![Miili ya waliokufa kwa Ebola yatupwa hovyo mitaani, Liberia](http://www.timesfm.co.tz/content/uploads/2014/8/7/cache/Ebola_full.jpg)
UGONJWA wa Ebola unaendelea kuwa tishio kubwa kwa watu Afrika Magharibi huku idadi kubwa ya watu ikipoteza maisha.
Kufuatia hofu ya kuambukizwa ugonjwa huo
hatari kwa kugusa au kuwa karibu na wagonjwa au miili ya waliopoteza
maisha kwa ugonjwa huo, ndugu wa marehemu wameripotiwa kuiburuza miili
ya ndugu zao kutoka majumbani kwao na kuitupa hovyo mitaani hali
inayoongeza hatari zaidi ya maambukizi.
![](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/08/06/article-2717762-2048F81100000578-534_634x421.jpg)
Kwa mujibu wa Daily Mail, ugojwa huo
hatari unaoweza kusababisha mtu kutokwa na damu machoni, mdomoni na
masikioni umeshaua takribani watu 9,000 katika nchi za Afrika Mashariki.
Madaktari wanaohudumia wagonjwa wa Ebola
wanapata changamoto kubwa ya kukwepa maambukizi huku baadhi yao
wakiripotiwa kupata maambukizi na kupoteza maisha.
Hali ya hatari imesababisha abiria
wanaosafiri kutoka Afrika Magharibi kufanyiwa vipimo katika viwanja vya
ndege kwa hofu ya kuusambaza ugonjwa huo katika nchi wanazokwenda.
0 comments:
Post a Comment