Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAGONGA
Nyundo wa jijini Mbeya, Mbeya City fc jana walitoka nyuma na kushinda
mabao 3-2 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi katika mchezo wa kundi B
wa michuano ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea mjini Khartoum nchini
Sudan.
Mbeya
City fc waliofika Khartoum siku moja kabla ya mechi walianza kufungwa
bao katika dakika ya 10 baada ya Rashid kumtungua kipa wao, lakini
walirudi mchezoni baada ya Paul Nonga kusawazisha bao hilo dakika 5
baadaye.
Dakika ya
27, nahodha wa Mbeya City fc, Mwegane Yeya kama ilivyo kawaida yake
alifunga bao la pili kwa njia ya kichwa. Them Felix `Mnyama`
alihitimisha karamu ya mabao dakika ya 37 baada ya kufunga bao safi na
kuwapeleka Mbeya City mapumziko wakiwa na furaha.
Kipindi cha pili, Waburundi walikuja na Presha kubwa na katika dakika ya 68 Manirakiza alifunga bao la pili.
Kocha wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi aliwapongeza vijana wake kwa ushindi na kuahidi kufanya vizuri mchezo unafuata.
"Vijana walipunguza kasi kipindi cha pili, lakini nawasifu kwa kuvuna pointi tatu muhimu". Alisema Mwambusi.
Mpinzani wake, Ndayizeye Jimmy aliwapongeza Mbeya City kwa soka safi.
Wafungaji wa mabao: Academie Tchite: (Rashid Patient-10’, Manirakiza 68’).
Mbeya City: (Nonga paul-15’, Mwagane Yeya 27’ and Themy Felix 37’).
Mchezo
mwingine ulipigwa kuanzia majira ya saa 2:00 usiku na kushuhudia AFC
Leopard ya Kenya ikiibuka na ushindi mabao 2-0 dhidi ya Etincelles.
0 comments:
Post a Comment