Saturday, December 17, 2016

PRINCE HARRY NA MPENZI WAKE MEGHAN MARKLE WAONEKANA PAMOJA KWA MARA YA KWANZA

MAISHA ya uhusiano ya Prince Harry wa Uingereza yamekuwa yakifuatiliwa kwa muda sasa huku akidaiwa kuwa na uhusiano na muigizaji Meghan Markle. Na usiku wa Alhamis hii, wawili hao walionekana hadharani na kupigwa picha kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja jijini London.
Wawili hao walionekana wakiwa karibu kwenye mtaa ulio na watu wengi zaidi jijini humo, Shaftesbury Avenue wakitembea kwa mguu kwenda kwenye jumba la sinema la Gielgud Theatre huku wakifuatwa nyumba na mlinzi wa kifalme.
Tovuti ya The Sun imeandika kuwa walinunua tiketi za mwisho kwenda kuangalia mchezo wa The Curious Incident of the Dog in the Nighttime.
Watu wa karibu wamedai kuwa wawili hao wanapendana sana. Meghan ni muigizaji maarufu wa filamu nchini Marekani. Amekuwa akiishi na Harry, 22 kwenye nyumba iliyopo kwenye viwanja vya ikulu ya Kensington.
Meghan ni maarufu kwenye series ya Suits.


0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI