Tuesday, October 6, 2015

KAULI YA NAPE NNAUYE BAADA YA KINGUNGE KUJIVUA UANACHAMA WA CCM

Katibu  wa  Itikadi na Uenezi wa chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema  chama  chake kimepata unafuu mkubwa baada ya kuondoka kwa kada wake mkongwe, Kingunge Ngombare Mwiru, ambaye juzi alitangaza kuachana na chama hicho, akitoa sababu kuwa taasisi hiyo aliyoshiriki kuijenga, imekiuka katiba yake.

Akizungumza mara tu baada ya Kingunge kutangaza azma yake hiyo katika mkutano na waandishi wa habari juzi uliofanyika nyumbani kwake maeneo ya Victoria, jijini Dar es Salaam, Nape alisema wanamtakia kila la kheri huko aendako, kwani uwepo wake ulikuwa ukikigawa chama.

Alisema akiwa kama mzee wa chama, kitendo chake cha kuegemea kwa mgombea mmoja wa urais, kiliwagawa wanachama na kauli zake za mara kwa mara kupinga maamuzi ya chama, yaliwafanya wanachama wake kugawanyika, jambo ambalo lilimfanya ageuke kuwa mzigo, ambao haukubebeka.

“Mara zote tulishindwa kujibu kauli za kushangaza za mzee Kingunge kwa sababu, tuliogopa kujiabisha kama chama, lakini maadam ameondoka, sasa tutakuwa tayari kumjibu kwa matamshi yoyote atakayotoa dhidi ya chama, sasa tutakuwa imara zaidi kuliko awali,” alisema Nape.

Katika mkutano wake na wanahabari, licha ya madai yake ya chama hicho kukiuka katika yake, lakini pia alisema lipo hitaji kubwa la mabadiliko linalotakiwa na vijana, hivyo kwa kutambua jambo hilo, ameamua kuwa bega kwa bega na vijana hao katika kutaka mabadiliko.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI