Wednesday, October 22, 2014

REKODI ILIYOVUNJWA MWAKA HUU KATIKA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Klabu za Bayern Munich, Chelsea pamoja na Shakhtar Donetsk zimeweka rekodi ya kufunga mabao mengi katika nusu ya kwanza ya michezo ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Klabu hizo tatu zimefanya hivyo usiku wa kuamkia hii leo katika michezo ya mzunguuko wa tatu ambapo FC Bayern Munich walikuwa ugenini mjini Roma nchini Italia, wakipambana na AS Roma ilihali Shakhtar Donetsk walikuwa nyumbani mjini Donetsk nchini Ukraine wakicheza dhidi ya BATE Borisove huku Chelsea wakicheza nyumbani Stamford Bridge dhidi ya NK Maribor kutoka nchini Slovenia.FC Bayern Munich pamoja na Shakhtar Donetsk ziilifanikiwa kuacha vilio kwa wapinzani wao kufuatia ushindi wa mabao saba waliouvuna na kwa upande w
a Chelsea waliibuka na ushindi wa mabao sita kwa sifuri na hivyo kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kuichungulia nafasi ya kutinga katika hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya abingwa barani Ulaya msimu huu.
Katika mchezo wa FC Bayern Munich dhidi ya AS Roma mabao ya mabingwa hao kutoka nchini Ujerumani yalifungwa na Mario Goetze, Robert Lewandowski, Thomas Mueller, Xherdan Shaqiri, Franck Ribery pamoja na Arjen Robben aliyefunga mabao mawili.
Bao la AS Roma katika mchezo huo lilipachikwa wavuni na mshambuliaji kutoka nyumbani Afrika katika nchi ya Ivory Coast Gervais Yao Kouassi Gervinho.
Kwa upande wa Shakhtar Donetsk mabao yao yalifungwa na Alex Teixeira, Douglas Costa pamoja na Luiz Adriano aliyefunga mabao matano.
Chelsea mabao yao yalipachikwa wavuni na Loic Remy, Didier Drogba, John Terry pamoja na  Eden Hazard aliefumnga mabao mawili huku Mitja Viler akijifunga mwenyewe.
Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo ni kwamba
 Schalke 04    4 - 3    Sporting CP
FC Porto    2 - 1 Athletic Bilbao
APOEL Nicosia 0 - 1 Paris Saint Germain
Barcelona 3 - 1 Ajax
CSKA Moscow 2 - 2    Manchester City

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI