Friday, October 30, 2015

KANYE WEST AGEUKA KITUKO KWA GEORGE BUSH

Siku chache zimepita tangu tangu mwanamuziki na mwanamitindo nchini Marekani, kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais nchini humo, imeonekana kuwa kichekesho kwa baadhi ya watu.
Inadaiwa kuwa Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush, ameangua kicheko kutokana na wazo la rapa Kanye West, kuwania urais wa Marekani mwaka 2020.
Inadaiwa kuwa Bush, alikuwa akitoka kwenye mlo wa usiku Jijini Washington DC, ambapo alisimama kusaini picha kadhaa walizokuwa nazo watu na ndipo mpiga picha mmoja alipomuuliza juu hatma ya kisiasa ya Kanye.
Taarifa zinadai kuwa Rais huyo wa zamani wa Marekani, alionekana kukwepa kujibu swali la mpigapicha huyo na badala yake aliangua kicheko kwa mara mbili.
Sambamba na hilo rais Obama, alimtaka Kanye, kutumia muda mwingi kufanya maamuzi kwa sababu kuna watu wengi ambao wana tabia za ajabu hivyo anapaswa kukabaliana nao ili aweze kumudu nafasi yake.Hata hivyo siku za nyuma rais Obama, alishangazwa na uamuzi wa Kanye West kuwania nafasi hiyo na pia hakuwa na kikubwa cha kumshauri kuhusu uamuzi wake huo.
Pia alimuuliza kama anafikiri tena Wamarekani watampa Mmarekani mweusi nafasi ya kuwaongoza kama ilivyokuwa kwake.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI