Katibu
Mkuu Dkt.Servacius Likwelile akiwa na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Nd. Gabriel Negatu katika
Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ecobank Jijini Kigali Rwanda.
Waziri
wa Fedha Mh.Saada Mkuya Salum akiwa na baadhi ya wajumbe wa mkuatno
mkuu wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika uliofanyika Kigali Nchini
Rwanda.
Mh.Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akijadiliana jambo na mmoja wa washiriki wa Mkutano
wa 49 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unafanyika Kigali Rwanda. Pembeni ni mwa
Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile na msaidizi wa
Waziri Bw. Thomas Mabeba.
Mkutano Mkuu wa 49 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
umemalizika Jijini Kigali,Rwanda kwa Viongozi wa Benki kuahidi kujenga Afrika
ambayo ni itakuwa na Umoja,mshikamano na yenye miundombinu ya uhakika.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika,Dkt. Donald Kaberuka
amesema Benki itasaidia utekelezaji wa mipango bora ambayo itatokana na
majadiliano yatakayofikiwa kwenye vikao nchi wananchama. Miongoni mwa
vipaumbele vya benki kwa kipindi cha miaka kumi ijayo ni kujenga mazingira ya
kuwa na uchumi imara na endelevu,usimamizi wa maliasili za bara la Afrika na
ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha zaidi wanawake na vijana katika ukuaji wa
uchumi wa bara la Afrika.
Katika kuhakikisha maendeleo ya Bara la Afrika
yanafikiwa kupitia Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kipindi cha miaka 50 ijayo
ni pamoka na kusimamia utekelezaji wa
mpango wa ‘Afrika 50’ ambao utapelekea kuongeza ufadhili wa kiasi cha Dola
bilioni 100 ambazo zinahitajika katika kuimarisha miundombinu ya Bara la
Afrika.
Awali katika mkutano uliofanyika kati ya Mkurugenzi wa
AfDB kanda ya Afrika Mashariki Nd. Gabriel Negatu na ujumbe wa Tanzania, Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile aliishukuru benki kwa jitihada
zake za kuhakikisha Tanzania inatekeleza kwa ufanisi miradi yote inayofadhiliwa
na Benki hiyo. ‘Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Barani Afrika ambayo
inanufaika na fedha kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika,kwa sasa tuna zaidi ya
miradi 31 ambayo inatekelezwa na AfDB’ alisema Dkt.Likwilile.
Mwishoni mwa Mkutano wa Magavana wa Benki,Pia
walipitisha kuanzishwa kwa ‘Africa Growing Together Fund (AGTF)’,na kiasi cha
dola bilioni 2 zitatolewa na china ili kuwezesha AfDB kukabiliana na kuongezeka
kwa mahitaji ya kikanda kwa nchi wanachama wa benki na wateja wa sekta binafsi.
Mkutano ujao wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika
utafanyika Jijini Abidjan,nchini Ivory coast ambayo pia itakuwa mwenyeji wa
maadhimisho ya miaka 50 ya benki ya maendeleo ya Afrika yatakayoadhimishwa
Novemba,2015.
0 comments:
Post a Comment