BAADA ya Amber Rose kuomba talaka na haki zote za mtoto wao, rapper Wiz Khalifa amefunguka kuwa anaamini mke wake alikuwa na mahusiano na mume wa Mariah Carey ‘Nick Cannon’.
Amber Rose pia amefunguka kuwa mume wake amemsaliti na wanawake wengi wakati yupo kwenye ndoa yao.
Nick Cannon ameibuka na kutangaza kuwa hajahusika na kuvunja ndoa ya Amber na Wiz Khalifa,Kwa mujibu wa Nick Cannon, mahusiano yake na Amber ni ya kazi tu. Fahamu kuwa Nick Cannon na mke wake Mariah Carey wanaelekea kutengana baada ya kutangaza talaka yao hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment