KENYATTA amemkabidhi mamlaka kwa muda
naibu wake William Ruto kwa siku mbili atakazokuwa nje. Mahakama ya
kimataifa ya ICC, inajianda kuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa siku mbili
kuhusu kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye atakuwa rais wa kwanza aliye
mamlakani kufika mbele ya mahakama hiyo.
Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za
uhalifu dhidi ya binadamu anazodaiwa kutenda baada ya uchaguzi wa mwaka
2007.Mahakama hiyo inasama kuwa Kenyatta alihusia katika kupanga na kufadhili
ghasia za kikabila baada ya uchaguzi uliozua utata mwaka 2007/08Zaidi ya
wakenya 1,000 waliuawa kwenye gasia hizo.
Ruto ambaye ni rais kwa muda naye pia anakabiliwa na kesi
katika mahakama hiyo ya ICC
Mawakili wa Kenyatta wanasema kuwa kesi hiyo inapaswa kufutiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.
Kenyatta ameombwa na mahakama hiyo kufika mbele yake ili kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na kiongozi wa mashtaka Fatou Bensouda kwamba serikali ya Kenya imekataa kuwasilisha ushahidi unaohitajika katika kesi ya Kenyatta.
Majaji wa mahakama hiyo hata hivyo watathmini kauli kutoka kwa pande zote mbili.

Mkutano huo wa siku
mbili unatarajiwa pia kutangaza tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya
Kenyatta.
ICC imemtaka Kenyatta
kujibu madai ya upande wa mashitaka kuwa Kenya inakataa kutoa ushahidi
unaotakikana na mahakama hiyo.
Rais Kenyatta akikagua gwaride la heshima
kabla ya kuondoka nchini kuelekea Hague.
Mwezi Septemba, mahakama iliahirisha
kesi dhidi ya Kenyatta baada ya upande wa mashitaka kusema kuwa Kenya imekosa
kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.
Mashahidi wa upande
wa mashitaka wamejiondoa katika kesi hiyo.
Mamia ya wabunge wa
Kenya wanatarajiwa kuambatana na Kenyatta kama ishara ya kumuunga mkono.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment