Wednesday, July 16, 2014

WAFUASI WA CCM, CHADEMA NUSURA WAZICHAPE KAVU KAVU MKUTANO WA NAIBU WAZIRI WA MAJI, AMOS MAKALLA




 Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (kulia), akiamulia ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam.
 Wafuasi wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akihutubia na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia katika mkutano huo.
 Poilisi wakiwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada hani amezifanya binafsi kama mbunge kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema) wakitofautiana jukwaani wakati Makalla, alipoamuru Polisi kuwatoa wafuasi wa Chadema waliokuwa wakimzomea wakati akihutubia kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM kuhusu maji.
Mnyika aliwataka wafuasi wake waendelee kuzomea akidai kuwa Waziri huyo hakufanya haki.
 Mfuasi wa CCM  akiwa na bango la kumshutumu Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka, Dar es Salaam, EvaSinare (katikati) akijaribu kuunusuru mzozo huo kwa kuzungumza na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika. 
 Polisi akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na Chadema
 Mbunge wa Jimbola Kinondoni, Idd Azzan akihutubia katika mkutano huo
 Wafuasi wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia kwakueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM, ambapo aliwahakikishia wananchi wa  jiji la Dares Salaam kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao tatizo la maji litakuwa historia hasa baada ya kukamilika upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu ambao ujenzi wake umeanza sasa.
 Makalla akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi kuhusu ujenzi wa Tanki jipya la maji eneo la Kibamba, Dares Salaam, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dares Salaam na Pwani.
 Mkazi wa Kibamba, Chrisant Kibogoyo akiuliza swalikatika mkutanouliofanyika Kata ya Kibamba.
 Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kibwegere, Hellen Mshana akiuliza swali kwa waziri kwambanilini maji yatasambazwa katika shule hiyo na zinginezo.
 Askari akimuondoa mfuasi wa Chadema aliyekuwa akilazimisha kumuuliza swali Waziri Makalla katika mkutano huo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maji Safi na Taka Dares Salaam, (Dawasco), Jackson Midalla akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na Diwani wa Kata ya Kibamba, Issa Mtemvu wakati Waziri Makalla, alipotembelea mradi wa maji katika kata hiyo.
Wafuasi wa CCM  na Chadema wakishindana kupeperusha bendera za vyama vyao wakiwakwenye magari eneo la Kibamba. 
Picha zote na kamanda wa matukio.
§§§§§§§§§§§
ZIARA ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla iliingia dosari baada ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge na Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota (Chadema), kurushiana matusi mbele ya wananchi na nusura wakunjane mashati.
Tukio hilo lilitokea wakati wa mkutano wa wananchi wa Kata ya Saranga, Kimara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mavurunza ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya Makalla katika ukaguzi wa miradi maji ya Dawasco.

Vurugu hizo zilitokea baada ya Makalla kuagiza polisi kuwakamata wafuasi wa Chadema kwa madai kuwa walitaka kuvuruga mkutano huo. 
Baada ya Makalla kutoa agizo hilo, Diwani Manota na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika walisimama na kupinga uamuzi huo na walirushiana maneno na Mwenyekiti Madenge aliyesema wawili hao waache upumbavu.
“Unatetea nini? Acha upumbavu... Hatuwezi kuendesha mkutano na watu wanaofanya vurugu,” alitusi Madenge huku Manota akiwa na jazba kabla ya viongozi wengine wa kisiasa kuwatuliza.
Hata hivyo, kabla ya Makala kuzungumza, Mnyika aliyekuwa ameongozana naye katika ziara hiyo alikuwa na wakati mgumu wa kuzungumza kutokana na zomeazomea kutoka kwa wafuasi wa CCM.

Makalla alisema kosa kubwa lililosababisha kutokea kwa vurugu hizo ni maandalizi mabovu ya wafuasi wa vyama vyote.
“Wafuasi walikuwa na itikadi zao zaidi kuliko kuja kusikiliza hoja za serikali kupitia ziara. Pia labda waliwakosa uvumilivu kutokana na ahadi ya maji kuwapo kwa muda mrefu, lakini kuvurugana wanasiasa ni kukosa uvumilivu,” alisema.
Kwa upande wake, Mnyika alipendekeza ziara zote za kiserikali zisiwe na uhusiano na vyama vya kisiasa.
“Kama ingekuwa ni mambo ya kuzungumzia ilani ya chama, tangu mwaka 2005/10 ahadi ya maji ya asilimia 90 kwa Jiji la Dar es Salaam haijatekelezwa,” alisema Mnyika
>Na Mwanaharakati blog<

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI