SIKU ya Boxing day ni maalum kwa watu kupeana zawadi za sikukuu ya Christmas kama ishara ya Upendo kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki, tumeona mastar mbalimbali ndani na nje ya Tz, wakiwa wamepost picha za siku hiyo katika mitandao ya kijamii wakipeana zawadi na familia zao, lakini Rappa na mwingizaji kutoka Amerika Ludacris, ameamua kutoa zawadi ambayo nitofauti na tuliloziona kwa kutangaza nia kwa mpenzi wake na kuifanya siku hiyo ya Boxing day kuwa siku muhimu katika maisha yao.
Star huyo ameamua kuitumia siku hiyo kwa kumchumbia mpenzi wake wa siku nyingi waliodumu kwenye mahusiano kwa miaka minne Eudoxie Agnan, ambaye ni Mwanafunzi anaesomea masomo ya Medical.
Ludacris aliwaalika marafiki kadhaa akiwemo Star LeToya Luckett, kutoka kundi la Destiny’s Child, na kusafiri nao kutoka Atlanta hadi Costa Rica, kwa kukodi Ndege binafsi kwa ajili ya tukio hilo muhimu katika maisha yao na kumwuliza swali kubwa mpenzi wake ‘ Will you marry me?
Bila shaka jibu ni ndiyo lakini Eudoxie Agnan, hakusema ndiyo, unajua alisemaje? Ludacris alishare picha za kutio hilo katika ukurasa wake wa Instagram na kuandika “She didn’t say yes. She said HELL YES! #milehighproposal,”
0 comments:
Post a Comment