Saturday, October 18, 2014

ANGALIA MAZOEZI YA KIJESHI - USHIRIKIANO IMARA 2014 - BURUNDI

2a
Meja Jenerali James Mwakibolwa wa nne kulia akiwa na Brigedia Jenerali Joseph Chengelela wa tano kulia na Mwambata wa JWTZ nchini Burundi kanali Venant Mutashobya wa tatu kulia mara baada ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI.
1a
Brigedia Jenerali Joseph Chengelela (kushoto)akimkabidhi bendera ya Afrika Mashariki msaidizi wa zoezi mara baada ya kukabidhiwa kutoka kwa mgeni rasmi hayupo pichani siku ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI.
jes
Picha ya Pamoja ya maofisa wa serikali ya Burundi na Maafisa Wakuu wa Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI
unnamed
Majeshi hayo yakiwa katika mazoezi.
***********
ZOEZI la Ushirikiano Imara linalojumuisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki limefunguliwa leo nchini Burundi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa chi hiyo. Gwaride maalumu linalojumuisha majeshi yote ya nchi wanachama lilikuwa limesimama mbele ya wageni mbalimbali katika uwanja wa kambi ya kijeshi ya Muzinga nje ya mji wa Bujumbura wakati Makamu huyo wa Kwanza wa Rais alipokabidhi Bendera ya jumuiya kuashiria kuanza rasmi wa mazoezi hayo.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liliwakilishwa na Meja Jenerali James Mwakibolwa ambaye ni Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita Makao Makuu ya Jeshi.
Mazoezi haya ya medani hufanyika kila mwaka katika moja ya nchi wanachama kwa utaratibu wa kupokezana yakiwa na lengo kuu la kudumisha ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama.
Pamoja na mambo mengine, mazoezi haya yatatoa fursa kwa nchi wanachama kuandaa na kuweka mikakati ya pamoja katika kukabiliana na matishio mbalimbali yanayoweza kutokea katika ukanda wetu wa afrika mashariki.
Maudhui makuu ya zoezi la mwaka huu yanajikita katika kukabiliana na changamoto katika ulinzi wa amani, majanga ya asili na ya kibinadamu, ugaidi, pamoja na uharamia ambavyo vimekuwa tishio katika maeneo mengi duniani.
Aidha, kutakuwa na mazoezi ya kuyaweka tayari majeshi yetu katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ili kupunguza na kuzuia kabisa madhara ya magonjwa hayo. 
kwa ujumla, mazoezi haya ni kipimo cha jinsi gani nchi yetu imejiandaa na kujiweka tayari kupambana na changamoto hizi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na jumuiya.
JWTZ limejiadaa vyema katika ushiriki likishirikisha waajeshi wa fai malimali ili kutimiza malengo ya nchi yetu na jumuiya kwa ujumla katika kukabiliana na changamoto zilizotajwa.
Aidha, kikosi cha Tanzania kupitia kitengo cha Uhusiano na Raia (Civil Military Cooperation) kimepanga kutoa misaada mbalimbali kwa wananchi wa Burundi waishio maeneo ya karibu na kambi ikiwa ni pamoja na vifaa kwa ajili ya wanafunzi. Ikumbukwe kuwa, jeshi bora ni lile ambalo askari wake wamefunzwa vizuri na kupata mzoezi ya mara kwa mara katika kutimiza majukumu yao, mazoezi ndiyo hulifaya jeshi letu kuwa tayari wakati wote kuwatumikia wananchi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI