Wednesday, October 22, 2014

MFAHAMU MWANAHABARI ALIYEUGUA EBOLA NA KUPONA

Ashoka 
IDADI ya watu wanaoendelea kutajwa kupata tiba ya Ebola, imezidi kuongezeka, leo pia shirika la utangazaji Sky News wameripoti kuhusiana na mtu mwingine aliyepona Ebola.
Ashoka Mukpo (33), mpiga picha wa gazeti la NBC News ametajwa kuwa mmoja ya watu wachache ‘waliobahatika’ kupona Ebola.
Mwanahabari huyo alipata maambukizi hayo akiwa Liberia, amesema alipogundua ana dalili za maambukizi ya ugonjwa huo, alisafiri kurudi Marekani na baada ya kufikishwa hospitali alihudumiwa kwa kuongezewa damu kutoka kwa Dk. Kent Brantly, ambaye ni mmoja wa watu waliotibiwa ugonjwa huo na kupona nchini humo. Mukpo & Blant
Mukpo anakuwa mmoja kati ya watu 8 kutibiwa ugonjwa wa Ebola nchini Marekani, huku taarifa kuhusiana na wauguzi wawili waliopata maambukizi wakimhudumia Thomas Duncan aliyefariki kwa Ebola nchini Marekani, zinasema kuwa hali ya kiafya ya mmoja wa wauguzi hao, Nina Pham anaendelea vizuri. Marekani imeimarisha uchunguzi wa virusi vya Ebola katika maeneo ya viwanja vyake 5 vya ndege ambapo watu wanaoingia nchini humo wakitokea Afrika Magharibi, wanalazimika kupitia katika viwanja hivyo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI