Saturday, December 8, 2012

JIPANGE WOMEN GROUP YAENDELEA NA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI


SUALA la elimu ya Ukimwi nchini limetakiwa kutiliwa mkazo kutokana na ugonjwa huo kuendelea kuwa tishio kwa wananchi wengi wa Tanzania.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jipange Women Group Bi. Janeth Mavinza wakati wa kutoa huduma ya kupima Ukimwi eneo la Ujiji lililopo Mwananyamala, jijini Dar es salaam.
Bi. Janeth Mavinza Mwenyekiti wa Jipange Women Group akiongea na waandishi wa habari katika eneo la ujiji, Mwananyamala, jijini Dar es salaam.
Bi. Janeth Mavinza amesema licha ya wanawake hao kujishughulisha na ujasiliamali, pia wanatoa msaada wa upimaji Ukimwi kwa hiari.

Kikundi hicho cha Jipange Women kina asili ya VICOBA ambapo kimewakutanisha akina mama wajasiliamali ili kuleta maendeleo ya kijamii.


Badhi ya wananchi waliojitokeza kushiriki katika mchakato huo
Bi. Frola Mwakajinga - Katibu
Bi. Frola Mwakajinga kama katibu wa Jipange Women Group akaeleza umuhimu wa jumuiya hiyo, huku akisisitiza wanawake kujiunga pamoja na kutatua matatizo yao kupitia vikundi mbalimbali wanavyoviunda, lakini kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii.

Wananchi nao walijitokeza katika kupata huduma hiyo ya kupima kwa hiari huku wengi wakizitaka taasisi nyingine za Afya kutoa huduma hiyo kwa watu waliopopembezoni mwa mji kutokana na ukweli kwamba katika maeneo hayo huduma hii ni duni sana.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI