Thursday, November 17, 2016

MUHONGO - 'HATUTAKI UMEME WA MGAO DAR ES SALAAM'

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo amesema kuwa watanzania wamechoka kukatika katika kwa umeme na huku akiwaambia Tanesco kuwa Watanzania wanataka umeme wa bei nafuu.
Akizungumza Jumatano hii Waziri huyo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam alisema “Hatutaki mgao wa umeme, naomba niwaeleze Tanesco hatutaki mgao wa umeme la kwanza hilo, la pili Watanzania wamechoka na kukatika katika kwa umeme, hatutaki kuona umeme unakatika katika, la tatu ili tujenge nchi ya viwanda tunahitaji umeme wa uhakika narudia umeme wa uhakika , umeme unaotabirika na wa bei nafuu,” alisema Muhongo.
Nae Mkurugenzi mkuu wa Shirika la umeme Tanzania (Tanesco), Felschimi Mramba amesema mradi huo umejengwa kwa msaada wa serikali ya Finland kwa kushirikiana serikali ya Tanzania.
“Utekelezaji wa mradi huu umehusisha pia ujenzi wa kuunganisha vituo vyetu vyote vilivyopo katika ya jiji, vituo vya city centre, Kariakoo, Stesheni, Sokoine pamoja na Ilala na hivyo kufanya kuwepo kwa mfumo unaosaidiana pale upande mmoja unapokuwa hauna umeme,”alisema Mramba.
Siku za hivi karibuni Tanesco walitoa taarifa ya kuomba kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.19.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI