![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMGXdzvI-oH8zd1r-0oIYvTMakKzfnKrnowMd7L1SSqIDMfCE38qH0VFIwE6Nkg2T_H0q-H-Q5_tLa6ZRXiHHE2znQ-Wtvn2FX6cDeEmh-DaxqfcBA2AnwargA0M7hdIo0b-ChNmR7Ihm9/s400/alimazrui.jpg)
Mwakilishi wa wanachama wa Coastal Union, Salim Al Mazrui akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana.
MKUTANO
mkuu wa dharura wa wanachama kujadili kuhusu aliyekuwa Mwenyekiti wa
Coastal Union, Hemed Aurora kujiuzulu unatarajiwa kufanyika Jumapili
wiki hii kwenye ukumbi wa Makao makuu ya Klabu ya Coastal Union barabara
ya 11 jijini Tanga.
Mkutano huo unatarajiwa kuanza saa nne asubuhi utakaohusisha wanachama hai ambao wamelipia kadi zao na hawadaiwi madeni yoyote.
Akizungumza
na waandishi wa habari,Mwakilishi wa Wanachama wa Coastal Union, Salim
Al-Mazrui alisema maandalizi ya kuelekea mkutano huo yamekamilika kwa
asilimia kubwa na utakuwa na agenda mbili muhimu zitakazojadiliwa.
Al
Mazrui alisema agenda ya kwanza itakuwa ni kujadili uvumi uliojitokeza
wa kujadili kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Klabu ya Coastal
Union, Hemed Hilal Aurora.
Alisema
agenda ya pili itakuwa ni kujadili utendaji wa Makamu Mwenyekiti wa
Coastal Union, Steven Mguto ndani ya klabu hiyo hasa kuelekea msimu mpya
wa Ligi kuu Tanzania bara na kutoa maamuzi.
Mwakilishi
huyo aliwataka wanachama wa Coastal Union waliokuwa hai kuhakikisha
wanajitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wenye lango pia la kuangalia
namna ya kuipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi
kuu.
Kwa
upande wake,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alithibitisha
kupokea taarifa ya mkutano huo na hivyo utafanyika siku ya Jumapili
kutokana na wanachama hao kufuata taratibu zote.
0 comments:
Post a Comment