Friday, April 3, 2015

WAZIRI WA FEDHA AWABAINI WAKWEPA KODI BAADA YA KUFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARI KAVU*PICHAZ*

BAADHI ya wafanyabiashara wabainika kukwepa kulipa kodi kwa kuingiza bidhaa kutoka nje kupitia bandari ya Dar es Salaam, ambapo huandikisha taarifa na maelezo tofauti na bidhaa halisi zilizomo ndani ya makontena ili kuwawezesha kukwepa kodi kwa kulipia kiasi kidogo.
Kutokana na udanganyifu huo, Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya alifanya ziara ya kushtukiza katika bandari kavu Karibu na BP Kurasini jijini Dar es Salaam na kubaini kuwepo kwa makontena nane yenye bidhaa tofauti na zilizoandikishwa kwenye nyaraka.
Bidhaa zilizokutwa kwenye makontena hayo ni pamoja na Vitenge pamoja na  Vifaa vya  kutengenezea pikipiki.
Mhe. Waziri wa fedha vilevile alifanya mshtukizo huo kwa siku mbili ambapo siku ya pili alishtukiza bandari kavu ambayo ni TRH iliyoko kurasini.
Huko aligundua kuwa waliweka Luninga na Biskuti katika makontena yenye ukubwa wa futi 40 kila moja.
Waziri wa Fedha Mhe Saada Mkuya, akiwasili katika bandari kavu ya Tanzania Road Haulage (TRH) Kurasini jijini Dar es Salaam, akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tiagi Kabisi pamoja na waandishi wa habari.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile, Msaidizi wa Waziri Bw. Thomas Mabeba, Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Tiagi Kabisi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma wakisikiliza kwa makini ufafanuzi  wa nyaraka za makontena hayo.
Waziri  wa Fedha Mhe. Saada Mkuya akishuhudia kilichomo ndani ya moja ya makontena mara baada ya kufunguliwa.
Watumishi wakikagua kilichomo ndani ya maboksi yaliyotolewa kwenye kontena.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano Mamlaka ya Mapato Tanzania  Bw. Richard Kayombo.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya akipata ufafanuzi kutoka kwa Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Tiagi Kabisi kuhusiana na kontena hilo lenye biskuti.
Wafanyakazi wa TRH wakishusha biskuti za maziwa katika kontena.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya akiongea na simu katikati ya runinga zilizoshushwa katika kontena.
Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Tiagi Kabisi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
 
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiangalia kontena lenye shehena ya vitenge badala ya unga wa gypsum kama nyaraka zilivyoonyesha.
Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tiagi Kabisi, aliyeshika kitenge akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya  na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile akiangalia baadhi ya vitenge vilivyotolewa katika kontena.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  na wa  bandari kavu wakihakiki vitenge vilivyotolewa katika makontena.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya pamoja na Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Tiagi Kabisi wakipitia kwa makini nyaraka za vifaa hivyo.
Kontena lililosheheni spea za pikipiki.
Kontena lililosheheni vitenge.
#Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - HAZINA

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI