Wednesday, November 16, 2016

JULITHA KABETE AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI KWENYE MISS AFRICA 2016 NIGERIA

MSHIRIKI wa shindano la Miss Africa 2016, Julitha Kabete (19) amekabidhiwa bendera na Waziri Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano hayo yatakayofanyika nchini Nigeria Novemba 26 mwaka huu.
Mrembo huyo alichaguliwa kutokana na shindano lililoandaliwa na kampuni tanzu ya Millen Magese Group of Companies (MMG) inayomilikiwa na Miss Tanzania 2001, Millen Magese.
Baada ya kuchaguliwa mrembo huyo kupitia mtandao wa Instagram aliandika:
Napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Kampuni ya MMG (Millen Magese Group Ltd) , Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo; Mheshimiwa Nape Nnauye, na walionivumbua Kamati ya Miss Tanzania (Asanteni SANA) . MMG wamenichagua kwenda kuiwakilisha nchi yangu Tanzania katika mashindano ya Miss Africa 2016. MMG baada kutumia usahili tuliopitia na kuchagua mrembo wa kuwakilisha katika mashindano haya ya Miss Africa. Kwahiyo nitapenda kuwashukuru sana timu nzima ya MMG; dada Millen Magese, Loveness Hoyange, Anitha Moshi, Kaka Matukio Chuma, Kebby designs, OGS studio, Devota Divas store na stylist Swalha Msabaha kufanikisha mipango yote ya safari ya kwenda Miss Africa 2016, Nigeria. Maandalizi yalikuwa ya wakati mfupi sana lakini kamati ya MMG na timu nzima niliyotaja hapo juu imehakikisha kila kitu kimeenda vizuri.
Napenda kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Nape kwa kunikabidhi Bendera ya Taifa langu Tukufu la Tanzania. Pia nitapenda kutoa shukrani kwa vyombo vya habari kusaidia kutoa ujumbe huu kwa muda mfupi tuliokuwa nao. Wananchi nawaomba ari, hamasa na hata kupigiwa kura nikiwa nchini Nigeria (www.missafrica.tv) . Ninawahaidi kupeperusha vizuri Bendera ya Tanzania vizuri na kuwa Balozi mwema wa Tanzania kwenye mashindano ya Miss Africa 2016. Asanteni SANA!

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI