KAMA masihara vilee, Meneja wa Mwanamuziki Mirror na kaka wa hiyari wa Wema Sepetu, Petitman amemchukua jumla dada wa mwanamuziki Diamond Platnumz aitwaye Esma baada ya kufunga nae ndoa takatifu ya kiislamu Ijumaa ya Septemba 19 katika sherehe iliyohudhuriwa na ndugu wa karibu wa wanandoa hao.
”Namshukuru mungu kwa kila jambo na leo naomba nitoe tamko rasmi kuwa @esmaplatnum ndio mke wangu kipenzi nampenda sana na ndomaana nipo Nae pia nashukuru kwa team yangu @endlessfame na wote waliosupport na piaaa @martinkadinda @wemasepetu nawapenda sana na bila kisahau dada angu kipenzi na mama angu kipenzi @teddygipson namalizia kusema niko nalala….😋😋” aliandika Petitman kwenye ukurasa wake wa Instagram na kisha kuposti picha kadhaa za harusi yake.
”namshukuru sana mamaangu kwani yeye ndo kila kitu ktk maisha yangu pia nashukuru ndugu zangu wote kwa kuwa pamoja na mimi ktk hii shughuli nashukuru pia my lovely husband nampenda sana @petitman_wakuache …. tulianza km mchezo yamesemwa mengi but ndo mambo ya binadamu… pia siwezi msaahau mtu mmoja @auntyezekiel wee mwenyewe unajua… my lovely wiii @wemasepetu thank uuu @romyjons @diamondplatnumz nawapenda sana hamkuniacha nyuma mlikuwa pamoja nami… tupendane kweli kweli wabaya waulizane… nawapenda na nyie hapo mashabiki zangu 😘😘😘😘” aliandika Esma
0 comments:
Post a Comment