaka 1969 katika hospitali ya Queen Charlotte.
Zaidi ya Madaktari na wauguzi 12 walilazimika kufanya kazi ya ziada ilikumsaidia Bi. Danielle kujifungua watoto hao ambao hawakuwa wametimiza umri wa miezi tisa tumboni kwa njia ya upasuaji.

Baba wa Danielle huyo, Adam Busby amewamiminia sifa kedede na kuwashukuru wahudumu wote wa hospitali hiyo waliofanikisha operesheni ya mwanaye hadi kujifungua watoto hao watano.
Taarifa Zaidi zinasema kuwa, Bi. Busby alikuwa na tatizo la kupata ujauzito hivyo akatumia mbegu pandikizi ya uzazi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI