Friday, September 26, 2014

BARAZA LA WANAWAKE CHADEMA KUANDAMANA KWA AMANI WIKI IJAYO

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Taifa Chadema, (BAWACHA), Halima Mdee akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya azma ya baraza hilo la wanawake kufanya maandamano makubwa ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete asipokee rasimu  iliyotengenezwa na bunge maalum la katiba. mwenyekiti huyo alimesema maandamano hayo yamepangwa kufanyika katika wiki ijao hajataja siku gani lengo kubwa la maandamano ni kufikishwa ujumbe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Kikwete kuwa rasimu hiyo si ya wananchi huku akisema yatakuwa ya amani tuu.
Baadhi ya wakazi wa mji wa dodoma wakipita mbele ya uzio wa Ofisi kuu ya CCM Mkoa huku  wakisoma ujumbe ulioandikwa kwenye uzio wa CCM  wenye maandishi yanayosomeka Ufisadi no Katiba, ujumbe huo haukujulikana umeandikwa na Watu gani  katika maeneo mbalimbali mjini hapa Dodoma

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI